Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Karibu Makala yangu ya "Kwa Maslahi ya Taifa" Jumapili ya Leo
Hii ni makala mwendelezo ilianzia hapa Je, jicho la Rais Samia litauangazia Ubatili huu ndani ya Katiba yetu unaopora Haki ya Msingi, uliochomekewa kibatili ili kuuhalalisha?
Kama kawaida yangu, kila Jumapili, huibuka na makala zangu za "kwa Maslahi ya Taifa"
Makala hizi huandikwa kwa mtindo wa maswali fikirishi.
Swali la makala ya leo ni "Je wajua kuna fupa fulani la dhulma fulani inayofanywa kwa Watanzania?. Fupo hilo la dhulma hiyo, liliwashinda Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli, , tena wote hao ni marais wanaume, wakitegemewa ni majabali, lakini fupa hili liliwashinda!. Rais Samia, japo ni rais Mwanamke, ameisha onyesha kwa kauli na matendo, yeye ni mpenda haki na mtenda haki kuliko hata marais waliomtangulia. Jee Mama Samia ataliweza fupa hili?.
Fupa lenyewe ni haki ya kuchagua na kuchaguliwa. Katiba yetu ya mwaka 1977, ilitoa haki sawa kwa kila Mtanzania kuchagua viongozi wake, yaani haki ya kupiga kura ni kwa Watanzania wote, na vivyo hivyo, haki ya kuchaguliwa pia ilitolewa kwa Watanzania wote, kupitia kugombea uangozi, haki hiyo ya kuchaguliwa ikaja kuporwa kwa kuchomekewa vipengele vilivyoipora haki hiyo.
Lengo la makala hii ni kuiangazia haki hii muhimu iliyoporwa ili jicho la haki la rais wetu Mama Samia liiangazie haki hii muhimu na kuirejesha kwa Watanzania.
Jee fupa hili lililowashinda watangulizi wake mijibaba, jee Mama ataliweza
Andamana nami katika makala hii.
Nakutakia Jumapili Njema
Paskali