utopolo og
JF-Expert Member
- Nov 29, 2022
- 575
- 1,575
Ingawa huu usemi umetamalaki kwenye sekta mbalimbali hasa za michezo hapa Tanzania, ila kama ulikuwa hujui basi chukua hii Leo.
Mwaka 1993 klabu ya Simba ilifika fainali ya michuano iliyoitwa Caf cup dhidi ya Stella Abidjan ya nchini Ivory coast.
Mchezo wa kwanza ulipigwa nchini Ivory Coast uliisha kwa suluhu, hivyo mechi ya marudia ilikuwa lazima mshindi apatikane
Simba walijiandaa vizuri na mchezo huu wa marudia na hamasa ilikuwa kubwa ambapo aliyekuwa mfadhili wa Simba wakati huo ndugu Azim Dewji aliwaahidi wachezaji wote kuwanunulia magari aina ya Toyota KIA endapo wangeshinda mchezo huo.
Siku ya mchezo ilifika na Uwanja wa taifa wa wakati huo( Uwanja wa Uhuru) ulijaa pomoni kuisapoti timu ya nyumbani simba
Stella Abidjan walipiga mpira mwingi sana na kuichabanga Simba 2-0 magoli yote yakiwekwa kimiani na Mshambuliaji wao hatari BOLIZOZO
Ndipo baada ya mchezo huo, mgeni rasmi akitoka jukwaa kuu huku akiwa amelowa kwa aibu kubwa baada ya kuona timu ya nyumbani inafungwa mbele yake na kombe linachukuliwa kwenye ardhi ya nyumbani alitoa kauli hii" TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU" maneno haya alikuwa akiwalenga Simba waliokubali kufungwa uwanja wa nyumban Tena mbele ya mashabiki wao.