Uchaguzi 2020 Je, wajua kuwa Mfumo wa Serikali ya Majimbo unatumika kwenye Nchi zenye kukosa Umoja wa Kitaifa?

Ndugu,

Tuna balozi mtaani
Tuna mwenyekiti
Tuna mtendaji wa Kijiji
Tuna diwani
Tuna mkurugenzi
Tuna mkuu wa wilaya

Sasa tunataka nini?
 
Japo so kweli... Lakini nikubaliane na wewe kuwa ccm imesababisha kukosekana kwa umoja wa kitaifa nchini kwa miaka 60 sasa...
Najua utabisha....lakini nikuulize...
Hivi kweli kuna umoja wa kitaifa ikiwa wengine wanakunywa maji ya mabomba tena yaliyotibiwa wakati huo huo wengine wanakunywa maji ya tope na hawaoni tatizo lolote...??
Je kuna umoja wa kitaifa ikiwa wengine wanatiririka kwenye mabarabara ya lami wakati huo huo wengine hata lami hawajui inavyofanana...!!
Je, kuna umoja wa kitaifa ikiwa kama mfanyakazi mafao yako unaambiwa ni hadi uzeeni wakati huoni uhakika wa kuufikia huo uzee... Na hata ukifanikiwa kuufikia bado mafao ni ahadi hewa...??

Mkuu rejesheni madaraka kwa wananchi...!!!
 
Badala ukadanganye huko Nanjilinji ambako kuna watu wanaoikubali ccm kwa mujibu wa TWAWEZA, sasa ulivyo MBULULA unakuja hapa kudanganya ma GT?
Lumumba lini mtakuwa na akili?!

Sent from my Infinix X606B using JamiiForums mobile app
 
Nchi haiendeshwi kwa ndoto ya mzee Mtei ambayo CHADEMA wote wanalazimika kuihubiri na kuitetea. Haifai kwani itatuletea shida kubwa Kama taifa. Tutawakataa na hata sasa tumewakataa
Nakushauri useme umewakataa, na siyo mmewakataa, kwa sababu hujashirikiana na mtu kuweka hili andiko, na zaidi ya hapo 28oct
 
Mwambie hata kabla ya East na West kuungana, West walishakuwa na majimbo. UK ni mfano mwingine. Nchi kubwa huwezi kuzitawala toka sehemu moja, majimbo yanakuja naturally.
 
Nieleze n kivipi serikali ya majimbo itashughulikia hayo uliyoyataja
 
Wengi wanaongelea serikali ya majimbo kwasababu tuu Lissu na CHADEMA wamesema ilihali hawalijui chimbuko lake
 
Ngoja kwanza, Majimbo yanayohubiriwa na Chadema Unayajua? Kila Jimbo Linajumuisha Mikoa mingapi na ipi?

Haya hubiri utengano namna utakavyotokea.
 
Badala ukadanganye huko Nanjilinji ambako kuna watu wanaoikubali ccm kwa mujibu wa TWAWEZA, sasa ulivyo MBULULA unakuja hapa kudanganya ma GT?
Lumumba lini mtakuwa na akili?!

Sent from my Infinix X606B using JamiiForums mobile app
Tumewazoea pingapinga.

Nipo Kivukoni hapa naongea na wavuvi. Nimewaeleza kuhusu ubovu wa Sera za CHADEMA, wameniemewa Sana. Wamesema hivi " hapa labda kidogo utaje ACT hao wapinzani wengine hamna kitu. Sisi tunakuahudi tunamchagua diwani Tarik, mbunge Zungu na Rais Magufuli.
 
Ndugu,

Tuna balozi mtaani
Tuna mwenyekiti
Tuna mtendaji wa Kijiji
Tuna diwani
Tuna mkurugenzi
Tuna mkuu wa wilaya

Sasa tunataka nini?
Hao Watendaji na Wakuu wa Wilaya wasiteuliwe na serikali, wachaguliwe na wananchi kama Madiwani. Mkurugenzi awe mwajiriwa wa Wilaya husika na siyo mteule wa Rais toka Dodoma!!
 
Nieleze n kivipi serikali ya majimbo itashughulikia hayo uliyoyataja

Yaani hata kama hili huna jibu basi upo gizani...!!
Kupitia serikali ya majimbo kila eneo litakuwa na funds za kutokana na vyanzo nyake kwa ajili ya miradi yake...!! Mipango ya mapato na matumizi watafanya watu wa eneo husika...!!
Serikali kuu itakuwa ndogo na yenye wajibu wa kusaidia bajeti au miradi pale inapohitajika hasa hasa kwenye majimbo yenye changamoto...!!
Kwa utaratibu wa sasa... Kazi tunafanye sisi huku mikoani lakini mipango na matumizi wapange Dar/Dodoma... Maendeleo yanaelekezwa kule Chato kunakowafurahisha mawaziri...
Hakika huu ni unyonyaji, ukandamizaji na ukoloni zaidi ya ule wa wajerumani na waingereza...

Pelekeni Madaraka Kwa Wananchi...!!
 
Badala ukadanganye huko Nanjilinji ambako kuna watu wanaoikubali ccm kwa mujibu wa TWAWEZA, sasa ulivyo MBULULA unakuja hapa kudanganya ma GT?
Lumumba lini mtakuwa na akili?!

Sent from my Infinix X606B using JamiiForums mobile app
Wahurumie tu CCM . Hawajui kuwa humu Tupo watu wengi wenye exposure zetu na ufahamu mkubwa wa mambo ya dunia na maendeleo
 
Lakini huo mfumo wa majimbo angalia Marekani na hio Canada ilipo kimaendeleo sisi miaka 58 Ujamaa umetufilisi mpaka akili zetu.


Ndukiiiii πŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈπŸƒβ€β™‚οΈ
Hukuelewa logic ya mtoa Uzi.
 
Mada ya kitoto kabisa hii.
 
Kwavile dawa ya kutojitenga ni majimbo sasa ubaya wake nini?.
 
Huko hakuna wewe ni kabila flani au dini flani. Halafu nchi yao imeshaendelea na wanapata mahitaji yote. Hapa kwetu aki tutashikana uchawi. Kwani Nigeria au Somalia ni mbali kaka? Mifano ipo hai
Kwani kipi kilianza;majimbo au maendeleo? N unaposema issue ya Ukabila inakujaje? Kwani tukisema Mwanza,Geita,Shinyanga liwe jimbo moja ndio itachochea ukabila? Kwani watu wa makabila mengine hawatoruhusiwa kufanya kazi?Kazi zitatolewa kwa kigezo cha ukabila? Shule zitafundishwa kwa kisukuma? Askari watakao toka depo watagawanywa kwa ukabila? maswali mengi tu
 
Sio ishu ya Rais, n ishu ya bunge. Bajeti huandaliwa kutoka ngazi ya chini kabisa ili kuleta uwakilishi
Ilitakiwa iwe hivyo lakini siyo hivyo. Bajeti inatayarishwa, pesa zinakusanywa kuanzia huku chini ... lakini matumizi yanaamuliwa Dodoma. Mfano, Chato Airport iko kwenye bajeti ya mwaka gani ...!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…