Je, wajua kuwa hatma ya CHADEMA ipo mikononi kwa Lwakatare? Baada ya CHADEMA kumwaga ugali, Lwaka akiamua kumwaga mboga, CHADEMA kwishney!

Mkuu Mshana Jr, kwanza heshima mbele, hakuna mtu yoyote anayeiombea Chadema ife, kosa langu ni kuwa mkweli too much.

Humu jf tuna members wa aina 3, tuna
  1. Simple minds, discuss people, wao badala ya kujadili hoja iliyo mezani, hawa watamjadili mtoa hoja.
  2. Ordinary minds, discuss events, hawa watadili matukio, nini kimetokea etc
  3. Great minds discuss ideas, hawa watajadili hoja iliyo mezani.
Hivyo naomba keep on being free, kujadili watu, matukio na hoja, katika mabandiko yangu, ukiweza kujibu hoja, nitashukuru, ila hata ukinijadili, sikulaumu na likes nakutwangia.
Ukipata muda karibu ujibu hoja za bandiko hili.

Asante
P
 
Update kuhusu angalizo la uchangiaji.

Japo jf was ment to be a home of great thinkers,
Lakini humu jf tuna members wa aina 3, tuna
  1. Simple minds, discuss people, wao badala ya kujadili hoja iliyo mezani, hawa watamjadili mtoa hoja.
  2. Ordinary minds, discuss events, hawa watadili matukio, nini kimetokea etc
  3. Great minds discuss ideas, hawa watajadili hoja iliyo mezani.
Mtu kuwa simple mind, ordinary mind na great minds ni the way one comprehend and thinking capacity, nimesema Lwakatare ameishika hatma ya Chadema mkononi mwake. Kwa vile Chadema wao wamemwaga ugali yeye akiamua Kumwaga mboga, Chadema keisha!.

Ma simple minds watamdiscus mleta mada, Pasco na Lwakatare, hivi na vile, sii lolote sii chochote, that is their level.

Ordinary mind wao wata discuss event ya Lwakatare kutimuliwa na atamwaga vipi mboga, atakakata tawi alilokalia etc.

Great minds wata discuss hiyo hatma ya Chadema, jee ni kweli ikijulikana Chadema kinakufa?, hiyo hatma yenyewe ya Chadema Lwakatare aliyo mayo ni nini haswa?, does have merits hadi Chadema ife, etc

Hivyo be free kujadili kwa kadri ya uwezo wako na kundi lako keep on being free, kujadili watu, matukio na hoja, katika mabandiko yangu, ukiweza kujibu hoja, nitashukuru, ila hata ukinijadili, sikulaumu na likes nakutwangia.
Ukipata muda karibu ujibu hoja za bandiko hili.

Asante
P
 
Naunga mkono hoja. Mara nyingi mtu akianzisha mada au kuchangia kitu ni watu wachache sana wanaoweza kuchangia hoja. Wengi wetu ni kuporomosha matusi nk. Hata huwa nafikiria kuwa sisi siyo 'critical/intelligent thinkers' maana hata hatujui namna ya kuchangia hoja, bali tukiona upande wetu unasifiwa tunaunga mkono na kama unakosolewa tunaporomosha matusi. Kufanya hivi siyo kujali hoja, bali ni kuonyesha ushabiki tulionao. Kuchangia hoja ni kujadili hoja, tena kwa lugha ya staha bila kumuudhi mchangiaji mwingine 'personally' bali ni kutiririka na kushusha points kama ilivyokuwa (enzi hizo) kwenye debates kama: jadili kuwa 'baiskeli ni bora kuliko kuwa na radio' - upande wa wanaoona kuwa na baiskeli ni bora watashusha points na upande wa wanaoona kuwa na radio ni bora watashusha points pia, na hakuna upande utakaoanza kuwatukana wa upande mwingine. Mijadala yetu yote inapaswa iwe hivyo.
 
Tangu mmeingia madarakani jitihada za kuiua chadema zimefanikiwa kwa asilimia ngapi hadi sasa? Umewahi kujiuliza baada ya wale wabunge wa cdm kuhamia ccm uchaguzi ukarudiwa ni kwanini militumia nguvu kubwa kiasi kile na kulazimisha kuwatangaza kuwa wabunge? imagine mbunge yuleyule akiwa cdm anapewa kura ila akihama tu anaacha kura zote cdm unajua ni kwanini? kwa sababu cdm siyo Mbowe wala Lwakatare bali ni wananchi. Angalia mnavyotumia nguvu kubwa hadi kubambikia watu kesi, hii dhambi mnayofanya ya kuwatesa viongozi na wafuasi/wanachama wa chadema au wapinzani wa ccm ndo inayowamalizeni, wananchi wanaona na wanajua kinachoendelea na hawapendi uonevu wenu. Kwa taarifa yako mnaweza kuamua kuwafunga jela viongozi wote wa cdm hadi wabunge na madiwani cdm ikakosa wagombea au mkaamua kukifuta chama kabisa na bado kwenye kura mkatumia nguvu ileile ya kulazimisha ushindi.
 
Hizi kauli za kutabiri kifo cha CHADEMA zimeanza siku nyingi, na zinatokana na watu kuweka mwendelezo wa "vifo" vya vyama vya upinzani hapa nchini, ukianzia na chama cha NCCR-MAGEUZI.

NCCR-MAGEUZI ilikumbwa na "ngumi" mfululizo za CCM na mwisho "ikafa". Kifo hicho kilitokea sambamba na kuporomoka toka chama kikuu cha upinzani, hadi kilivyo sasa hivi, chama chenye mbunge mmoja na ndie mwenyekiti. Lakini pia sasa hivi kinajinasibisha kama CCM B, sawa na mwelekeo wa TLP ambayo imefilisika kabisa, kiasi cha kumpitisha Magufuli kuwa mgombea urais. Lakini hii ni "biashara" kama ambavyo mwenyekiti wake, Lyatonga Mrema, ameiita.

CUF, chama kilichoirithi NCCR-MAGEUZI kuwa chama kikuu cha upinzani, nacho kilipokea dozi kubwa ya "ngumi" za CCM, na kwa kweli tunaweza kusema nacho "kimekufa". Tofauti iliyopo hapa ni kuwa CUF haijafa, ila kuna MUTATION imetokea.

Kwanza ilitokea BINARY DIVISION, ambapo tulipata CUF LIPUMBA na CUF MAALIM. CUF LIPUMBA nayo ikawa CCM B, na CUF MAALIM ikaimeza ACT-WAZALENDO, na kubeba jina hilo katika hiyo mutation. Kwa maoni yangu, CUF MAALIM a.k.a. ACT-WAZALENDO, siyo rahisi kufa. Chama hiki kina viasili vinavyofanana na vile vya CHADEMA, na hivyo vyote siyo rahisi kufa.

Nasema siyo rahisi kufa, sijasema haiwezekani kufa.

CUF MAALIM ina CONSTITUANCE, ina watu ambao wamekula yamini kukilinda. Wanaangalia afya yake daima. Kina chimbuko katika mikinzano ya kisiasa huko Zanzibar. Pia kina misimamo imara ya upinzani. Hakiyumbishwi. Sifa hizi za mwisho zinakifanya chama chochote cha upinzani kuungwa mkono angalau na sehemu ya wananchi wa kawaida.

ACT-WAZALENDO kimeundwa ofisini, waliokiunda ni "waasi" kutoka CHADEMA. Kimsingi ACT haina Constituance, japo mwasisi mmoja, Zitto, amejaribu kuichomeka Kigoma kama Constituance ya ACT. Muasisi mwingine, Kitila Mkumbo, "aliasi" tena mara ya pili na kumwacha Solemba Zitto. Chama cha aina hii, chenye viasili vinavyofanana na vile vya NCCR-MAGEUZI, ni rahisi "kuuwawa".

Kabla ya "kuchinjwa", ACT imemezwa na CUF MAALIM, hapo tutarajie mabadiliko katika political landscape. CHADEMA na ACT ni heavyweights ambao wanahitaji kushirikiana.

CCM ya leo, ambayo huitwa pia CCM ya Magufuli, ilishaacha miaka mingi kuwa chama cha siasa. Ilishakufa kisiasa. Inapumulia mashine ya Dola. Magufuli alipoingia madarakani, ameigeuza kuwa SACCOS yake binafsi. Hata ile semblance tuu ya chama kama taasisi iliyokuwepo zamani, sasa haipo. Ushahidi kamilifu wa hili ni sakata la makatibu Wakuu wastaafu, Kinana na Makamba. Licha ya kuwa na misimamo binafsi, waliandika waraka ambao ungeweza kusaidia kuirejesha CCM kwenye reli. Lakini kwa kuwa CCM siyo taasisi tena, kauli zao binafsi ndio zikasikilizwa, na bila hata chembe ya aibu, zinarushwa hewani.

Hapakuwa na taratibu zozote za kitaasisi kuufanyia kazi waraka huo. SACCOS hii ya Magufuli, inaendeshwa kwa Majungu ya akina Musiba na wengine. Maamuzi yaliyotolewa dhidi ya makatibu hawa wakuu ni ya kimagufulimagufuli. Salama ya akina Nape, Ngeleja, Makamba Jr na Makamba Sr ikawa kulamba buti za Magufuli tu, si vinginevyo. Hiyo ndiyo SACCOS ya Magufuli inayoitwa CCM.

Huko ni kufilisika asilimia mia moja
 
Natamani sana amwage hiyo mboga maana
hawa jamaa wamezidi ujuaji na matusi
Paskali you stooping too low! Mbona unajiharibia heshima yako ambayo umeijenga haoa ukumbini kwa muda mrefu? Au ni kwa vile uchaguzi umekaribia?
 
Ahsante kwa kutuletea mjadala nzuri na wenye kuhitaji dhana Pana na tofauti katika kuujadili.

Kuna sehemu umeandika simple mind discussing people, great mind discuss ideas.
Tuanze na simple mind , kwa hiyo Lwakatare Ni mtu uliyeamua tumjadili kuhusu hatma ya CHADEMA ambayo Ni taasisi definitely inabaki kuwa philosophy ya simple mind ,Chadema has nothing to loose nothing to discuss about him fullstop.
Hii inachagizwa na uwepo wa watu watendaji wengi walio Kama yeye, mwache sense ili taasisi ikue.

Wapo waliosema akiondoka Makamba sijui Nani ataoweza Dar es Salaam. Ghafla Makonda huyooooo na mji umetulia Mara Mia ya ilivyokuwa kwa Makamba Tena huenda Makonda amemzidi Makamba maeneo mengi tu.
Haya nimeyasema kukumbusha maneno yako kwamba simple mind discuss people. Ukiwajidili watu Mara zote utapoteza uelekeo. Chadema hatuna sababu ya kumjadili Lwaka kwa sababu tuta justify philosophy ya simple mind discuss . Chadema never and will never deal with Lwakatare.

Turudi kwenye kitengo Cha Lwakatare, na video ya Lwaka Kama unavyomtaja. Unadhani Dr. Slaa hajui Nani kamtuma Lwakatare?????
Mbona kaenda CCM na kapewa ubalozi , huu so ndio muda nzuri wa yeye aliyekuwa karibu mkuu na mtendaji wa chama kuungana na LWAKATARE ili waibomoe CDM.

Alishindwa Slaa master politician mwenye Kila Siri ya Chama ,ndio atusumbue lwakare meeeen wewe Paskali sio huyu ninayekujua.


Secondly, great mind discussing ideas.
CDM Ni great mind na kunajadiliwa maswala mtambuka sio watu binafsi.CDM Ina zalisha watu Sina tofauti kulingana na mahitaji ya muda husika. Ukimya wa Chadema na uimara wao wa kuvuka vihunzi una reflect kuwa Taasisi ya CHADEMA imeimarika Mara dufu baada ya uchaguzi wa 2015.

*Information quality and security
Alipokuaja Lowassa , tulibezwa tumeacha asset na kuichukua liability Ila ukweli yule mzee ndiye mchawi wao.
Kwa jicho lililopevuka utakubaliana na Mimi Chadema iliimarika zaidi kwenye idara ya ulinzi na usalama wa chama kuliko siku zote alizowahi kuhudumu Lwakare na wale vijana wa ulinzi wa chama.
Paskali hivi hujui impact ya Apson Mwang'onda kwenye Chadema ??????
Hata Kama amefariki lakini I hope He did something to them na ndipo Lwakatare akapoteza ushawishi kwa Nini chama kimtegemee kwa idara.

Nadhani since then mpaka uchaguzi unaisha idara ya intelligence ya CHADEMA ilibaki na ujuzi mkubwa Sana.
Na hili linathibitishwa na vihunzi walivyokutana navyo Chadema na kuvishinda.

Taasisi imekuwa imara zaidi kuliko siku zote,kwa sababu they quality information about sabotage and they know how to handle it. Ndio maana nasema we are great thinker and discussing issues not personalities.

Endelea kuamini Chadema inakufa, halafu wenzio tunatoboa na hapo ndio utajua hujui kwa Ni CCM wanamshambulia Mbowe na sio kuinadi ilani yao na mgombea wao.

Ukinijibu nitarudi, ahsante kwa mada mujarabu bro Paskali.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Mh Lwakatare bado tu hajamwaga hiyo mboga?
 
Uzuri
Uzuri ni kwamba jf nzima inajua mshana kakuzidi IQ na unamuogopa.
 

Una maoni gani bwana paskali kama tu Bukoba ambapo ndio jikoni kabisa mboga inapomwagikia ndio hivi!!
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…