Je, Waislam mtakubali kupandikiziwa figo ya nguruwe?

Kwani ni waislam pekee ndio wanaosema nguruwe haramu? Hujui nchi hii km kuna baadhi ya Wakristo pia.

Kwann uzi wako umeegemea kwa Waislamu tu.

Ikumbukwe kuwa kula nguruwe mtu wa dini yeyote kubwa katika hizi dini kuu, ni ulafi wake tu, kwakuwa vitabu vimeweka wazi kabisa kuwa nguruwe hafai kuliwa.

Isaya 65:4
[4]waketio kati ya makaburi, na kulala katika mahali pao pa siri; walao nyama ya nguruwe, na mchuzi wa vitu vinichukizavyo u katika vyombo vyao;

Kumbukumbu la Torati 14:8
[8]na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.

Kutumia kwa kuokoa uhai katika hali ngumu hii haina tatizo.

Maamuzi ni yako.
 
Sisi Waislam hatuna shida ya kupandikiza Figo la nguruwe wakati dawa zetu za asili zipo na zinatibu hayo maradhi ya kufeli kwa figo kwa muda wa siku 90 mgonjwa atakuwa amepona dawa ninaijuwa kwamgonjwa wa kufeli kwa figo anitafute mimi nipate kumtibia amradhi yake na atapona in-sha-Allah.
 
Kama mnamchukia nguruwe asiye na hatia, kwanini msijiulize busara na mantiki ya 'kuumbwa' kwake?
Enyi wagalatia msiokuwa na akili.
Ni nani aliyewaloga? Galatia 3:1

Unafahamu tofauti ya kilicho haramishwa na kilicho chukizwa?
Tumchukie nguruwe kwa sababu zipi? Kaiba au kadhulumu mtu au anaabudu sanamu km wengi humu?
Nguruwe ni HARAMU kumla.
Ndio maana YESU hakuwahi kula Nguruwe na Yale mapepo machafu aliyasukumia kwa Nguruwe.

Lkn hakuna binaadamu mwenye akili timamu AKAMCHUKIA NGURUWE.
Get some knowledge Son.
This world [emoji289] is very ugly place for morons.
 
Kama mnamchukia nguruwe asiye na hatia, kwanini msijiulize busara na mantiki ya 'kuumbwa' kwake?
BIBLIA YA ASILI YA AGANO LA KALE INASEMA.

Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu. Msile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao; hao ni najisi kwenu.

Mambo ya Walawi 11.7-8

Tatizo lote la nyie kula nguruwe kalileta Paulo. Mtu ambae alijipa utume , hakuwahi kumuona Yesu wala mwanafunzi yyt wa Yesu.

Huyu ndie aliyewaposha wengi wenu kwa kusema.

Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri; maana Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.

1 Wakorintho 10.25-26

Kwahio ukikuta mavi makavu.
Au zile ngozi za govi wanakusanyaga wale watindiga zinauzwa sokoni we KULA TU
Usiulize .

Sasa hapo ntamwambia nini uelewe?
 
Kula chakula kinachouzwa sokoni ni kula chakula kilichoruhusiwa na serikari kama ukipenda.

Mfano, miaka ya Nyuma serikari ilikataza kula nyama ya Mamba. Hapo wafuasi wa Kristo pia wanaambia waitii Serikali.

Miaka ya Karibuni Serikali imeruhusu kuvua Mamba kwa vibali na kula, basi hapo imeruhususiwa kula kwani Wataalamu wa afya wamejiridhisha kuwa ni nyama isiyo na madhara kwa Binadamu.

Hilo andiko ndio lilikuwa na maana hiyo.

Ndio maana huoni hivyo ulivyo andika vikiuzwa sokoni, hiyo ndiyo maana ya haramu.
Na sio lazima kula hivyo vyote vinavyo uzwa sokoni.

Hata Waislamu mnakula vyakula vyote vinavyo uzwa sokoni.

Kama unabisha nitajie hapa chakula gani kilichoruhusiwa kuliwa na Serikali na kinachouzwa sokoni ambacho Waislamu hamli ?
 
Hili jibu konki sana. Kula vs kutumiwa kama dawa/sehemu ya matibabu. Kuna watu imani zinawaharibu hata reasoning ndogo wanashindwa kuwa nazo. Asant sana kahtaan
 
Tofautisha kupandikiza kiungo na kula.Dunia nzima,awe muislamu,mkristo,Buda,asiye na dini,baniani,ni haramu kula nyama ya binadamu,lakini wanapandikizwq viungo vya binadamu mwenzake.
 
Tofautisha kupandikiza kiungo na kula.Dunia nzima,awe muislamu,mkristo,Buda,asiye na dini,baniani,ni haramu kula nyama ya binadamu,lakini wanapandikizwq viungo vya binadamu mwenzake.
ukila chakula huwa kinaenda wapi? Tuanzie hapo kwanza nisije kuwa najadili na wewe pasipokujua uelewa wako upoje
 

Inawezekana wakatoliki hao (Dr Leonardo Riella na Dr Nael Elias) wakishirikiana na asiyekuwa na dini (Dr Tatusa Kawai) wanafanya uchokozi kwa makusudi. Kuamua kutafiti matumizi ya figo za nguruwe badala ya figo za wanyama wengine kama mbuzi ni kuwatikisa waislamu na wasabato. Halafu mgonjwa akianza kupata nafuu anapewa bia moja ya kustimulate circulation!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…