Je, wajua kuwa Rais wa JMT ndie Serikali, Bunge na Mahakama? Yuko juu ya Mihimili yote 3. Je, kuna uwezekano Rais wa JMT pia yuko juu Katiba?

Ndio Rais yupo juu ya Katiba, amewekwa juu ya Katiba kwa kipengele cha kutomtaka ashtakiwe kwa makosa atakayotenda akiwa uongozini, hiyo maana yake ni sawa na kusema, Rais anaweza kwenda kinyume cha Katiba kwenye uongozi wake kwa kuivunja Katiba yenyewe na asishtakiwe popote.

Kwa muktadha huo, ukiniambia Rais yupo juu ya Katiba nakubaliana nawe.
 
Ripoti yako ni njema katika kukumbusha wanajamii maana sidhani kama kuna aliyetimamu hafahamu haya maswala. Ila Jifunze kuchapa ripoti yako kwa ufasaha wa maandishi mwandishi. Asante
Asante kwa angalizo, kitu gani sio fasaha?.
P
 
Kinga ya rais kutokushitakiwa inahusu
1. Makosa yoyote katika utekelezaji majukumu yake ya urais tuu, hivyo rais akifanya makosa mengine yoyote ambayo sio sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya urais, anashitakika.
2. Rais anakula kiapo cha kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, akikiuka katiba, anashitakiwa ila sio Mahakamani bali Bungeni. Ibara ya 56A.
P
 
Umenikumbusha swali ulilowahi kumuuliza Hatati MAGHUFURI Kwenye kikao Cha wahariri WA vyombo vya habari kama sikosei, Kuna swali uliuliza lenye mrengo huu
Alikutania Kwa Jina lako Kisha Akakuuliza
Nani anatafuta Hela kati ya SERIKALI ,mahakama na BUNGE😂😂😂
 
- Hata kama Rais akilewa akamchapa kofi yeyote uraiani, bado sioni akishtakiwa popote na hizi mahakama zao.

- Na bunge lile la Tulia kila siku kumpamba Rais, uje utokee muujiza lije kupiga kura ya kutokuwa na imani nae....!!! Utakuwa mwisho wa dunia.
 
Spika wa Afrika Kusini kapelekwa mahakamani Pretoria
 
Fahamu kuwa hii nakala yako inasomwa na umati mkubwa. Nashauri, pendelea kupitia uandishi wa sarufi kwani inakuongezea heshima kwa wasomaji kwa ujumla. Ni hayo tu ndugu mwandishi 📌
No one is perfect, nitakushukuru sana kama utaainisha kosa lolote la kisarufi katika andiko langu hili ili nijirekebishe.
P
 
Hope you're doing great.
Tuwekee chart ya government tuweze kujua kama unayosema yana taswiswi.

Ninachojua Rais ndo overroll wa watu.

Yuko hapo juu ya anaweza kukataa kile kilichoamuliwa kikaonekana kitaleta madhara kwa taifa
Kwenye organisation chart, rais ndio the top most, ila katiba ndio overall!. Kwa mujibu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977, rais wa JMT anaweza kukosea kosa lolote na anakinga ya kutokushitakiwa, ila akikiuka katiba, anashitakiwa kwa mujibu wa ibara ya 56A.
P
 
Na mtani wangu Paschal Mayalla akiwa mmojawapo wa kuinanga Demokrasia na Vyama vya Upinzani.
 
Mkuu Paskali
mpaka sasa mamlaka ya Rais imeshafanya mambo kadhaa ambayo ni questionable Kikatiba. Kwa mfano Rais anateua mtu kuwa Mbunge na kabla hajaapishwa kiapo cha ubunge anateuliwa na kuapishwa kuwa Waziri....

Wakati Dkt Shein anaapishwa muhula wa kwanza wa urais wa Zanzibar, Huku Bara alikuwa bado kikatiba anasomeka kuwa Makamu wa Rais wa JMT.....

Rais kuzuia shughuli za kisiasa hususan vyama pinzani kufanya shughuli halali za Kisiasa ni pigo kubwa dhidi ya Katiba

Mambo kama hayo na mengine mengi yanaleta ushawishi kuamini kuwa Rais yupo juu ya Katiba. Hata wewe kwenye baadhi ya makala zako humu umewahi kusema kuwa mambo kadhaa ikiwemo ruhusa ya mikutano ya kisasa kwa vyama vya siasa kwamba ni HISANI ya RAIS.... nilikupinga lakini ulifafanua kwa nini ni hisani. Hivyo swali hili lenye hoja makinika kuhusu Ukuu wa Urais dhidi ya Ukuu wa KAtiba naona kama vile unapaswa kuandika zaidi ya hiki. Lakini nimekuelewa.
 
Mkuu Paskali, inawezekana Rais Samia asiwe juu ya mihimili mingine?, na nini kifanyike ikiwa yuko juu ya hiyo mihimili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…