Je, Waandishi wa Habari Wako Tayari Kukabiliana na Upotoshaji?

Je, Waandishi wa Habari Wako Tayari Kukabiliana na Upotoshaji?

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mwezi Disemba, 2024 ulichapishwa utafiti katika jarida la communication studies in Africa, uliohusu waandishi wa habari wa Tanzania katika kupambana na taarifa Potofu.

Katika waandishi wa habari 306 walioshiriki katika utafiti huo 51% ya waandishi walisema hawajawahi kupatiwa mafunzo rasmi ya kukabiliana na taarifa potoshi ambapo hii ni tatizo, kwa sababu linawaacha waandishi bila ujuzi wa msingi wa kusaidia jamii kupata taarifa sahihi. Bila mafunzo, ni rahisi kusambaza taarifa za kupotosha bila kujua.

Aidha kwa waandishi wa, Online/Digital Media – 64% walieleza kuwa na mafunzo ambapo ndio wanaoongoza kwa kupokea mafunzo hayo.

📺 TV – 53% Zaidi ya nusu ya waandishi wa televisheni wamepata mafunzo, lakini bado kuna uhitaji zaidi ili kuongeza ubora wa taarifa wanazotoa kwa umma.

📻 Redio – 50% Nusu kwa nusu. Kwa kuwa redio ni chanzo kikuu cha habari vijijini na kwa watu wengi wa kawaida, hili linaonyesha umuhimu wa kuongeza mafunzo kwa watangazaji wa redio ili kusaidia kupambana na upotoshaji vijijini.

📰 Magazeti – 32.7% tu wamepata mafunzo, Hii ndiyo kundi lililo nyuma zaidi. Ina maana kuwa karibu waandishi watatu kati ya wanne wa magazeti hawana elimu rasmi ya kutambua fake news. Hii ni hatari hasa ukizingatia kuwa magazeti bado yanaaminika na kusomwa na watu wengi.

🤔 Kwa Nini Haya Yote Ni Muhimu?
Taarifa potofu si jambo la kawaida tu zinaweza kusababisha madhara makubwa, kuharibu uchaguzi, kuchochea vurugu, kusambaza hofu isiyo ya lazima, au hata kuhatarisha maisha ya watu (mfano kwenye taarifa za afya au usalama).

Waandishi wa habari wakiwa hawana mafunzo sahihi, kuna uwezekano mkubwa wa wao wenyewe kuchangia kusambaza taarifa zisizo za kweli kwa bahati mbaya au kwa kushindwa kuchambua vyanzo vyao vizuri.

Mafunzo ya uhakiki na uthibitishaji wa taarifa yanawapa waandishi silaha muhimu kujua jinsi ya kuhakiki taarifa, kutambua vyanzo feki, kuchambua ushahidi, na hatimaye kuandika kwa uaminifu na weledi.

Kupata jamii yenye taarifa sahihi, basi tunahitaji kuwawezesha waandishi wa habari kupata maarifa sahihi pia.
 

Attachments

90% of all media outlets are controlled. We listen, watch and told what they want us to know, not what's actually happened.
 
Back
Top Bottom