Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?

Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?

Hope you're doing great.
Tuwekee chart ya government tuweze kujua kama unayosema yana taswiswi.

Ninachojua Rais ndo overroll wa watu.

Yuko hapo juu ya anaweza kukataa kile kilichoamuliwa kikaonekana kitaleta madhara kwa taifa
Anakuwa juu ya mihimuli mingine sababu ya ile "Ukuu wa nchi" (head of state) Kwa mujibu wa katiba.
 
Wanabodi
Hii ni makala kwenye gazeti la Mwananchi la Jumatano View attachment 2953461

Paskali

Uko sahihi, na haya madaraka ya urais kuwa juu ya katiba ndio yamesababisha udhaifu wa mihimili yote. Hiki cheo Cha rais ndio kinachobeba ile amri yenye nguvu kuliko Sheria na katiba, ile amri inayoitwa amri toka juu, asili yake kabisa ni madaraka ya rais. Hakuna chochote kinaweza kufanya kazi iwe Sheria au katiba, iwapo amri toka juu itakataa. Kama hatutaondoa madaraka ya rais yaliyo juu ya Sheria na katiba., hatutakaa tuwe na taasisi ama mihimili imara ndani ya nchi hii.
 
Katiba yetu ni ya Zamani

Ukiangalia modern na modelled kama Kenya constitution of 2010 na South Africa constitution of 1996 utaona kwamba president anawajibika sana kwa parliament mambo mengi ya anayotakiwa kufanya rais yanatakiwa kupitishwa na bunge
And thats how inatakiwa, ina act kama check and balance mechanism
 
Wanabodi
Hii ni makala kwenye gazeti la Mwananchi la Jumatano View attachment 2953461

Paskali
Kwa maana nyingine unataka kutuambia Tanzania ni nchi inayo ongozwa Kifalme? Tatizo ni sisi Watanzania wenyewe. Tunashabikia vitendo vya hovyo vinavyofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi kwa kujidanganya tunaikomoa Chadema. Katiba mpya ilikuwa inaipunguza kama si kuiondoa hii kitu.
 
Rais ndiye mwenyekiti wa chama tawala ambaye pia husimamia mchakato wa kumpata mgombea wa nafasi ya uspika. Spika akienda kinyume na matakwa ya mwenyekiti anaweza kupokwa uanachama na akapoteza ubunge na uspika.

Rais huyu huyu ndiye huteua jina la waziri mkuu kisha kuthibitishwa na bunge. Waziri mkuu ndiye msimamizi wa shughuli za serikali bungeni.

Muswada wowote lazima upite kwenye Kamati ya bunge uangaliiwe na kuridhiwa na serikali (kupitia waziri mkuu na mwanasheria wa serikali) ndipo upate kibali na utengewe muda na spika wa kujadiliwa bungeni .

Kwa mazingira hayo, rais tayari amepoka nguvu na mamlaka ya ibara ya 56A. Hakuna namna rais anaweza kuwajibishwa na bunge.
katiba ingewatoa Mawaziri,spika nje ubunge hapo ingekaa sawa. Waziri ateuliwe kutoka nje ya mhimili wa bunge
 
Wanabodi,

Hii ni makala kwenye gazeti la Mwananchi la Jumatano.

View attachment 2953461
Kwa wasomaji wapya, naendelea kutoa darasa kuhusu kuijua katiba ya JMT ya mwaka 1977, kwa jicho la Mtunga Katiba, alidhamiria nini alipoweka kifungu fulani. Wiki iliyopita nilizungumzia jinsi jinsi mihimili mitatu ya serikali, Bunge na Mahakama inavyopaswa kuheshimiana, lakini pia kusimamiana, na kudhibitiana, (The doctrine of Separation of Powers Checks and Balance) na kuleza jinsi Bunge la awamu zilizopita lilivyotunga kipengele batili, kinyume cha katiba, na japo Mahakama Kuu ya Tanzania ilitengua, ubatili huo, katika kuheshimiana kwa mihimili hii, Mahakama ya Rufaa ikaurejesha ubatili kwenye Mhimili wa Bunge, ili Bunge liloutenda ubatili huo ndio litengue, lakini Bunge letu Tukufu, limekula kobisi, (yaani limekaa kimya na kujikausha), hiyo ubatili huo bado imo ndani ya katiba yetu mpaka sasa!.

Japo Tanzania ina mihimili mitatu, ya Serikali, Bunge na Mahakama, na wakuu wa mihimili hii ni Rais wa JMT, ni mkuu wa mhimili wa serikali, Spika wa Bunge ni mkuu wa mhimili wa Bunge, na Jaji Mkuu ni mkuu wa mhimili wa mahakama, lakini kwa mfumo wetu, Rais wa JMT ndie mkuu kificho wa mihimili yote mitatu, Rais wa JMT ndie Mkuu wa serikali na Amiri Jeshi Mkuu, wa majeshi ya ulinzi na usalama, yaani mkuu wa dola.

Rais wa Tanzania ni sehemu ya Mahakama, kwa rais kumteua mkuu wa mhimili wa Mahakama, yaani, Jaji Mkuu, majaji na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, na mahakama inaweza kutoa adhabu yoyote, lakini rais wa JMT amepewa mamlaka ya kusamehe wafungwa wowote, na mahakama ikitoa adhabu kubwa kuliko zote, capital punishment, yaani adhabu ya kifo, adhabu hiyo haitekelezwi mpaka kwanza rais wa JMT, asaini death warrant yaani hati ya kifo, hivyo Rais ndio kila kitu kwenye mhimili wa Mahakama!.

Tukija kwenye mhimili wa Bunge, rais wa JMT ni sehemu ya Bunge kwa kuliunda, kulivunja, kuteua mtenjaji mkuu wa Bunge, na Katibu wa Bunge, na katika utungaji wa sheria, Bunge linatunga tuu sheria lakini sheria hizo haziwi sheria mpaka kwanza rais wa JMT, aridhie na kusaini ridhio hilo, accent, ndipo sheria inakuwa sheria, hivyo na kwenye mhimili wa Bunge, rais pia ndie kila kitu!.

Rais wa Tanzania, tukiisha mchagua, anaapishwa kwa kula kiapo cha kuilinda na kuiteteta katiba ya JMT, na kumuomba “Mungu nisaidie”, ili rais wetu aweze kutekeleza majukumu yake ya urais, katiba yetu imempa rais wetu kinga ya kutokushitakiwa kwa kosa lolote atakalo litenda katika kutekeleza majukumu yake ya urais, wakati akiwa madarakani, na kinga hiyo inaendelea hata baada ya kustaafu.

Hili la Kinga ya Rais kutokushitakiwa mahakamani, naomba tulipigie mstari, kinga ya rais kutokushitakiwa mahakamani, inahusu kosa lolote ambalo rais wa JMT, atalitenda katika kutekeleza majukumu yake ya kuuraisi tuu, hii maana yake, rais wa JMT, anaweza kushitakiwa mahakamani kwa kesi ya madai, au akitenda kosa jingine lolote ambalo sio la utekelezaji wa makumu yake ya urais, kwasababu rais pia ni binadamu, anaweza kutenda makosa ya kibinadamu, hivyo anaweza kushitakiwa kwa kesi ya madai, ila ni baada ya kumaliza kipindi chake cha urais.

Hivyo japo katiba yetu imempa kinga rais wa JMT, kutokushitakiwa kwa makosa yoyote atakayo yatenda, hii maana yake ni, rais wa Tanzania anaruhusiwa kutenda makosa ndio maana amewekewa kinga ya kutokushitakiwa.

Lakini katika kuonyesha ukuu wa katiba, uitwao constitutional supremacy, katiba ndio iko juu ya kila kitu, hata rais wa JMT japo yuko juu ya serikali, Bunge na Mahakama lakini yuko chini ya katiba, hii maana yake katiba ya JMT ndio iko juu ya kila kitu, hakuna aliye juu ya katiba, hata rais wa JMT yuko chini ya katiba.

Japo nimeeleza kule juu kuwa Rais wa JMT, anaruhusiwa kufanya makosa mengine yotote lakini rais wa JMT haruhusiwi kufanya kosa lolote la kukiuka katiba, kwasababu katiba iko juu yake. Hivyo katiba imeweka Ibara ya 56A, iwapo rais atakiuka katiba, anaweza kushitakiwa na Bunge na kuondolewa madarakani.

Kitendo cha serikali kupeleka Bungeni, muswada wenye kipengele batili, kinachokwenda kinyume cha katiba ya JMT, huu ni ukiukwaji wa katiba ya JMT. Kitendo cha Bunge kupokea muswada wenye kipengele batili kinyume cha katiba, na kukitunga kuwa sheria, pia huu ni ukiukwaji wa katiba ya JMT, na kitendo cha Rais wa JMT, ila mamlaka pekee yenye kuweza kutamka kipengele fulani ni batili na linakwenda kinyume cha katiba, ni Mahakama Kuu ya JMT.

Wiki ijayo nitaendelea kwa kukuletea hiyo sheria batili ni ipi, na ubatili wake ni upi, jinsi Mahakama Kuu ya Tanzania ilivyoitengua hiyo, sheria batili na nini kilitokea.

Paskali
Ripoti yako ni njema katika kukumbusha wanajamii maana sidhani kama kuna aliyetimamu hafahamu haya maswala. Ila Jifunze kuchapa ripoti yako kwa ufasaha wa maandishi mwandishi. Asante
 
Back
Top Bottom