Emmanuel180
JF-Expert Member
- Dec 17, 2019
- 342
- 626
Je, Wajua?
Mara ya mwisho Bwawa la Mtera kufunguliwa ili kuruhusu maji yapungue ilikuwa 21/3/2020 na haikuwahi kufanyika hivyo toka mvua za El Nino mwaka 1997/98
Je, Wajua?
Ujenzi wa bwawa la Mtera ulianza enzi za Nyerere, mwaka 1970 na lina ukubwa wa 'catchment' kilomita za mraba 68000
Je, Wajua?
Wazo la kwanza la ujenzi wa Bwawa la Mtera lilikuwa ni kwa ajili ya kuhifadhi maji na kuyachepusha kwenda Bwawa la Kidatu ili yatumike kuzalisha umeme. Baadae ikaonekana iwekwe mitambo ili izalishe umeme Mtera bila kuathiri flow ya maji kuelekea Kidatu.
Je, Wajua?
Pale darajani unapopita kwenye bwawa ni kizuizi cha kuzuia maji ili yaingie kwenye njia maalum na yakazalishe umeme baadae yashuke mpaka Kidatu
Je, Wajua?
Mtera kuna 'Turbines' mbili tu zenye uwezo wa kuzalisha umeme Megawati 80 japo uwezo wa maji kwenye Bwawa ni kuendesha 'Turbines' zaidi ya nne. Kutokana na lilivyojengwa hakuna namna ya kuongeza mitambo mingine zaid ya kujenga bwawa sehem ingine
Je, Wajua?
Mtera kuna handaki lenye urefu zaidi ya mita 800 limechongwa kwenye mwamba na ndani huko kuna chumba cha mkata umeme(control room) na mitambo yote ya kuzalisha umeme na kuingiza kwenye 'grid' ya Taifa ipo handakini.Yaani maji yamepitishwa chini kwa chini mpk mitamboni
Je, Wajua?
Licha ya kuwa maji ya Mtera ndio tegemezi kwa Bwawa la Kidatu, Bwawa la Mtera linazalisha umeme kiasi kidogo Megawati 80 kulinganisha na Bwawa la Kidatu MegaWati 200
Je, Wajua?
Kuanzia saa 10 mpaka saa 4 usiku ndio 'Peak Hour' yaani muda ambao Watanzania wanakuwa na matumizi ya umeme ya makubwa sana.
Je, Wajua?
Umeme wa AC huanza kutumika hapohapo baada ya kutengenezwa na ndio maana hauwezi kuhifadhika!
Je, Wajua?
Kigoma na baadhi ya sehemu mkoani Lindi haijaungwa kwenye umeme gridi ya Taifa, maana yake hata ikitokea hitilafu kwenye gridi ya Taifa kwenyewe umeme hautoathirika
Je, Wajua?
Je wajua zote hizi hazina picha kwasababu ni MARUFUKU kupiga picha maeneo ya Bwawa la Mtera kwenye mitambo na mifumo ya kuzalisha umeme.
Je, Wajua?
Mojawapo ya sababu ya kuzuia kupiga picha maeneo ya Bwawa la Mtera ni kulinda hakimiliki ya teknolojia iliyotumika kupatengeneza. Kuna kamera sehemu nyingi kiasi kwamba uwezekano wa kuonwa ukipiga picha hata ukiwa ndani ya gari ni mkubwa sana
Cc. imma