Lyaka Mlima Jr
JF-Expert Member
- Mar 24, 2020
- 361
- 521
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waadilifu wapo kote. Huwezi kunilazimamisha mimi kuwa Mkristo au kuwa Mwislamu wakati mimi siaamini huko. Kuwa CCM au kuwa CHADEMA au Kuwa NCCR ni imani na Mtu kugombea wapi ni imani yake.Kwa hiyo hivyo vyama vingine havina Imani inayovutia waadilifu na wazalendo kunifunga navyo?
Yes I did...Did you do a serious campaign?
..uliwafikia wajumbe wote wanaopiga kura na kuwaeleza sera zako kabla ya siku ya kupiga kura?
..Tunapenda kukupa pole, lakini pia tunapenda kujua kama kuna jambo ulilojifunza, au wapi ulipokosea.
Nakubaliana nawe Wakili msomi. Zile nafasi kumi za uteuzi wa Rais ni ili kama anawatu ambao anadhani anataka wamsaidie lakini wenyewe hawakuingia kwenye mchakato wa kupigiwa kura au hata walioshindwa basi awateuwe wamsaidie kama alivyofanya kwa Dr Mpango Philip, Prof Ndalichako Joice na Prof Palamagamba Aidan Mwaluko.Kama kweli kuna watu waadilifu na wa maslahi ya taifa, watakumbukwa kwenye nafasi 10 za Wabunge wa kuteuliwa. Asilimia kubwa ya waliogombea ni wasaka vyeo tu, wazalendo ni wachache sana. Ndiyo maana tuhuma za rushwa zimetapakaa.
Mkuu Pascal,Yes I did.
Karibu.
P
Nakubaliana nawe Wakili msomi. Zile nafasi kumi za uteuzi wa Rais ni ili kama anawatu ambao anadhani anataka wamsaidie lakini wenyewe hawakuingia kwenye mchakato wa kupigiwa kura au hata walioshindwa basi awateuwe wamsaidie kama alivyofanya kwa Dr Mpango Philip, Prof Ndalichako Joice na Prof Palamagamba Aidan Mwaluko
Kwa afya ya demokrasia haifai kutamani Bungeni waende watu "watakaoweza kufanya kazi na rais". Hii haina tafsiri nzuri sana hasa katika siasa zetu ambazo zinachukulia critics kua ni antagonism!
Wakuu wa Chama wanasema anaweza akateuliwa hata aliyepata kura sifuri kutoka na ripoti za uchunguzi kwenye chaguzi za kura ya maoniMayalla kapata kura 1 kura za maoni ,mwambieni tu ukweli kua bunge ataendelea kuliona kwenye Tv.
Eti kukosoa kwa staha? Kila mtu aina yake ya kuwasilisha hisia zake,msitupangiePascal umeleta mada nzuri. Ni mada ambayo inakwenda na wakati huu tulionao.
Kwanza na mimi niseme wazi kabisa hapa kuwa nina maslahi na mada hii. Nilitia nia nyumbani kwetu na niliambulia kura "0". Kwa mazingira ya pale kwetu sikuona au kusikia tetesi za rushwa japo kwakusema hivyo haina maana ya mimi kudhibitisha kuwepo au kutokuwepo kwa rushwa. Hii ilinisukuma kuandika andiko hili:
Hongera sana CCM kwa mchakato wa kura za maoni
Kama ulivyoeleza, na mimi nilienda kwenye mchakato huu nikiwa na moyo wa dhati kabisa wa kuwatumikia watu wangu kwa nafasi hiyo. Kuhusu uadilifu, uwezo na uzoefu wangu, hilo sio jambo la kutilia shaka na wanaonifahamu wanajua hilo.
Niliandaa kipeperushi changu na kukisambaza kwa watu wangu wa karibu, punde katibu wa NEC - Itikadi na Uenezi ndugu Polepole akatoa onyo juu ya Jambo hilo. Haraka sana nikatii na kuwataka ndugu, jamaa na marafiki waache kusambaza kipeperushi hicho. Na hilo lilifanyika "with immediate effect".
Ndugu Pascal na wasemaji, baada ya hatua hiyo sikufanya tena aina yoyote ya kampeni wala sikutoa rushwa. Siku ya kujieleza kwa wajumbe ikafika, nikajieleza, mwenyekiti anauliza, " Kuna swali lolote kwa mgombea?" Wajumbe wakajibu kwa sauti moja "hakunaaaa". Nikatoka. Kura zikapigwa na zikahesabiwa wazi kwa kila mgombea kupewa kura zake. Kika zikitajwa, sitajwi mpaka mwisho.
Basi msimamizi wa uchaguzi akawa anaita mtia nia mmojammoja kupita mbele na kusema amepata kura ngapi. Akaita " Amani Msumari" nikapita mbele na kusema " ninawashukuru ndugu wajumbe, sijapata kura yoyote, nimepata sufuri".
Baada ya mchakato huo, moyo wangu umefarijika kwani nimefanya kile ninachokiamini. Nilifurahi zaidi baada ya wazee flani watatu kuniita na kuniambia " kijana umeongea vizuri Sana, wewe ni kiongozi mzuri Ila kwasasa umegombea na mtu ambaye sisi tunamuamini Sana na ni muhimu kwa Jimbo letu, Mungu hakutaka iwe kipindi hiki". Kwakweli nilifurahi Sana.
Kama hakuna rushwa, ni vigumu Sana kumrudisha mtu aliyepata kura sifuri kwani wajumbe walikuwa na sababu kwanini wasimpe kura. Cha muhimu ni kuwa tumepata ya kujifunza kwenye mchakato huu.
Pascal, mimi na wewe tunazo shughuli zetu zinazotuingizia vipato halali, tena vizuri tuu. Ushauri wangu ni kuwa tuendelee kuonesha uzalendo kwa kuitumikia nchi yetu na chama chetu kwa nafasi nyingine.
Binafsi nimejivika kuwa balozi wa kuyasema mema ya chama na serikali. Kukosoa kwa staha pale inapobidi na sikosolei humu mitandaoni. Sio lazima tuwe wabunge kwenye jitihada za kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele zaidi.
Amani Msumari
Tanga
Lazima kuwe na utaratibu bwasheeEti kukosoa kwa staha? Kila mtu aina yake ya kuwasilisha hisia zake,msitupangie