Uchaguzi 2020 Je, wajua kuna watu wazuri, waadilifu wenye uwezo, wanaotaka kuingia Bungeni kulisaidia Taifa, Bunge na kumsaidia JPM kwa dhati, lakini kwa vile...

Watu wanaenda bungeni kuwakilisha wananchi na kuisimamia serikali lakini sio kumsaidia JPM. Bunge lililopita wabunge wa ccm walikua wanaogopa hata kuihoji serikali ,wamepitisha miswaha mibovu kama (takwimu,habari) huku wakijua ina mapungufu makubwa.

Hao waliopitishwa na wajumbe ndiyo ambao wameonwa na wananchi kama wakishinda ubunge wata wakilisha maslahi yao. Mfano Mzee mwakyembe ameshindwa kwenye kura za maoni kyela halafu apitishwe na makao makuu[emoji134]? Haitakua poa.
 
Paskali ulitaka uteuliwa bila kupigiwa kura na wajumbe,ambao ni wawakilishi wa wana CCM katika jimbo lako?

Siasa za Tanzania ni ulaghai,ujanja ,unafiki.Sasa wewe ulitegemea wanachagua Askofu au Sheikh?

Wakiteua viazi ,na kuwakata wanaochangamka watapigwa chini katika sanduku la kura.
 
Wakati ule unatuaminisha hauna chama tayari ulishaanza kuwa na mapenzi kwa CCM, ndio maana wengine tukawa wagumu kukuamini na ule msimamo wako.
 
Ni kweli kabisa! Achilia mbali na hao walio katika vyama ambao hawakupigiwa kura kabisa,Wapo ambao hawana hata chama lakini ni waadilifu ambao wanaweza kulisaidia Taifa letu.Nadhani ingekuwa muafaka kama Katiba ingefanyiwa marekebisho ili iruhusu Mgombea huru kwa nafasi ya Urais,ubunge na udiwani,huenda tunaweza kuwapata huko watu waadilifu.

Kwa sasa hivi watu waadilifu ambao wako tayari kulisaidia Taifa letu wako nje ya CCM kwenye Vyama vya Upinzani! Hasa wale waliokataa kununuliwa na kuwa tayari kuteswa, kufungwa, kupigwa na hata wengine kuuawa.
 
Kwa hiyo hivyo vyama vingine havina Imani inayovutia waadilifu na wazalendo kunifunga navyo?
Waadilifu wapo kote. Huwezi kunilazimamisha mimi kuwa Mkristo au kuwa Mwislamu wakati mimi siaamini huko. Kuwa CCM au kuwa CHADEMA au Kuwa NCCR ni imani na Mtu kugombea wapi ni imani yake.
 
..Did you do a serious campaign?

..uliwafikia wajumbe wote wanaopiga kura na kuwaeleza sera zako kabla ya siku ya kupiga kura?

..Tunapenda kukupa pole, lakini pia tunapenda kujua kama kuna jambo ulilojifunza, au wapi ulipokosea.
Yes I did.
Karibu.
P
 
Usikufuta uzi huu.
Uzalendo haupigiwi chapuo.
Ukiona mtu anajiita mzalendo ni fisi kwa siri
 
Kama kweli kuna watu waadilifu na wa maslahi ya taifa, watakumbukwa kwenye nafasi 10 za Wabunge wa kuteuliwa. Asilimia kubwa ya waliogombea ni wasaka vyeo tu, wazalendo ni wachache sana. Ndiyo maana tuhuma za rushwa zimetapakaa.
Nakubaliana nawe Wakili msomi. Zile nafasi kumi za uteuzi wa Rais ni ili kama anawatu ambao anadhani anataka wamsaidie lakini wenyewe hawakuingia kwenye mchakato wa kupigiwa kura au hata walioshindwa basi awateuwe wamsaidie kama alivyofanya kwa Dr Mpango Philip, Prof Ndalichako Joice na Prof Palamagamba Aidan Mwaluko.

Kwa afya ya demokrasia haifai kutamani Bungeni waende watu "watakaoweza kufanya kazi na rais". Hii haina tafsiri nzuri sana hasa katika siasa zetu ambazo zinachukulia critics kua ni antagonism!
 
Yes I did.
Karibu.
P
Mkuu Pascal,

Hivi wajumbe hasa wa CCM walikua wanahaja ya kusikiliza mipango na mikakati ya mgombea? Kwa taaluma yako unaweza kuelezea kama kweli kulikua na tofauti ya aina ya watu na malengo ya wagombea kati ya Chama Tawala na wale wa Upinzani? Namaanisha kiitikadi, Je kulikua na tofauti yoyote katika kunadi hoja?

Kama jibu hapo juu ni hapana huoni kama ilikua ni mashindano ya personalities na mlungula tu na sio kushindanisha hoja, mipango wala mitazamo ya kimawazo?
 


Mayalla kapata kura 1 kura za maoni ,mwambieni tu ukweli kua bunge ataendelea kuliona kwenye Tv.
 
Mayalla kapata kura 1 kura za maoni ,mwambieni tu ukweli kua bunge ataendelea kuliona kwenye Tv.
Wakuu wa Chama wanasema anaweza akateuliwa hata aliyepata kura sifuri kutoka na ripoti za uchunguzi kwenye chaguzi za kura ya maoni

Jambo la kuzingatia; wale ambao kuna fununu kwmba ni chaguo la "nambari one" basi wote wamefanyiwa kampeni za nguvu na nyingine chafu ikiwemo kutembeza bahasha na wameongoza kwenye kura za maoni. Naambiwa eti Kawe ni miongoni mwa majimbo husika!
 
You are questioning to the fundamental fact of democracy system

What I know the majority of people are stupid while only few are intelligent ones

And in order to win you need to win the majority and this is the meaning of "reality is conflictual "
 
Eti kukosoa kwa staha? Kila mtu aina yake ya kuwasilisha hisia zake,msitupangie
 
Usiogope Mayalla huenda jina lako likarejeshwa ulingoni na mwenyekiti wa chama chako (Ccm), muhimu kwako ni kuwa mvumilivu.

Isitoshe wewe unafahamika na wakubwa hivyo unaweza kukumbukwa muda wowote kama sio kwenye ubunge huenda ukateuliwa kuwa DED,DAS, RAS,RC, DC au hata balozi kama babu Slaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…