Salaam, shalom!!
Twende haraka kwenye mada, nimekuwa nikipost mada za intelligence ya Mbinguni katika jukwaa hili na zinahamishiwa majukwaa mengine,
Leo tuanze mwaka na swali hili, Je vipofu wa Kuzaliwa huota ndoto?
Kurahisisha upatikanaji wa jibu kuhusu ndoto za vipofu, tupate tafsiri ya
1. Silver cord/ Kamba ya Fedha. 2. Mtu 3. NAFSI 4. Mwili. 5. NDOTO. 6. ULIMWENGU WA ROHO.
1. SILVER CORD/ KAMBA YA FEDHA.
Hiki ndicho kiunganishi kati ya MWILI wa mtu na Roho. Inapatikana katika ( Mhubiri 12:6): Or ever silver cord to be loosed. Ukisikia mtu amekata Kamba, ndo hii silver cord.
2. MTU.
MTU- Ni ROHO, ANAYO NAFSI NA ANAISHI NDANI YA MWILI.
3. NAFSI./ Soul.
Mwili/ udongo ulipopuliziwa Pumzi ya uhai, ikazaliwa NAFSI. Ikumbukwe, Pumzi ya uhai ndiyo Roho.
NAFSI ndiyo inayobeba hisia, akili, uwezo wa kufanya maamuzi. Hapa ndipo panapochakata taarifa Kutoka kwenye Mwili na Kutoka kwenye Roho( mtu). Kumbuka hisia, akili, will vyote havishikiki katika mwili physical bt vipo.
4. MWILI.
Hili ni frame, kopo, vazi la mtu ambaye ni ROHO. Mwili Si mtu, Bali mwili ni vazi la mtu ambaye ni ROHO.
Ukienda msibani, utasikia tunaenda kuaga mwili wa marehemu, marehemu na mwili ni vitu viwili tofauti.
5. NDOTO - Ni tukio halisi Si illusions kama wanasayansi wengi wanavyodhani. NDOTO ni tukio linalofanyika katika Ulimwengu wa Roho wa mwili au katika Ulimwengu wa Roho.
NDOTO type 1- Hizi ni za Kutoka kwenye Mwili kupitia macho na mawazo ndizo ziitwazo ndoto kulingana na shughuli za Kila siku.
6. ULIMWENGU WA ROHO.
Kwakuwa mtu ni ROHO anayo NAFSI na anaishi ndani ya MWILI, anapata na kutunza taarifa zote katika kitu kinachoitwa NAFSI.
Matukio yanayotengenezwa katika Ulimwengu wa mwili, NAFSI itayachakata na utayaota kupitia akili iliyo ndani ya NAFSI.
Matukio yaliyotokea kwenye Ulimwengu wa Roho, ,utayapata sababu silver cord imeungwa na mwili, NAFSI itakuletea tukio Hilo halisi kupitia ndoto, na ndoto zote ziko katika Ulimwengu wa Roho wa Nuru au Giza.
NDOTO type 2.- Hizi ni Kutoka katika Roho, ndizo ndoto ambazo ni taarifa Kutoka Ulimwengu wa Roho, ni tukio halisi, ndoto za aina hii ni HALISI.
Hivyo mtu kipofu, ikiwa Yeye ni ROHO, tutakuwa kwenye nafasi nzuri kujua ikiwa anaota ndoto au la. Na ikiwa anaota, ni Kwa mfumo upi?
Cc:
Sea Beast
Karibuni🙏