Je wajua "cognitive interviews" za kiintelijensia

Je wajua "cognitive interviews" za kiintelijensia

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,278
Reaction score
956
Mwanasaikolojia Edward geiselman ni Miongoni mwa waliofanya tafiti nyingi sana kuhusiana na Cognitive interview ( mahujiano ya utambuzi ) katika chuo kikuu cha California . Njia hizi ndizo zinazotumika na mapolisi duniani hadi Leo, ingawa kuna maboresho.

Katika kusoma kwangu vitabu vya kada hii , nilikumbana na mambo very interesting .

Kuna kitu wanaita " cognitive load",,,, unapomuuliza maswali mtuhumiwa ,,, yaani unamuuliza swali anakakaa kwa muda kulitafuta kichwani jibu lake,,,,,. Wakati huo huo anajiandaa ,,,,,unaongeza mzigo mwingine wa swali , wao wanasema unampa " Mental energy". wakimaanisha ili aweze kufunguka zaidi ,,,, watoto wa mjini wanasema kutiririka.

Yote haya wanataka kumbaini muhusika na kumpelekea kukiri, huku wakimhoji kama rafiki na kwa upole na kama anataka chochote wakati wa mahojiano unaweza kumpa mfano sigara, kinywaji nk.

wao mbinu hii wanaita ( confession oriented method with distinctly parent tone).

Kuna mbinu nyingi wanatumia ili mradi wakutie hatiani . Kuna njia common sana ya kijasusi ya kumhoji mtu ukimuangalia mwili wake hasa macho.

Katika macho wanatafuta kumbukumbu yako na ubunifu wako , maana kuna watu wajanja duniani lakini kwa falsafa hii wengi wanafeli.

Katika Macho , Mtu yeyote akitaka kukumbuka kitu , Macho yake huenda kulia , wataalamu wa cognitive interviews wanaelewa ubongo wake wa kumbukumbu unaanza kufanya kazi. Anapoanza kufikiri ( thinking) , macho yake yanaenda juu kushoto hapo , yakiashiria utambuzi wa jambo katika ubongo wa kati ,,,,,,,na ndipo uongo na ukweli wanaupatia hapo huku wakiongeza maswali ya kukuchanganya , dhumuni lao wao wanakusoma mwili , wewe unapaparika na Maneno .

Wao wanaita ( Mental note of the suspect's eye activity).

Kuna mbinu nyingine ambayo hata watu wote huwa wanaitumia,,, inaitwa ya kiuandishi habari ( journalistic approach).

Kwa wale waliosoma uandishi habari utakumbuka...

ili uandike habari na iitwe habari lazima kuwepo,,,,,,,, 5W ( Five wai)

5W ,,,,,,ni maneno 5 kwa kizungu ambayo ni ( where, when what , who, why ) , wataalam wa journalism waliongeza ingine " How" .

Watafiti wanasema mtu mkweli huwa anatiririka na anatoa maelezo ya ziada katika mtiririko , ila Muongo au ambaye ni mtuhumiwa kweli na anataka kukwepa , anasimamia jibu lake la msingi .

Sasa kuna wakati nasikiliza haya majibu ya watu makini katika jamii , wanasema katika
"" jibu langu la msingi "". Je Majibu haya yanatusogeza katika ukweli

Tafakari , soma , Fanya tafiti

Be inspired and respired
 
Kuna watu wanaidanganya 'lie detector'lakini ukikutana na interrogator ambae ni specialist asee anakuchota akili unajikuta unaongea kila kitu kilaaaiiini kabisa
 
mkuu hao watu makini ktk jamii ndo watu gani..?
 
Vipi na wale watu ambao unawahoji alafu mwishoni wanakwambia bora uniue?
Huyu hana tofauti na anayeomba uhakika wa usalama wake kabla hajaongea kitu.

Lazima abembelezwe na approach ibadilike kabisa,mpaka aone kuna umuhimu wa kuendelea kuishi.
 
,
Dunia inaenda kwa kasi sana. Ngoja niishie hapa.
 
Kuna movie niliiona zamani vidogo ya 2pac inaitwa gang related kama sikosei kuna mtu alikuwa anaulizwa maswali nilipenda sana.

Wakati mwingine hiyo LIE DETECTOR haiitajiki sana ukikutana na wabobezi wa fani.
 
Back
Top Bottom