Je, wajua kuwa idadi ya wapiga kura nchini inakaribiana sana na idadi ya watu wenye kutumia mtandao (internet)?

Je, wajua kuwa idadi ya wapiga kura nchini inakaribiana sana na idadi ya watu wenye kutumia mtandao (internet)?

Chadema inasifika sana kuwa na wanachama vijana, wenye exposure, elimu na wapenda mabadiliko na ukiona hali mtandaoni ina onesha uhalisia uliopo katika jamii...


Na hili kundi kuna wakati halihitaji sana kwenda kwenye mikutano ili kuaccess taarifa..tunasoma Ilani kwa mtandao...tunaangalia hotuba kwa mtandao...tunasoma na kupima sera za wagombea na tunafanya analysis ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi ambayo tunaamini ni sahihi ..

Lakini lipo group ambalo pia linafanya maamuzi kulingana na peer pressure hususani vijana chipukizi.....ambalo pia ni mtaji wa Chadema..

Wapo watu walioumizwa na serikali hii either direct au indirect....ambao pia wanadeviate katika group ulilosema hapo juu...

Elimu ya Uraia kwa sasa hata vijijini ni tofauti na miaka ya nyuma ambapo baadhi ya watu walikuwa wanajua Nyerere bado yupo..


Last week nilikuwa kijiji fulani nikachokpoza mjadala fulani nilishangazwa sana na uelewa walio nao wale wananchi na mazingira wanayoishi havilingani...yaani ukimkuta mtu anatetea CCM au CDM anatetea kwa hoja....

Kingine hili ni kundi ambalo hatutegemei kuchagua mbunge ili atuletee maendeleo bali atunge na kutetea sheria zitakazowezesha maendeleo(enabling environment)...maendeleo binafsi tunapambana nayo sisi wenyewe japo tunaangushwa na sera mbovu zinazodidimisha ustawi wa waajiriwa na wafanyabiashara ...ndo maana tunapenda watu wenye midomo kama Zitto...Lissu n.k who can speak out kwa niaba yetu na sio mabubu kama Abood ambao uwepo wao hausaidii .

CCM mtaji wenu ni wazee na ndo hao ambao generation yao inaisha na pia mnawanyima Mafao....mnaharibu biashara zao za Korosho....nk
Hizi ni hoja nzito sana, thanks na big up
 
Udhihirisho rahisi tu. Mabango ya Magufuli yametapakaa kila kona ya nchi. Nimezunguka sehemu nyingi lakini sijaona bango hata moja la Tundu Lissu, lakini ajabu ni kuwa kadri siku zinavyokwenda ndivyo anavyozidi kupata uungwaji mkono. Mwaka huu ccm imepata challenge inayowahusu kweli na wanatoka madarakani.
 
Hujaongeza hapo kuwa siku hizi taarifa nyingi zinapatikana kwa lugha adhimu ya Kiswahili. Hivyo waliosoma na wasio soma wote tunaelewana kwa ufasaha. Kinachofuata kwa hawa jamaa ni kufungia mtandao, maana watu wamehama kujadili whatsapp na kuhamisia twitter na jamii forum wanakoweza kujificha.
 
Kuna watu wanazibeza takwimu zinazotolewa mitandaoni. Takwimu ambazo nyingi kila mara zinaonyesha kuwa Tundu Lissu anamshinda Magufuli.

Binafsi ninaweza kusema kuwa hizi takwimu (polls) zinaweza kuwa credible (zenye kuaminika) zaidi nyakati hizi za sasa kuliko baadhi ya watu wanavyodhani na nitaelezea sababu za kitakwimu

Sababu zenyewe ni hizi zifuatazo

1. Aina ya Sampuli (Sampuli nasibu/random sampling)
2. Uwepo wa Taarifa unaoshabihiana na takwimu hizi (Triangulation of information)
3. Jumuia ambayo takwimu hizi zinatoka(credible population from which the sample is drawn

1. Aina ya Sampuli
Tumeona kuwa takwimu zinazochukuliwa ni kutoka kwa mtu yeyote anayeamua kwa utashi wake bila kulazimishwa na yeyote na hakuna wa kumzuia yeyote kupiga kura yake katika mtandao husika. Hii tayari inaonyesha kuwa kuna "nasibu" au randomness, kwa sababu hujui mtu atakayefuata atampigia nani, Kwa kigezo hiki tayari Takwimu za mitandaoni zinapata credibility

2. Uwepo wa Takwimu zinazoshabihiana na Taarifa hizi (Triangulation)
Mwaka 2017 Taasisi ya TWAWEZA ilionyesha kuwa umaarufu wa Magufuli umeshuka kutoka asilimia zaidi ya 90 mwaka 2016 hadi asilimia 55 mwaka huo.

Pili kwa mujibu wa Taarifa aliyoitoa Zitto Kabwe humu JF kuwa TISS imefanya utafiti mwaka 2018 na kuonyesha kuwa Uchaguzi ukifanyika mwaka huo basi Magufuli anashindwa.

Tatu kukosekana kwa takwimu yoyote ya mtandaoni iliyo wazi inayoonyesha Magufuli kumshinda Lissu, Isipokuwa ni Lissu tu ndo anaonekana kumshinda Magufuli hivi.
Kwa majumuisho ya sources hizi hii inaonyesha kuwa huenda ni kweli Lissu anakubalika kuliko Magufuli

3. Jumuia ya mtandaoni inaakisi Jumuia ya wapiga kura nchini (credible population)
Kwa mujibu wa NEC waliojiandikisha kupiga kura nchini ni milioni 29 na kwa mujibu wa TCRA zaidi ya Watanzania milioni 23 wana access ya mtandao (internet), Hii maana yake ni kuwa sampuli ya takwimu za mtandao inatoka kwenye population halisi ya wapiga kura nchini.

Kwa hiyo kutokana na vigezo hivyo vitatu huenda takwimu zinazotolewa mitandaoni, ambazo kila mara zinaonyesha Tundu Lissu anakubalika zaidi ya Magufuli zina ukweli ndani yake.

Lissu alikuwa sahihi kusema kuwa waachie CCM na ma TV yao na Magazeti yao ila washughulikiwe kwenye mitandao ikiwemo Whatsapp, huenda alijua ukweli huu kuwa Jamii ya Watanzania kwa sasa ni Jamii ya kidijitali zaidi (digital society)

Na huenda ndiyo maana serikali ya CCM imeanza kusumbuasumbua vijana wa mitandaoni wanaorusha maudhui ya Lissu. Hata hivyo wameshachelewa. Wananchi wanajua wapi pa kupata taarifa za Lissu wakizitaka, napo ni mtandaoni!

Hitimisho:
Huu uchaguzi siyo mwepesi kwa CCM hata kidogo, labda walete magumashi yao

Hapa chini ni Taarifa ya Shirika la habari la Reuters, ya mwaka 2018 wakiinukuu TCRA kuhusu kiwango cha watumia internet na wenye kutumia smartphones kuaccess mtandao

View attachment 1575675
Do you want us to believe that INTERNET USERS EQUALS REGISTERED VOTERS!? Hivi ni vitu viwili tofauti sana sana. In fact many INTERNET USERS hata hawakujiandikisha kwenye DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIG KURA. Many of us ni wapenzi na washabiki tu, na hasa tunashabikia KIMUHEKO ZAIDI!
 
Back
Top Bottom