Uchaguzi 2020 Je, wajua kuwa Mfumo wa Serikali ya Majimbo unatumika kwenye Nchi zenye kukosa Umoja wa Kitaifa?

Uchaguzi 2020 Je, wajua kuwa Mfumo wa Serikali ya Majimbo unatumika kwenye Nchi zenye kukosa Umoja wa Kitaifa?

Waungwana,

Chunguzeni leo hii nchi zote ambazo ni kinara wa mfumo wa Serikali za majimbo (federal government) duniani ni nchi ambazo zilikuwa zinakabiliwa Sana na tatizo la kukosa umoja wa Kitaifa kutokana na Vita, udini au Kukosa lugha ya kuwaunganisha.

Marekani walikuwa mataifa huru 50. Kuwaunganisha ni lazima uwaachie baadhi ya madaraka yao, hivyo mfumo wa Serikali ya Majimbo ni sahihi kwao.

Canada wanashida ya lugha. Kuna majimbo hawajui au hawaongei kabisa kiingereza, wenyewe wanaongea kifaransa. Hawa ni muhimu kuwa na majimbo ili wawe huru kutumia lugha waipendayo.

Ujerumani walitawanyika na kuwa nchi mbili tofauti na ukuta ukajengwa Kati ya Ujerumani ya Mashariki na ile ya magharibi. Hawa ili kuwaunganisha mfumo wa Serikali ya Majimbo ulikuwa lazima ila maeneo hayo yabaki na sehemu ya utawala wake wa awali.

Nigeria imepitia mengi sana sana Kati ya waislamu wa kaskazini na wakristo wa kusini. Waafrika kusini vilevile wamepitia mengi Kuhusu ukoloni na ukaburu. Wazungu wengi walibaki Afrika Kusini baada ya Uhuru kamili mwaka 1994. Kwa misingi hiyo, unaweza kabisa kuona Nigeria na Afrika kusini walihitaji utawala wa majimbo.

Sisi Tanzania tunahitaji utawala wa majimbo ili iweje? Je, changamoto za kiuchumi, utamaduni na kisiasa zinatokana na mazingira hayo niliyoyataja hapo juu?

Wazungu hawana makabila na karibu wote wana dini au imani sawa. Kuwawekea utawala wa majimbo sio mbaya. Hapa kwetu tunajadili sio to dini Bali hata dhehebu. Kuna baadhi ya watu walisema katika uchaguzi wa 2015, Sasa ni zamu ya M-KKKT kuwa wa -RC wametawala Sana. Sasa kwenye nchi Kama hii uanze umajimbo, tunategemea nini kitokee?

Majimbo yatatutenga zaidi badala ya kutuleta pamoja. Mfumo wa Serikali za mitaa kwa Tanzania ni mzuri na toshelevu. Kama Kuna changamoto basi ni Kuboresha tuu.

Ninawashangaa Sana wapinzani, sijui wamekunywa wanzuki ya wapi. Tasilimali za kila eneo husaidia eneo hilo na maeneo mengine. Hii ni kwasababu watu wanaingiliana na wanaweza kuishi popote. Mtoto wa Kagera anapangiwa kazi Tanga na maisha yanaenda. Mtu wa Mtwara anahamia Mbeya anakuwa mnyaki maisha yanaenda.

Watanzania tuukumbatie umoja, amani na mshikamano wetu kwa kuchagua mafiga matatu hapo 28 Oktoba, 2020. Tuwaadhibu wapinzani wanaotaka kutugawa kwa kuwanyima kura.

Amani Msumari

Tanga (kwasasa Kigamboni kumtafutia Rais Magufuli kura za bonus).
Kumbe unafaa sana Tanzania
 
Acha uwongo . Marekani kuna udini ? Marekani kuna ukabila ? Mfumo wa majimbo ni sahihi kwa kusukuma maendeleo kwa kasi zaidi. Kajifunze India uone majimbo yao ya Gujarat, Uttar Pradesh na mengineyo. Kuna ukabIla India ? Shenzi wewe
Akili yako ndogo. Hayo mataifa ni kama hakuna makabila vile ndo maana hawana hiyo shida. Igawe Tz katika majimbo uone kinachotokea.
 
Mtoa mada nia yako nzuri ila mikoa ndio shida zaidi kuliko majimbo maana mikoa iko kikabila zaidi na hili huwezi kuliepuka ukiweka kimajimbo unaunganisha mikoa zaidi ya mitatu yenye makabila tofauti, dini tofauti kuwa jimbo. mfano mdogo chukuwa Dodoma+Singida+Moro ikiwa jimbo la kati hapo makabila mengi wameungana. Hoja ya udini au ukabila haina nguvu ila kila unapokata mikoa kila siku ndio unaleta hali fulani ya ukabila. nchi nyingi duniani wanatumia majimbo kuleta changamoto ya maendeleo na kuondoa ukiritimba wa serikali kuu. watu kufanya mipango ya maendeleo wenyewe badala ya kutegemea serikali kuu.
 
Akili yako ndogo. Hayo mataifa ni kama hakuna makabila vile ndo maana hawana hiyo shida. Igawe Tz katika majimbo uone kinachotokea.
Ukabila umeanza lini Tanzania ? Afu unasema mi na akili ndogo ? Pumbavu kabisa, Pambaf indeed
 
Usifuate maneno ya vijiweni.

Mimi naamin watanzania bado hawana elimu ya mifumo ya serkali yao inavyoongozwa.

Leo hata nikikwambia uchore kaomchoro serkali kuu usikute hujui.

Hivyo kunaumuhimu wa elimu kwanza.
Dogo, kwa taarifa yako hizo nchi nilizozitaja hapo awali mi nimeshakaa sana. Sijakaa tu kule kwetu kantalamba peke yake, nimekaa duniani nimeona.
Na hivi ninavyoongea na wewe ninafanya research katika hiyo mifumo ya kiutawala kwa level ya Ph.D so usidhani unaongea na jinga jinga hapa. Upotoshaji unaofanywa na wanasiasa kwa makusudi ndiyo tatizo.
Mfumo wa serikali za majimbo ni mzuri sana kwa sababu unapeleka madaraka kwa wananchi.

Hebu jiulize swali dogo kwa mfano, kwa nini Dar es Salaam isiwe na meya wa jiji ambaye anachaguliwa na wananchi wenyewe na atakuwa mkuu wa serikali ya mkoa? Kuna haja gani ya Dar es Salaam kuwa na mkuu wa mkoa kama ukiwa na meya mwenye nguvu na madaraka sawa na mkuu wa mkoa ?

Ila kwa sababu tunajazwa hofu na propaganda ndiyo maana wengi tunaogopa ila uhalisia ni kwamba madara kwa wananchi ndiyo nyenzo ya maendeleo kwa karne hii ya 21. Ninaandika vitu ambavyo nina ushahidi navyo dogo.

Mfumo wa majimbo umetulia sana mzee. Nitaeleza zaidi kwa kirefu siku za usoni.

Just somebody,
Ph.D candidate in Political Science (American University)
 
Hatakama umezaliwa huko.
Lakini lazima uangalie uwezo wa jamii yako ya kiafrika ilivyo.

Kama hata.hata kawa tunaowachagua leo mtu anasimama mbele ya watanzania wenzake na kwasababu yeye ninkiongozi pale basi anataka kuogopeka ajione yy kama mungu.
Utafananishaje mtu.huyu na huko ulikokaa.

Hapa police akiva uniform anaona raia ote kama kuku.
Shida watu hawajaelimika.
Huwezi kumuletea mtu mfumo mpya wakati ule wa.kwanza wenyewe hajaufahamu.
 
Back
Top Bottom