Je, wajua haya kuhusu bwawa la Mtera?

Je, wajua haya kuhusu bwawa la Mtera?

Hilo eneo la catchment mbona kubwa sana!! Kuzuia kupiga picha ni ishu za kizamani kabisa na ushamba, kama kuhamishia TV chumbani miaka hii. Waruhusu tu, pana potential kubwa ya utalii.
 
Pia naomba kuuliza. Ule ukuta unaozuia maji ya mto unaitwaje kwa kiswahili?
 
Umeongeza chumvi na wee au nimuite engineer wangu hap aje kutoa ufafanuzi
 
Sindio hapo ama?
Screenshot_20220211-195833_Maps.jpg
 
Hii ya mwisho ni chai
Ni kwel mzee 2014 Kuna mwamba tulikuwa nae kweny basi tukitoka jkt jamaa akapiga picha tumevuka tu daraja Gari ikasimamishwa private mmoja akaingia aka mfuata jamaa moja kwa moja akamwambia futa picha zote kweny smu kilicho tusaidi kutoka pale mapema ni sababu tulikuwa wote tumetoka mafunzoni kwaiyo Kuna kamera zina nasa mpak ndani ya Gari
 
Hilo eneo la catchment mbona kubwa sana!! Kuzuia kupiga picha ni ishu za kizamani kabisa na ushamba, kama kuhamishia TV chumbani miaka hii. Waruhusu tu, pana potential kubwa ya utalii.
mambo ya usalama mkuu sio iyo copyright aliyosema
 
Kuna msela wangu alikuwaga Apo alinambia mwamba uliochongwa ndani kwa urefu ni ghorofa 3
 
Dah umenikumbusha nilipiga picha nikiwa kwenye Basi nikitoka Iringa, mbele kwenye geti wakasimamisha basi Askari wa SUMA JKT akatangaza kuna mtu kapiga picha Ajisalimishe, dah nilikosa amani watu wote kimya konda naye akaanza kusema jamani aliypuga licha ashuke, huku askari ananikazia macho akaniuliza ni wewe nikamwambia hapana uzuri nilikuwa nikishafuta picha zote nikampa simu nikamwambia angalia huku mapigo ya moyo yakienda resi vibaya sana.

Mwisho wa siku wakaturuhu dah ilikuwa siku mbaya sana kwangu
Pole sana mkuu
 
Technology gani unayoisemea kiasi kwamba hautakiwi kupiga picha...?
Kipi kigeni haswa??
Watu wana ma rover yanatembea sayari ya Mars, watu wana fighter jet kalii zinakimbia zaidi ya mara 5 ya spidi ya sauti...
 
Hivi kuna uhusiano gani wa mahandaki na control room za power station maana nakumbuka zamani tulienda study tour kidatu na kule control room ipo kwenye mwamba uliopasuliwa, nakumbuka kuna lami kabisa magari yanaingia hadi ndani uko
 
Back
Top Bottom