Je, Wachagga na Wamasai ni ndugu moja?

Je, Wachagga na Wamasai ni ndugu moja?

hamna kitu.
Unataka kutuambia zile zisizoonekana na wamama wa Kichanga na vile vitambi kama gunia ndo maumbo ya wakushi na Wanilotiki??
Wachaga wako encircled na nilotes na cushitcs so inawezekana kuna genetic exchange kwa muda mrefu hadi kukatokea wengine wana non bantu features
 
Wachagga ni mchanganyiko kati ya banti na maasai na makabila mengine ,babu yangu alikuwa na ndugu zake wamaasai wa huko Kenya,Kuna kipindi walikuwa wanakuja ila tulipotezana nao,Kuna koo za kichaga ambazo Zina asili ya kimasai,Kila ukoo uchagani una asili ya chimbuko lake,koo nyingine zinatokana na wapare,wengine wakamba,wengine wataita,ila wamaasai wanamchanganyiko mkubwa zaidi kwa sababu hii,kulingana na deaturi za uchagani wakati wa vita ,haikuruhusiwa kujua watoto,wakati wa vita Babu zetu walienda maeneo ya Masai na kupigana nao,waliposhindwa wanawake na watoto walichukuliwa na kuja kuishi kwenye nchi ya uchagani kama watu huru,haikuruhusiwa kabisa kuua mtoto mdogo kwenye vita.Na jambo jingine Kuna wachaga wa huko machame,hawa waliona na wamasai na walikuwa na ushirika nao mkubwa
 
Nilikuwa nasoma kitabu Desturi za Wachagga, by S. J. Ntiro, 1953. Jisomee mwenyewe.

MLANGO WA 5

ASILI YA WACHAGGA

Wachagga ni kabila lenye mchanganyiko wa makabila mengi sana. Makabila haya yameingia katika nchi ya Kilimanjaro katika nyakati tofauti. Makabila mengi yameingia Kilimanjaro yakikimbilia mwinuko wa nchi ili yaweze kuwaepuka maadui wao. Makabila mengi yalivutwa na rutuba ya nchi. Kwanza walijenga nyumba zao porini, lakini baadaye walipanda milima na kushika mahali kulikokuwa na vyakula zaidi. Iliwapasa kuwaheshimu wakubwa wa nchi ili wawaruhusu kuingia katika nchi. Makabila mengine yaliwafuata watu waliokuwa wakiishi katika nchi kwa kusudi la kuwanyang'anya mali, kama ng'ombe, mbuzi, na kondoo zao. Mara kwa mara mapigano yalitokea. Wenyeji waliwakimbilia kwa mikuki na marungu kuwazuia wasichukue mali zao. Wakati mwingine makabila yaliyoingia yalishindwa na wenyeji, lakini wakati mwingine ilikuwa kinyume. Kwa ufupi, hizi ndizo sababu kubwa zilizovuta makabila mbalimbali yaliyoingia Kilimanjaro.

Lugha za Kichagga ni uthibitisho mmoja mkubwa wa kuonyesha kuwa asili ya Wachagga ni makabila mengi. Nchi nzima ya Kilimanjaro imegawanyika katika sehemu ndogo ndogo 22 za watu wasemao lugha tofauti za Kichagga. Maneno ya sehemu moja ni tofauti na maneno ya sehemu nyingine kwa namna wanavyotamka ijapokuwa mtu wa sehemu moja anaweza kuelewa asemayo mtu wa sehemu nyingine. Tofauti ya namna hii katika sehemu za kabila moja si nzuri kwa sababu ni rahisi kuleta matangamano katika nchi.

Sehemu kubwa ya asili ya kabila la Kichagga ni Masai. Masai ni watu wapendao ng'ombe. Waliingia Kilimanjaro wakapigana na wenyeji na kuwanyang'anya ng'ombe na mbuzi na kondoo: kila wakati Masai walipokuja ilikuwa vita. Wengi wa Masai walifukuzwa na kurejea maporini ambako wanaishi mpaka leo, lakini wengi wao walibaki katika nchi wakageuka kuwa Wachagga. Kupata wanawake lilikuwa kusudi lingine lililowafanya Masai kupigana na watu waliokaa Kilimanjaro. Baada ya vita ambazo Masai walishinda, waliwachukua wanawake mateka Masaini. Tangu zamani za kale desturi ya kuwavizia wanawake na kuwaiba inaendelea mpaka hivi leo kidogo kidogo maporini. Siyo kwamba Masai wanawatesa wanawake hawa ila waliwapeleka kuzidisha kabila lao.

Wasambaa, Wapare, Wameru na Wakilindi ni makabila yaliyoingia Kilimanjaro katika nyakati mbalimbali. Makabila haya manne yaliingia kwa upole na utaratibu kuliko Masai. Mpaka leo hivi Wapare wanaingia Kilimanjaro ya mashariki kwa wingi.

NB. Kitabu kinapatikana ndani ya maktabaapp

View attachment 2510854
Yawezekana kua na mwingiliano kati ya makabila yaliyo jirani.

Sina shaka hilo
ila pia katka wachaga pia kuna watusi wengi walijichanganya na kujiita wachaga,,, hii hipo hata uhayani ambako hofu yao kubwa ilikua kukataliwa maana watanzania waliwaogopa watusi hawakutaka wala kuwataka nchini kisa roho zao za mauaji hivo wengi leo hujiita wahaya,wachaga au waha.

Achana na nyie watusi wa kujiandikisha
 
Back
Top Bottom