Unacheka kwa dharau unahisi una akili nyingi sana kuliko jamaa, sio!?
Kabla hajafunga macho kuwaza ghorofa, kumbuka huyu mtu ameshawahi kuliona ghorofa, pia kabla hajafumba macho kuwaza rangi ya gold, kumbuka ameshawahi kuiona gold na anajua rangi ya gold inafananaje. Kwahiyo atakavyofumba macho kuwaza, picha itakayokuja ni muunganiko wa vitu ambavyo ameshawahi kuviona (ghorofa na rangi ya gold). Kabla kipofu hajavuta picha au kuliota ghorofa la gold, unaweza kumuelekeza kipofu rangi ya gold ipoje?
Hivyo basi, kwa mtu ambaye macho yake yanafanya kazi sawasawa kuna mahusiano makubwa sana kati ya ndoto na vile alivyowahi kuviona katika maisha yake.
Kama wewe sio kipofu au ni kipofu lakini umeshawahi kuwa na macho yanayofanya kazi, yaani umeshawahi kuona, basi ndoto nyingi utakazokuwa unaziota kwa kiasi kikubwa zitakuwa na mahusiano na vitu ulivyowahi kuviona katika maisha yako.
Jibu langu kuhusu hii mada, vipofu wanaota, ila ndoto zao hazina mahusiano na macho(vitu walivyowahi kuviona), ndoto zao zinashirikisha ubongo(kumbukumbu) na milango mingine ya fahamu.