Najua Haters mtapinga tu hizo Amri za Shetani lakini Mwamba kapiga mle mle!! Mtapinga kwa ubishi tu, na wivu dhidi ya nondo za maana kwavile tumeaminishwa Mwamba sio kabisa, ingawaje kiuhaliisa, tunampigia shangwe... tena za kibingwa!
Ukweli usemwe, Mwamba hakukurupuka kama Bwana Yuleee!! Amri zake zimesimama na practical kuzidi hata zile alizotuletea Bwana Yule ambazo ni Impractical... hazitekelezeki maabara wala kwenye karakana!
Just imagine! Hakuna aliyekutaka ushauri wala kukuuliza lakini from nowhere"...oh, najua uukitaka kutoboa usawa huu, wekeza kwenye kilimo Kiongozi! Maparachichi yanalipa big time! Amini usiamini, parachichi ni Green Gold"
Pumbaaavu! Kwani we mwenyewe hutaki kutoboa? Ina maana huzitaki hizo Green Gold?! Kwamba Njombe wanakochimbua hizo green gold hukujui, ama?!
Nenda kalime mwenyewe hayo maparachchi, kenge wewe... kwani nimekuomba ushauri?
Unakuta mwingine hujamuuliza wala nini halafu eti anakushauri upande miti gani sijui ambayo kuivuna ni sawa na kifungo cha Sabaya!
Hivi zimetimia kweli wewe? Yaani kosa la babako aliyeshindwa kukulipia ada ya kusoma kozi uitakayo, na matokeo yake ukaishia kusomea Misitu SUA, halafu umeona mi ndo wa kunidondoshea jumba bovu? Unajifanya kutoa ushauri bila kuombwa ili upate sababu ya kupiga mizinga, sio?
Tena Wabongo kwa kupenda kutoa ushauri.... dah!!
Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni! Mwamba anajua! Unanipigia stori za matatizo yako kwani yananihusu nini wakati mwenyewe nina matatizo kibao?!
Nenda kasimulie kanisani au msikitini huko, kama nako hawajakuona tapeli tu!