Je, wajua Adam na Hawa walikua rangi gani?

Je, wajua Adam na Hawa walikua rangi gani?

Mkalibari

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2012
Posts
659
Reaction score
399
Hili swali anae weza kulijibu atatusaidia pia kutwambia kwanini kue kuna mgawanyiko wa rangi za wanadamu kama asili yetu ni moja?

Weupe/wazungu
Wekundu/wachina/waarabu/wahindi
Weusi/waafrika

Pia kinacho changanya kabisa hawa weusi hawa wanaonekana kama hawana mahusiano ya kiasili na hizi rangi nyingine!

Ebu mnaofahamu mtueleze maana tumetafta sources mpaka tumechoka, kwenye imani tunaishia kuambiwa kua ndio mapenzi ya mungu ili tupate kufahamiana..

Karibu..
 
Walikuwa Weusi Sema Wewe Siyo Mfuatiliaji Wa Mambo Ndo Maana Haujui
 
Inawezekana Adam na hawa ni weupe mpaka kipindi cha nuhu. Baada ya gharika nuhu alipoendelea kuzaa kati ya watoto mtoto mmoja anaeitwa sham ndie anaelezwa na biblia kuwa alikuwa mweusi. Maanake watoto wengine rangi yao ni nyeupe. Mwingine aliitwa kushi , hata baadae wakushi walielezwa kuishi afrika hasa kazkazini.
 
Najua.

Nitumie hela kwa mpesa nikwambie

Manake burebure hala mkipata uprofeseri mnamatusi sana nyie lipia tu upate jibu swaaaaafi.
 
Najua.

Nitumie hela kwa mpesa nikwambie

Manake burebure hala mkipata uprofeseri mnamatusi sana nyie lipia tu upate jibu swaaaaafi.

Aya nshakutumia m-pesa tayari nipe jibu..
 
Inawezekana Adam na hawa ni weupe mpaka kipindi cha nuhu. Baada ya gharika nuhu alipoendelea kuzaa kati ya watoto mtoto mmoja anaeitwa sham ndie anaelezwa na biblia kuwa alikuwa mweusi. Maanake watoto wengine rangi yao ni nyeupe. Mwingine aliitwa kushi , hata baadae wakushi walielezwa kuishi afrika hasa kazkazini.

Inawezekana!!!?
 
Hili swali anae weza kulijibu atatusaidia pia kutwambia kwanini kue kuna mgawanyiko wa rangi za wanadamu kama asili yetu ni moja?

Weupe/wazungu
Wekundu/wachina/waarabu/wahindi
Weusi/waafrika

Karibu..

Ukifuatilia mambo yaliyotokea pasipo uwepo wa mwanadamu aliyeshuhudia hata mmoja utaishia kuwa kichaa kama sio mwokota zege. Hebu nikuulize pia, ni kweli rangi za binadamu ni tofauti.
1. Unaweza niambia ni kwa nini Mungu hakuumba mnyama wa namna moja, mf simba tu. Si angewakilisha wanyama wote, au unaonaje?
2. Ni kwa nini ndani ya bahari aliweka samaki na viumbe wa namna tofauti tofauti? Kwa nini asiweke kiumbe mmoja tu(jamii moja).
3. Kwa nini hata ukiangalia rangi za jamii moja ya wanyama inatofautiana kulingana na mahali inakopatikana. Mfano, Tembo wa Afrika ni tofauti na tembo wa Asia.
4. Kwa nini hata katika miti kuna namna mbalimbali na sio namna moja?
Hivyo kama ilivyompendeza Mungu kuweka namna mbalimbali za wanyama, miti, ndege, samaki na viumbe vingine. Vivyo hivyo, ilimpendeza kuweka wanadamu wa rangi tofauti tofauti, pia wakiwa na vimo tofauti, na maumbo ya mwili yaliyo tofauti.
 
Adam and Hawa ni hadithi za kusadikika hakuna ushahidi wa kuwepo kwa watu hao.Kama kuna mwenye ushahidi alete.
 
Sikatai kua kuna maswali mengi kama hayo ya species za mimea, wanyama na viumbe wengine, lakin kwa leo nimeamua kuanza na la binadamu kwa kua tumeambia sisi sote tumetokana na mwanadam mmoja, sina uhakika saana na viumbe wengine kwa asili zao lakini nna uhakika na asili ya mwanadam..
Alafu mkuu kufaham na kujua jambo si dhambi, inawezekena kukuwa hakuna jibu ktk stock ya bongo zetu lakini kuna watu wanaweza kua na majibu tena yenye logic ndio maana mimi sijaona sababu ya kujifunga kwenye kibox nikaona niulize.
 
Adam and Hawa ni hadithi za kusadikika hakuna ushahidi wa kuwepo kwa watu hao.Kama kuna mwenye ushahidi alete.

Nimeshajua mawazo yako yanatokea wapi, wewe utakua ni product ya upuuzi wa akina Charles Darwin walio sema babu zako walikua nyani na ukaamini..
 
binadamu wa kwanza kuumbwa na mungu alikuwa adam according to our bible but haijaonyesha alikuwa na rangi gani..hizo picha zinaozonyesha weupe walitengeneza wazungu walipotuletea hiyo dini..
according to bible history wanadam walipozidi kuongezeka duniani na kufanya maovu mungu akajuta kwann alimuumba binadamu akapanga kuwakatilia mbali bt nuhu pekee akapata kibali machoni pa mungu.baada ya gharika nuhu akabaki na watoto wake watatu shemu(mweuc),hamu(mwekundu) na japhet(mweupe).
 
Nimeshajua mawazo yako yanatokea wapi, wewe utakua ni product ya upuuzi wa akina Charles Darwin walio sema babu zako walikua nyani na ukaamini..

Wewe ni mmoja kati ya wengi ambao walisoma history lakini hawakuelewa kipengele hicho,hakuna mahala palipoandikwa binadam wa zamani walikuwa masokwe wala manyani.

Lakini wewe unaeamini kwamba kuna mtu sijui kitua ama nguvu ilikuumba kutokana na udogo unaweza kuwa wa ajabu sana.
 
Lazima, una evidence? Au unaandika andika tu alimradi umeandika.
Nipe proof wapi mweupe kazaa mweusi. Weusi wanazaa weupe, kuna albino kuna wanaija walizaa wazungu. You can google.

Op! black man was the first hue man, either created, transmitted or evolved, black came first. do not be deceived with religion.
 
Back
Top Bottom