Je, wa-aborigine wa Australia wana asili ya Tanzania? Ni wazaramo, wasambaa au wamakonde?

Mkuu kama ulivyosema ni milion nyingi iliyopita(continental drift theory),kwa mujibu wa bwana Alfred Wegner,kinachofanana katika sehemu hizo za pwani ni mazingira(hali ya hewa na uoto wa asili)na labda mijusi na kenge wanaopatikana sehemu hizo.
 
Mkuu umenikumbusha mbali kweli. Yeah hapo kuna theories mbili kwenye geography A level which are continental drift na plate tectonic. Ukiangalia uoto wa asiri pwani ya afrika magharibi na east part ya south america zinafanana na hata watu wa maeneo hayo asiri zao ni moja. Hata umegukaji wa haya mapande mawili ya ardhi yanashabihiana.
Evidence nyingine ni uwepo wa bonde la ufa lililoanzia Middle East jordan huko likapita pande za Egypt hadi East Africa mpaka mto Tanganyika kuelekea kusini mwa Tanzania pande za Mbeya. Vitu ni vingi na vyote vinaelezea kuwa miaka milioni ya mamilioni iliyopita pande la ardhi lilikuwa moja.
 

Wakuu lumanyisa, Kituko, and mjasiria,
Hivi ni utafiti gani umeweza kusema beyond reasonable doubt kwamba mwanadamu wa kwanza aliishi duniani miaka X iliyopita na continental drift ilitokea miaka Y iliyopita? By the way, kama nilivyotangulia kusema hapo awali, mie sina ufahamu wa kutosha wa historia ambayo niliibwaga nikiwa kidato cha pili! Tell me am wrong here, kwamba kwa historia ile ya form II, tunaambiwa madai kwamba kufahamu mwanadamu wa kwanza aliishi miaka mingapi iliyopita, inatokana na kufanya utafiti katika masalia ya biandamu. Masalia haya ni yale yaliyogunduliwa; kwamba provided the oldest discovered fossils yatakuwa ni yale ya miaka 50 million iliyopita, basi hapo ndipo wataalamu watasema mwanadamu wa kwanza aliishi miaka 50 million iliyopita! If that is the case, kuna uhakika gani kwamba hakuna masalia ya kale zaidi kuliko hayo ya 50 million years ago?

Look here; jana, 18.03.2014, vyombo mbalimbali duniani vimetangaza ufahamu mpya kuhusu ni lini hasa kansa ilianza! Ufahamu huu mpya umetokana na masalia ya mwanadamu yaliyogunduliwa recently na baada ya kufanyiwa uchunguzi, ikaonekana kwamba mifupa yake ilikuwa imetoboka toboka na kutoa uwezekano mkubwa kwamba huyo mheshimiwa alikuwa anaumwa kansa!! Sasa basi, ikiwa tunalazimika ku-conclude kwamba mwanadamu wa mwanzo aliishi 50 million years ago kwa kuangalia masalia husika, what if kuna masalia ya miaka 200 million iliyopita lakini bado hayagundulika?4

In addition to that, ikiwa wataalamu hao wanaamini by the time of continental drift tayari kulikua na baadhi ya wanyama na mimea; and bila shaka na samaki, itashindikana nini basi kuwapo mnyama jamii ya mwanadamu? Hivi ni kwmba wakati wa continental drift hapakuwa na mwanadamu au there's no eveidence kwamba mwanadamu alikuwapo? Ikiwa ni kwamba there's no evidence in the existence of human life, this's different to there's no human life!

Mkuu Kituko umesema blacks wa sehemu kama Papua New Guinea and the like, uwepo wao kule umetokana na human migration. Hapa nimeuliza swali ambalo bado sijajibiwa! Ikiwa ni result of human migration, what' was the motivation of their migration? migrated from where? why did them had to risk their lives and migrate throughout islands?
 
Last edited by a moderator:

sawa kabisa mkuu.Tutazame fiziolojia ya binadamu tunayemuita wa kale zaidi.in some aspects anataka kufanana na primates.kwenye feeding mode,residence na mambo mengine.iwapo tunaamini kuwa binadamu wa kale amepitia badiliko toka kwa wanyama wenye jamii ya sokwe basi ukweli hautupeleki kuwa binadamu aliishi miaka million 150 iliyopita.ikiwa alikuwepo wakati huo aliishi wapi na alikuwa na umbo lipi.

sababu kubwa zinazofanya tutawanye wanadamu katika makudi ni mabadiliko ya mwili pamoja na ubadilikaji wa shughuli zao.tunaamini kuwa primates wameanza kuishi 60 million years bc but badiliko la kuwa na umbo la binadamu inadate back kwenye 2.5 au 3 million years bc.hapa tunapata picha kuwa binadamu ni wajuzi tu hapa.ingelikuwa wapo tangu zamani ingejulikana.mbona tunajua kuwa amphibians wameishi kuanzia miaka 360 millions bc.

uthibitisho huo unadhihirisha hata primates hawakuwepo wakati wa continental drift.ikiwa primates hawaitwi binadamu bali binadamu alitokana nao.basi suala li wazi kuwa bianadamu hakuwepo wakati huo.
 
Last edited by a moderator:
Nikipata nafasi nitaichangia thread hii; ni kati ya topics ambazo ninapenda kuzichangia kwa makini ila kwa sasa nitaiweka kiporo ili niendelee kufuatilia mijadala ya katiba.
 
 
Last edited by a moderator:
 
Last edited by a moderator:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…