At Calvary
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 4,533
- 3,595
Mimi nilikuwa nina namba tatu, ziko watsup!Unabisha bure, hebu tazama taarifa hii ya Reuters ya mwaka 2018 waliyoipata kutoka TCRA, watumiaji wako Milion 23, tena kati ya hao 82% wanaingia mitandaoni kwa kutumia Smartphone. Hapo ndo utajua power ya Whatsapp ambayo Lissu alisema tutawashughulikia CCM kupitia Whatsapp, hapo sijazungumzia mitandao mingine maarufu.
View attachment 1575673
Mimi nilikuwa nina namba tatu, ziko watsup!
Wanahesabuje hapo?
Sijazungumzia kwingine!
Kila namba inakuwa na group zake!Hizo whatsapp zako zina magrupu yaleyale au kila namba ina magrupu yake tofauti?
Kama ni magrupu tofauti basi inaonyesha unazidi kuinteract na watu wengi zaidi kitu kinachoongeza connectivity ya watu mtandaoni
Kila namba inakuwa na group zake!
Sasa hapo kwa mahesabu yao. Wa/anahesabika watu wangapi?
Kuna watu wanazibeza takwimu zinazotolewa mitandaoni. Takwimu ambazo nyingi kila mara zinaonyesha kuwa Tundu Lissu anamshinda Magufuli.
Binafsi ninaweza kusema kuwa hizi takwimu (polls) zinaweza kuwa credible (zenye kuaminika) zaidi nyakati hizi za sasa kuliko baadhi ya watu wanavyodhani na nitaelezea sababu za kitakwimu
Sababu zenyewe ni hizi zifuatazo
1. Aina ya Sampuli (Sampuli nasibu/random sampling)
2. Uwepo wa Taarifa unaoshabihiana na takwimu hizi (Triangulation of information)
3. Jumuia ambayo takwimu hizi zinatoka(credible population from which the sample is drawn
1. Aina ya Sampuli
Tumeona kuwa takwimu zinazochukuliwa ni kutoka kwa mtu yeyote anayeamua kwa utashi wake bila kulazimishwa na yeyote na hakuna wa kumzuia yeyote kupiga kura yake katika mtandao husika. Hii tayari inaonyesha kuwa kuna "nasibu" au randomness, kwa sababu hujui mtu atakayefuata atampigia nani, Kwa kigezo hiki tayari Takwimu za mitandaoni zinapata credibility
2. Uwepo wa Takwimu zinazoshabihiana na Taarifa hizi (Triangulation)
Mwaka 2017 Taasisi ya TWAWEZA ilionyesha kuwa umaarufu wa Magufuli umeshuka kutoka asilimia zaidi ya 90 mwaka 2016 hadi asilimia 55 mwaka huo.
Pili kwa mujibu wa Taarifa aliyoitoa Zitto Kabwe humu JF kuwa TISS imefanya utafiti mwaka 2018 na kuonyesha kuwa Uchaguzi ukifanyika mwaka huo basi Magufuli anashindwa.
Tatu kukosekana kwa takwimu yoyote ya mtandaoni iliyo wazi inayoonyesha Magufuli kumshinda Lissu, Isipokuwa ni Lissu tu ndo anaonekana kumshinda Magufuli hivi.
Kwa majumuisho ya sources hizi hii inaonyesha kuwa huenda ni kweli Lissu anakubalika kuliko Magufuli
3. Jumuia ya mtandaoni inaakisi Jumuia ya wapiga kura nchini (credible population)
Kwa mujibu wa NEC waliojiandikisha kupiga kura nchini ni milioni 29 na kwa mujibu wa TCRA zaidi ya Watanzania milioni 23 wana access ya mtandao (internet), Hii maana yake ni kuwa sampuli ya takwimu za mtandao inatoka kwenye population halisi ya wapiga kura nchini.
Kwa hiyo kutokana na vigezo hivyo vitatu huenda takwimu zinazotolewa mitandaoni, ambazo kila mara zinaonyesha Tundu Lissu anakubalika zaidi ya Magufuli zina ukweli ndani yake.
Lissu alikuwa sahihi kusema kuwa waachie CCM na ma TV yao na Magazeti yao ila washughulikiwe kwenye mitandao ikiwemo Whatsapp, huenda alijua ukweli huu kuwa Jamii ya Watanzania kwa sasa ni Jamii ya kidijitali zaidi (digital society)
Na huenda ndiyo maana serikali ya CCM imeanza kusumbuasumbua vijana wa mitandaoni wanaorusha maudhui ya Lissu. Hata hivyo wameshachelewa. Wananchi wanajua wapi pa kupata taarifa za Lissu wakizitaka, napo ni mtandaoni!
Hitimisho:
Huu uchaguzi siyo mwepesi kwa CCM hata kidogo, labda walete magumashi yao
Hapa chini ni Taarifa ya Shirika la habari la Reuters, ya mwaka 2018 wakiinukuu TCRA kuhusu kiwango cha watumia internet na wenye kutumia smartphones kuaccess mtandao
View attachment 1575675
Shukrani,TCRA wakitoa idadi ya Users wana uhakika na takwimu yao kwa sababu wana uwezo wa kufilter information based on the user ID hata kama mtumiaji ana line 50 kwa sababu ulisajili line kwa vitambulisho ambavyo vina information zako.
Kwa hiyo hata ukiwa na line 10 watalink line yako na ID yako na utahesabika mtumiaji mmoja tu.
Kwa hiyo wakisema watumiaji milion 23 wanaingia mtandaoni basi maana yake ni kuwa watu milion 23 wanaingia mtandaoni siyo line milion 23.
Hakuna mtanzania mwenye line moja ya simu. Wengine wana line mpaka 5 kila mtandao!! Hata maandamano ya Mange yalikuwa mtandaoni hivyo sioni cha ajabu. Bila kusahau wapiga kura za maruhani kwenye utabiri wenu feki!! Subirini mziki wa tarehe 28 Oct!! Msiseme mmeibiwa!! Endeleeni na kampeni zenu za mjini wakati wapigakura wapo vijijini!!
Nashauri mgombea mwenza wa Lissu apambane sio anabebwa kama demu!
Queen Esther
Teh teh teh, chukua mkutano wowote aliofanya Magufuli sehemu yoyote, then, angalia aina ya watu wanaohudhuria halafu utapata majibu kama wanna access na mitandao au hawana.
Hizo polls zinazofanywa na watu obviously matokeo yake yatategemea muelekeo wake. Unajua Nini kitatokea kwenye Poll iliyoanzishwa na Fatuma Katume au Maria Sarungi kwa sababu 90% ya wafuasi wake ni wale wanaopendezwa na misimamo yake.
Matokeo yatakuwa hivo hivo kwenye page ya Gerson Msigwa, Antony Mavunde au Hamis Kigwangala.
So acheni kujipa matumaini bure, angalieni Population anayopata Magu tena barabarani na kwenye vimiji vidogo, angalia aina ya watu wanaokwenda kwenye mikutano ya Magu na wale wanaokwenda kwenye mikutano ya Loketo utaona tofauti.
Mmoja ana wapiga kura, mwingine ana wafuasi.
Wewe unabebwaga kama yeye?Hakuna mtanzania mwenye line moja ya simu. Wengine wana line mpaka 5 kila mtandao!! Hata maandamano ya Mange yalikuwa mtandaoni hivyo sioni cha ajabu. Bila kusahau wapiga kura za maruhani kwenye utabiri wenu feki!! Subirini mziki wa tarehe 28 Oct!! Msiseme mmeibiwa!! Endeleeni na kampeni zenu za mjini wakati wapigakura wapo vijijini!!
Nashauri mgombea mwenza wa Lissu apambane sio anabebwa kama demu!
Queen Esther
Kama unasema wanaopiga kura kwa Fatma au Maria ni wale wanaoioppose serikali nenda jaribu kupita kwenye post ya mwisho ya Pombe twitter soma comments utajua hujui unachojua,wala ustumue nguvu nyingi
Unawezaje kuwasomba watu wasiokutaka!? πππKama hawalazimishwi, maana yake nia wanakuwa nayo, so wanawezeshwa na huo ni ushahidi kuwa hao ni wanaoiprnda CCM kwa sababu sidhani Kama Kuna mwana CDM au ACT atakubali kupanda trectaAndiko duni mno ! Magufuli anayekusanya raia kwa malori , matrekta na mabasi ya abiria wamlinganishaje na wanaokuja wenyewe ?
Kwani kwani Kuna Chama hakifanyi hivo. Kila chama kabla mgombea wake hajapita linafanya Mipango na maandizi ya kuhakikisha watu wapo wa kutosha, tofauti tu ni nani ana Mipango mizuri na anakubalika na watu!Hizo population za njiani nizakutengeneza,shituka
Unawezaje kuwasomba watu wasiokutaka!? πππKama hawalazimishwi, maana yake nia wanakuwa nayo, so wanawezeshwa na huo ni ushahidi kuwa hao ni wanaoiprnda CCM kwa sababu sidhani Kama Kuna mwana CDM au ACT atakubali kupanda trecta
Aise basi Nchi hii tuna watumishi wengi sana na tuna wanafunzi wengi Sana. Kama wale waliojaza CCM Kirumba na Lake Tanganyika walikuwa Watumishi na Wanafunzi basi wapo wengi mno.Watumishi wa serikali huko mikoani wanapigwa mkwara wahudhurie mikutano ya Magufuli.
Wakuu wa shule wanalazimishwa kufunga shule na kuwataka watoto wa shule wavae nguo za nyumbani na waende kwenye mikutano ya Magufuli
Aise basi Nchi hii tuna watumishi wengi sana na tuna wanafunzi wengi Sana. Kama wale waliojaza CCM Kirumba na Lake Tanganyika walikuwa Watumishi na Wanafunzi basi wapo wengi mno.
Kabisa mkuu! Sasa mtu unaanzisha polls kwenye group la Maria Sarungi unategemea upate matokeo gani?Teh teh teh, chukua mkutano wowote aliofanya Magufuli sehemu yoyote, then, angalia aina ya watu wanaohudhuria halafu utapata majibu kama wanna access na mitandao au hawana.
Hizo polls zinazofanywa na watu obviously matokeo yake yatategemea muelekeo wake. Unajua Nini kitatokea kwenye Poll iliyoanzishwa na Fatuma Katume au Maria Sarungi kwa sababu 90% ya wafuasi wake ni wale wanaopendezwa na misimamo yake.
Matokeo yatakuwa hivo hivo kwenye page ya Gerson Msigwa, Antony Mavunde au Hamis Kigwangala.
So acheni kujipa matumaini bure, angalieni Population anayopata Magu tena barabarani na kwenye vimiji vidogo, angalia aina ya watu wanaokwenda kwenye mikutano ya Magu na wale wanaokwenda kwenye mikutano ya Loketo utaona tofauti.
Mmoja ana wapiga kura, mwingine ana wafuasi.
Hiki kichaka cha kukusanya watu kwa malori kipo toka enzi za slaa!Andiko duni mno ! Magufuli anayekusanya raia kwa malori , matrekta na mabasi ya abiria wamlinganishaje na wanaokuja wenyewe ?
Umeandika kisomi mno !