Ukifuatilia mambo yaliyotokea pasipo uwepo wa mwanadamu aliyeshuhudia hata mmoja utaishia kuwa kichaa kama sio mwokota zege. Hebu nikuulize pia, ni kweli rangi za binadamu ni tofauti.
1. Unaweza niambia ni kwa nini Mungu hakuumba mnyama wa namna moja, mf simba tu. Si angewakilisha wanyama wote, au unaonaje?
2. Ni kwa nini ndani ya bahari aliweka samaki na viumbe wa namna tofauti tofauti? Kwa nini asiweke kiumbe mmoja tu(jamii moja).
3. Kwa nini hata ukiangalia rangi za jamii moja ya wanyama inatofautiana kulingana na mahali inakopatikana. Mfano, Tembo wa Afrika ni tofauti na tembo wa Asia.
4. Kwa nini hata katika miti kuna namna mbalimbali na sio namna moja?
Hivyo kama ilivyompendeza Mungu kuweka namna mbalimbali za wanyama, miti, ndege, samaki na viumbe vingine. Vivyo hivyo, ilimpendeza kuweka wanadamu wa rangi tofauti tofauti, pia wakiwa na vimo tofauti, na maumbo ya mwili yaliyo tofauti.