Je, wajua kuwa idadi ya wapiga kura nchini inakaribiana sana na idadi ya watu wenye kutumia mtandao (internet)?

Je, wajua kuwa idadi ya wapiga kura nchini inakaribiana sana na idadi ya watu wenye kutumia mtandao (internet)?

Unabisha bure, hebu tazama taarifa hii ya Reuters ya mwaka 2018 waliyoipata kutoka TCRA, watumiaji wako Milion 23, tena kati ya hao 82% wanaingia mitandaoni kwa kutumia Smartphone. Hapo ndo utajua power ya Whatsapp ambayo Lissu alisema tutawashughulikia CCM kupitia Whatsapp, hapo sijazungumzia mitandao mingine maarufu.

View attachment 1575673
Mimi nilikuwa nina namba tatu, ziko watsup!

Wanahesabuje hapo?

Sijazungumzia kwingine!
 
Mimi nilikuwa nina namba tatu, ziko watsup!

Wanahesabuje hapo?

Sijazungumzia kwingine!

Hizo whatsapp zako zina magrupu yaleyale au kila namba ina magrupu yake tofauti?

Kama ni magrupu tofauti basi inaonyesha unazidi kuinteract na watu wengi zaidi kitu kinachoongeza connectivity ya watu mtandaoni
 
Hahaha daftari la kujiandikisha au daftari la mpiga kura lilikuwa linakaa kwa kada wa ccm unategemea nini?!
Siku ya kupiga kura mtashangaa majina ya wananchi hayapo, ila ya wana ccm pekee.
 
Hizo whatsapp zako zina magrupu yaleyale au kila namba ina magrupu yake tofauti?

Kama ni magrupu tofauti basi inaonyesha unazidi kuinteract na watu wengi zaidi kitu kinachoongeza connectivity ya watu mtandaoni
Kila namba inakuwa na group zake!

Sasa hapo kwa mahesabu yao. Wa/anahesabika watu wangapi?
 
Kila namba inakuwa na group zake!

Sasa hapo kwa mahesabu yao. Wa/anahesabika watu wangapi?

TCRA wakitoa idadi ya Users wana uhakika na takwimu yao kwa sababu wana uwezo wa kufilter information based on the user ID hata kama mtumiaji ana line 50 kwa sababu ulisajili line kwa vitambulisho ambavyo vina information zako.
Kwa hiyo hata ukiwa na line 10 watalink line yako na ID yako na utahesabika mtumiaji mmoja tu.

Kwa hiyo wakisema watumiaji milion 23 wanaingia mtandaoni basi maana yake ni kuwa watu milion 23 wanaingia mtandaoni siyo line milion 23.
 
Kuna watu wanazibeza takwimu zinazotolewa mitandaoni. Takwimu ambazo nyingi kila mara zinaonyesha kuwa Tundu Lissu anamshinda Magufuli.

Binafsi ninaweza kusema kuwa hizi takwimu (polls) zinaweza kuwa credible (zenye kuaminika) zaidi nyakati hizi za sasa kuliko baadhi ya watu wanavyodhani na nitaelezea sababu za kitakwimu

Sababu zenyewe ni hizi zifuatazo

1. Aina ya Sampuli (Sampuli nasibu/random sampling)
2. Uwepo wa Taarifa unaoshabihiana na takwimu hizi (Triangulation of information)
3. Jumuia ambayo takwimu hizi zinatoka(credible population from which the sample is drawn

1. Aina ya Sampuli

Tumeona kuwa takwimu zinazochukuliwa ni kutoka kwa mtu yeyote anayeamua kwa utashi wake bila kulazimishwa na yeyote na hakuna wa kumzuia yeyote kupiga kura yake katika mtandao husika. Hii tayari inaonyesha kuwa kuna "nasibu" au randomness, kwa sababu hujui mtu atakayefuata atampigia nani, Kwa kigezo hiki tayari Takwimu za mitandaoni zinapata credibility

2. Uwepo wa Takwimu zinazoshabihiana na Taarifa hizi (Triangulation)

Mwaka 2017 Taasisi ya TWAWEZA ilionyesha kuwa umaarufu wa Magufuli umeshuka kutoka asilimia zaidi ya 90 mwaka 2016 hadi asilimia 55 mwaka huo.

Pili kwa mujibu wa Taarifa aliyoitoa Zitto Kabwe humu JF kuwa TISS imefanya utafiti mwaka 2018 na kuonyesha kuwa Uchaguzi ukifanyika mwaka huo basi Magufuli anashindwa.

Tatu kukosekana kwa takwimu yoyote ya mtandaoni iliyo wazi inayoonyesha Magufuli kumshinda Lissu, Isipokuwa ni Lissu tu ndo anaonekana kumshinda Magufuli hivi.
Kwa majumuisho ya sources hizi hii inaonyesha kuwa huenda ni kweli Lissu anakubalika kuliko Magufuli

3. Jumuia ya mtandaoni inaakisi Jumuia ya wapiga kura nchini (credible population)

Kwa mujibu wa NEC waliojiandikisha kupiga kura nchini ni milioni 29 na kwa mujibu wa TCRA zaidi ya Watanzania milioni 23 wana access ya mtandao (internet), Hii maana yake ni kuwa sampuli ya takwimu za mtandao inatoka kwenye population halisi ya wapiga kura nchini.

Kwa hiyo kutokana na vigezo hivyo vitatu huenda takwimu zinazotolewa mitandaoni, ambazo kila mara zinaonyesha Tundu Lissu anakubalika zaidi ya Magufuli zina ukweli ndani yake.

Lissu alikuwa sahihi kusema kuwa waachie CCM na ma TV yao na Magazeti yao ila washughulikiwe kwenye mitandao ikiwemo Whatsapp, huenda alijua ukweli huu kuwa Jamii ya Watanzania kwa sasa ni Jamii ya kidijitali zaidi (digital society)

Na huenda ndiyo maana serikali ya CCM imeanza kusumbuasumbua vijana wa mitandaoni wanaorusha maudhui ya Lissu. Hata hivyo wameshachelewa. Wananchi wanajua wapi pa kupata taarifa za Lissu wakizitaka, napo ni mtandaoni!

Hitimisho:

Huu uchaguzi siyo mwepesi kwa CCM hata kidogo, labda walete magumashi yao

Hapa chini ni Taarifa ya Shirika la habari la Reuters, ya mwaka 2018 wakiinukuu TCRA kuhusu kiwango cha watumia internet na wenye kutumia smartphones kuaccess mtandao

View attachment 1575675

Hakuna mtanzania mwenye line moja ya simu. Wengine wana line mpaka 5 kila mtandao!! Hata maandamano ya Mange yalikuwa mtandaoni hivyo sioni cha ajabu. Bila kusahau wapiga kura za maruhani kwenye utabiri wenu feki!! Subirini mziki wa tarehe 28 Oct!! Msiseme mmeibiwa!! Endeleeni na kampeni zenu za mjini wakati wapigakura wapo vijijini!!

Nashauri mgombea mwenza wa Lissu apambane sio anabebwa kama demu!

Queen Esther
 
TCRA wakitoa idadi ya Users wana uhakika na takwimu yao kwa sababu wana uwezo wa kufilter information based on the user ID hata kama mtumiaji ana line 50 kwa sababu ulisajili line kwa vitambulisho ambavyo vina information zako.
Kwa hiyo hata ukiwa na line 10 watalink line yako na ID yako na utahesabika mtumiaji mmoja tu.

Kwa hiyo wakisema watumiaji milion 23 wanaingia mtandaoni basi maana yake ni kuwa watu milion 23 wanaingia mtandaoni siyo line milion 23.
Shukrani,
Nimekuelewa!
 
Hakuna mtanzania mwenye line moja ya simu. Wengine wana line mpaka 5 kila mtandao!! Hata maandamano ya Mange yalikuwa mtandaoni hivyo sioni cha ajabu. Bila kusahau wapiga kura za maruhani kwenye utabiri wenu feki!! Subirini mziki wa tarehe 28 Oct!! Msiseme mmeibiwa!! Endeleeni na kampeni zenu za mjini wakati wapigakura wapo vijijini!!

Nashauri mgombea mwenza wa Lissu apambane sio anabebwa kama demu!

Queen Esther

TCRA wanahesabu user ID's siyo idadi ya line
Hata kama mtu una line 50, bado ni user Mmoja.

Takwimu za TCRA zinahusu idadi ya Users siyo idadi ya lines
 
Kama unasema wanaopiga kura kwa Fatma au Maria ni wale wanaoioppose serikali nenda jaribu kupita kwenye post ya mwisho ya Pombe twitter soma comments utajua hujui unachojua,wala ustumue nguvu nyingi
Teh teh teh, chukua mkutano wowote aliofanya Magufuli sehemu yoyote, then, angalia aina ya watu wanaohudhuria halafu utapata majibu kama wanna access na mitandao au hawana.
Hizo polls zinazofanywa na watu obviously matokeo yake yatategemea muelekeo wake. Unajua Nini kitatokea kwenye Poll iliyoanzishwa na Fatuma Katume au Maria Sarungi kwa sababu 90% ya wafuasi wake ni wale wanaopendezwa na misimamo yake.
Matokeo yatakuwa hivo hivo kwenye page ya Gerson Msigwa, Antony Mavunde au Hamis Kigwangala.
So acheni kujipa matumaini bure, angalieni Population anayopata Magu tena barabarani na kwenye vimiji vidogo, angalia aina ya watu wanaokwenda kwenye mikutano ya Magu na wale wanaokwenda kwenye mikutano ya Loketo utaona tofauti.
Mmoja ana wapiga kura, mwingine ana wafuasi.
 
Hakuna mtanzania mwenye line moja ya simu. Wengine wana line mpaka 5 kila mtandao!! Hata maandamano ya Mange yalikuwa mtandaoni hivyo sioni cha ajabu. Bila kusahau wapiga kura za maruhani kwenye utabiri wenu feki!! Subirini mziki wa tarehe 28 Oct!! Msiseme mmeibiwa!! Endeleeni na kampeni zenu za mjini wakati wapigakura wapo vijijini!!

Nashauri mgombea mwenza wa Lissu apambane sio anabebwa kama demu!

Queen Esther
Wewe unabebwaga kama yeye?
 
Kama unasema wanaopiga kura kwa Fatma au Maria ni wale wanaoioppose serikali nenda jaribu kupita kwenye post ya mwisho ya Pombe twitter soma comments utajua hujui unachojua,wala ustumue nguvu nyingi

umeongea point kubwa sana

Kama anadhani kuwa followers maana yake ni watu wanaokubaliana na wewe kila kitu basi wanaomfollow Magufuli mtandaoni wangekuwa ni wale wanaomkubali kindakindaki, lakini fact kwamba watu huwa wanamchallenge hata kwenye account yake mwenyewe inaonyesha kuwa watu wako dynamic, kuna muda wanakubaliana na wewe na kuna muda wanakupinga.

Kwa hiyo siyo sahihi kudharau online polls
 
Andiko duni mno ! Magufuli anayekusanya raia kwa malori , matrekta na mabasi ya abiria wamlinganishaje na wanaokuja wenyewe ?
Unawezaje kuwasomba watu wasiokutaka!? 😂😂😂Kama hawalazimishwi, maana yake nia wanakuwa nayo, so wanawezeshwa na huo ni ushahidi kuwa hao ni wanaoiprnda CCM kwa sababu sidhani Kama Kuna mwana CDM au ACT atakubali kupanda trecta
 
Hizo population za njiani nizakutengeneza,shituka
Kwani kwani Kuna Chama hakifanyi hivo. Kila chama kabla mgombea wake hajapita linafanya Mipango na maandizi ya kuhakikisha watu wapo wa kutosha, tofauti tu ni nani ana Mipango mizuri na anakubalika na watu!
 
Unawezaje kuwasomba watu wasiokutaka!? 😂😂😂Kama hawalazimishwi, maana yake nia wanakuwa nayo, so wanawezeshwa na huo ni ushahidi kuwa hao ni wanaoiprnda CCM kwa sababu sidhani Kama Kuna mwana CDM au ACT atakubali kupanda trecta

Watumishi wa serikali huko mikoani wanapigwa mkwara wahudhurie mikutano ya Magufuli.
Wakuu wa shule wanalazimishwa kufunga shule na kuwataka watoto wa shule wavae nguo za nyumbani na waende kwenye mikutano ya Magufuli
 
Aise basi Nchi hii tuna watumishi wengi sana na tuna wanafunzi wengi Sana. Kama wale waliojaza CCM Kirumba na Lake Tanganyika walikuwa Watumishi na Wanafunzi basi wapo wengi mno.
 
Aise basi Nchi hii tuna watumishi wengi sana na tuna wanafunzi wengi Sana. Kama wale waliojaza CCM Kirumba na Lake Tanganyika walikuwa Watumishi na Wanafunzi basi wapo wengi mno.

Sasa ulifikiri tuna wanafunzi wachache eh? 😁😁
 
Yani unaenda kwenye group la ccm alafu unasema haya tupige kura, alafu unashangaa mgombea wa ccm akishinda?

Alafu kwa taarifa yako tu ni kwamba hao hao wa mitandaoni ndio waliohamasishana wasiende kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura.
Kwa hiyo walioenda ni wazee na kina mama wa chama cha mapinduzi ndio watakaopiga kura.
.
Wapinzani wanashindwa kwa vingi na always wao huwa marais walioshinda kupitia mitandao.
 
Teh teh teh, chukua mkutano wowote aliofanya Magufuli sehemu yoyote, then, angalia aina ya watu wanaohudhuria halafu utapata majibu kama wanna access na mitandao au hawana.
Hizo polls zinazofanywa na watu obviously matokeo yake yatategemea muelekeo wake. Unajua Nini kitatokea kwenye Poll iliyoanzishwa na Fatuma Katume au Maria Sarungi kwa sababu 90% ya wafuasi wake ni wale wanaopendezwa na misimamo yake.
Matokeo yatakuwa hivo hivo kwenye page ya Gerson Msigwa, Antony Mavunde au Hamis Kigwangala.
So acheni kujipa matumaini bure, angalieni Population anayopata Magu tena barabarani na kwenye vimiji vidogo, angalia aina ya watu wanaokwenda kwenye mikutano ya Magu na wale wanaokwenda kwenye mikutano ya Loketo utaona tofauti.
Mmoja ana wapiga kura, mwingine ana wafuasi.
Kabisa mkuu! Sasa mtu unaanzisha polls kwenye group la Maria Sarungi unategemea upate matokeo gani?
Wakati huyo dada hatofautiani na Mange kwamba ukimchallange anakupiga ban?
 
Andiko duni mno ! Magufuli anayekusanya raia kwa malori , matrekta na mabasi ya abiria wamlinganishaje na wanaokuja wenyewe ?
Hiki kichaka cha kukusanya watu kwa malori kipo toka enzi za slaa!

Hivi unaweza kwenda kuwalazimisha wanachama wa simba kwenda kushabikia mpira wa yanga?
 
Back
Top Bottom