Je, Wabunge hutumia vipi vipato vyao? Inakuaje Mbunge baada ya miaka 10 bado njaa inamuendesha?

Je, Wabunge hutumia vipi vipato vyao? Inakuaje Mbunge baada ya miaka 10 bado njaa inamuendesha?

Kwani hela mtu anaridhika nayo. Ingekuwa hivyo kina Abood, Shabiby, Chenge wangestaafu zamani sana.

NB: Halafu nakushangaa mwanaume unajisifia pato la 1.5 m. Ebo, hiyo si hela ya bata tu wikiendi!
Mhhh 1.5m bata? Sio kipindi hichi cha mkulungwa wapo wachache Sana walio baki na life style hiyo nao wanaogopa Lusitania
 
Kufuatia sakata hili la 19 ambalo ni wazi inaonesha msukumo wake ni njaa ya mapesa na anasa za ubunge, nachelea kuhoji sasa hawa Wabunge wetu wanapanga vipi bajeti zao kutokana na mapesa wanayolipwa?

Fikiria mtu kama Halima, miaka 10 ya ubunge lakini anakuja kuishia kujimaliza kisiasa kwa sababu ya njaa na tamaa ya mapesa ya ubunge. Unajiuliza mtu kama huyu aliyedumu kama Mbunge kwa miaka 10 namna yake ya kuhifadhi akiba ya pesa ina nidhamu kiasi gani?

Mimi napata net income ya 1.5M na kwa mwezi naweza na ninafanya hivyo, naweka angalau 600k kama akiba na mpaka sasa nina mapesa mengi tu naweza kumkopesha Halima.

Sasa Halima ushapoteza uanachama. CCM wanakutumia kwa miaka hii mitano tu. Je, 2025 CCM hawatakutaka tena, itakuaje?

Tujadiliane hapa, hawa Wabunge wetu wanatumia vipi pesa zao ikiwa mtu kama Halima aliyetumika bungeni miaka 10 bado amefanya kitendo hiki cha aibu ya njaa?

Halima amekuwa mbunge kwa miaka 15 mfululizo ndugu. Alijisahau kwa kujiona ni wa daraja fulani, ambalo anajua fika hawezi kulifikia bila kuwa mbunge, maana hana ujanja wa utafutaji kuweza kupata hela hiyo nje ya ubunge. Nakuhakikishia Halima hana uwezo wa kutengeneza milioni 3@month kwani hiyo kazi ya ubunge ni kama imemlemaza, ndio maana akaamua kujitoa ufahamu.

Ningemshauri kama aliutaka sana ubunge angeenda mahakamani kudai kura zihesabiwe upya za jimbo la kawe na sio hi viti vya mbeleko. Huko angeupata ubunge bila kujidhalilisha kama alivyofanya sasa. Kilichofanyika kwenye uchaguzi ule tulikiona na kama mahakama itafanya kazi yake, uchaguzi huo utatangazwa ni batili.
 
Kwani hela mtu anaridhika nayo. Ingekuwa hivyo kina Abood, Shabiby, Chenge wangestaafu zamani sana.

NB: Halafu nakushangaa mwanaume unajisifia pato la 1.5 m. Ebo, hiyo si hela ya bata tu wikiendi!

Acha mbwembwe za kitoto ww, 1.5 ni hela ya Bata wikiendi moja tu, sio kwa biashara halali labda kama unauza unga. Hivi unadhani unaongea na mazoba wasiojua lolote?
 
Mshahara wa mbunge hauna uwezo wa kukopeshwa mil 600.
Ubunge ni miaka 5 (miezi 60). Mil 600 maana yake arudishe mil 10 kwa mwezi jumlisha na interest. Mshahara hauwezi kutosha.

In 2010 walikuwa wanakopeshwa mil 200 ambayo makato yake yalikuwa zaidi kidogo ya mil 4.

Ikifika kipindi cha kampeni, mil 50 inaweza kutumika kwa wiki mbili tu...
Yes ni kweli mshahara kama mshahara hautoshi ila jamaa wana mapato zaidi ya hayo,wengine wanakopesha hadi 800m Mkuu!! Rejea Mkopo wa Sugu wa Kujenga Hotel......Rejea kauli ya Spika kuhusu Deni la Lema.
 
Sawasawa, huyo mkopeshaji must be an irresponsible lender. Kuna harufu ya fraud kwenye ukopeshaji wa namna hii.
 
Kama yule wa babati amefungua mpesa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Yes Ukipata sehemu yenye Mzunguko mkubwa unapata faida safi tu ,Hata Humphrey polepole alikuwa na kibanda cha Mpesa Bahari Beach wakati anakaa kwa Shemeji yake.(Kipindi cha Ukawa kabla hajapata milungula ya CCM).
 
Kwani hela mtu anaridhika nayo. Ingekuwa hivyo kina Abood, Shabiby, Chenge wangestaafu zamani sana.

NB: Halafu nakushangaa mwanaume unajisifia pato la 1.5 m. Ebo, hiyo si hela ya bata tu wikiendi!

Hiyo ni hela yako ya bata kila weekend?!!--- ebo, wenzako hiyo ni ela ya bata kila siku.
 
Kufuatia sakata hili la 19 ambalo ni wazi inaonesha msukumo wake ni njaa ya mapesa na anasa za Ubunge, nachelea kuhoji sasa hawa Wabunge wetu wanapanga vipi bajeti zao kutokana na mapesa wanayolipwa?

Fikiria mtu kama Halima, miaka 10 ya Ubunge lakini anakuja kuishia kujimaliza kisiasa kwa sababu ya njaa na tamaa ya mapesa ya Ubunge. Unajiuliza mtu kama huyu aliyedumu kama Mbunge kwa miaka 10 namna yake ya kuhifadhi akiba ya pesa ina nidhamu kiasi gani?

Mimi napata net income ya 1.5M na kwa mwezi naweza na ninafanya hivyo, naweka angalau 600k kama akiba na mpaka sasa nina mapesa mengi tu naweza kumkopesha Halima.

Sasa Halima ushapoteza uanachama. CCM wanakutumia kwa miaka hii mitano tu. Je, 2025 CCM hawatakutaka tena, itakuaje?

Tujadiliane hapa, hawa Wabunge wetu wanatumia vipi pesa zao ikiwa mtu kama Halima aliyetumika Bungeni miaka 10 bado amefanya kitendo hiki cha aibu ya njaa?
Ww tangu umeaza kazi pesa zote za mishahara na posho bado unazo Mpaka Leo?
 
Usisahau bajeti ya kampeni. Kampeni ni bottomless pit. Mshahara wa mbunge ni wa kawaida sana ukiangalia lifestyle zao.
Kabisa na wakati huu chadema haikutoa ela yoyote kwa watu waliogombea majimbo so walitumia ela zao

Tena hata ziara za Lisu mikoani zilikuwa zinagharamiwa na wabunge wa majimbo husika
 
Kwani hela mtu anaridhika nayo. Ingekuwa hivyo kina Abood, Shabiby, Chenge wangestaafu zamani sana.

NB: Halafu nakushangaa mwanaume unajisifia pato la 1.5 m. Ebo, hiyo si hela ya bata tu wikiendi!
1.5m hela ya bata la weekend sio kwel
 
Hela haijawahi kutosha
Money is scarce..hiyo ni sifa ya pesa.
Mtawalaumu bure
 
Siasa ni mchezo, akitemwa anatafuta mlango mwingine wa kuingilia. Ni jibu la aliesema akitemwa baada ya miaka mitano itakuwaje!

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Kwani hela mtu anaridhika nayo. Ingekuwa hivyo kina Abood, Shabiby, Chenge wangestaafu zamani sana.

NB: Halafu nakushangaa mwanaume unajisifia pato la 1.5 m. Ebo, hiyo si hela ya bata tu wikiendi!
Usisahau wabunge wengi Wa ccm matajiri hukimbilia ubunge ili kuhalalisha biashara yao haramu.wasifuatiliwe,sio kwamba wanafata mshahara.
We mwenyewe uko ccm tu ili ukwepe kulipa kodi.
 
Mimi ni HR hizi kazi za muda mfupi siyo kazi kabisa maana zimewalemaza wengi kwa matumizi makubwa na kuishi maisha ya ghali sana, pesa inahitaji mzunguko wa kuingia na kutoka hata ni mapato madogo nikiasi Cha kujipanga na kujibana, Kuna kipindi watu walikuwa wanaacha nafasi serikalini wanakimbilia mgodini kulipwa pesa nyingi na NGO baada ya mkataba kuisha wanarudi nyumbani wanapoteza muelekeo kabisa, maana kazi za mkataba ni kazi za kutafutia mtaji tu Ila siyo ajira ya kufanya matumizi ya mtu mwenye kipato Cha juu.
 
Back
Top Bottom