Je, wajua kuwa Simba ndio ilisababisha Tanzania kuitwa kichwa cha Mwendawazimu?

Je, wajua kuwa Simba ndio ilisababisha Tanzania kuitwa kichwa cha Mwendawazimu?

utopolo og

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2022
Posts
575
Reaction score
1,575
Ingawa huu usemi umetamalaki kwenye sekta mbalimbali hasa za michezo hapa Tanzania, ila kama ulikuwa hujui basi chukua hii Leo.

Mwaka 1993 klabu ya Simba ilifika fainali ya michuano iliyoitwa Caf cup dhidi ya Stella Abidjan ya nchini Ivory coast.
Mchezo wa kwanza ulipigwa nchini Ivory Coast uliisha kwa suluhu, hivyo mechi ya marudia ilikuwa lazima mshindi apatikane

Simba walijiandaa vizuri na mchezo huu wa marudia na hamasa ilikuwa kubwa ambapo aliyekuwa mfadhili wa Simba wakati huo ndugu Azim Dewji aliwaahidi wachezaji wote kuwanunulia magari aina ya Toyota KIA endapo wangeshinda mchezo huo.

Siku ya mchezo ilifika na Uwanja wa taifa wa wakati huo( Uwanja wa Uhuru) ulijaa pomoni kuisapoti timu ya nyumbani simba

Stella Abidjan walipiga mpira mwingi sana na kuichabanga Simba 2-0 magoli yote yakiwekwa kimiani na Mshambuliaji wao hatari BOLIZOZO

Ndipo baada ya mchezo huo, mgeni rasmi akitoka jukwaa kuu huku akiwa amelowa kwa aibu kubwa baada ya kuona timu ya nyumbani inafungwa mbele yake na kombe linachukuliwa kwenye ardhi ya nyumbani alitoa kauli hii" TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU" maneno haya alikuwa akiwalenga Simba waliokubali kufungwa uwanja wa nyumban Tena mbele ya mashabiki wao.
 
Wanasiasa ndiyo waliivuruga Simba katika fainali ile. Dua Said, mchezaji wa Simba aliyekuwa katika kikosi kile aliyasema hayo wakati anachambua mechi moja hivi karibuni. Baada ya kuona Simba wanakaribia kuweka historia, wanasiasa walikuwa wanapishana kambini kujaribu kutafuta umaarufu kwa mgongo wa mafanikio ya timu kama wanavyofanya sasa wanavyoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kabla na baada ya mechi. Matokeo yake wanawachanganya na kuwachosha wachezaji kusikiliza mahotuba yao.

Ipe Simba heshima yake maana imefanya mengi kwa nchi hii. Ushabiki wa timu pinzani usikutoe ufahamu.
 
Kikosi cha simba cha wakati huo
screenshot_20200402-202043.jpg
 
Wanasiasa ndiyo waliivuruga Simba katika fainali ile. Dua Said, mchezaji wa Simba aliyekuwa katika kikosi kile aliyasema hayo wakati anachambua mechi moja hivi karibuni. Baada ya kuona Simba wanakaribia kuweka historia, wanasiasa walikuwa wanapishana kambini kujaribu kutafuta umaarufu kwa mgongo wa mafanikio ya timu kama wanavyofanya sasa wanavyoingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya mechi. Matokeo yake wanawachanganya na kuwachosha wachezaji kusikiliza mahotuba yao.

Ipe Simba heshima yake maana imefanya mengi kwa nchi hii. Ushabiki wa timu pinzani usikutoe ufahamu.
Wapi ufahamu wangu umetoka mkuu? Mbona bandiko liko wazi, wewe hutaki vijana wa kizazi hiki wajue maana halisi ya huu msemo na wapi chimbuko lake?
 
Kuna mtu alikua Mwenye kiti wa Simba kama sijasahau jina alikua akiitwa Amir Bamchawi, Yule Mzee kabla ya mechi alikua anatangaza njia ambazo kombe litapita.
Lile jukwaa kuu lote pale shamba labibi Lili pambwa na kanga zimeandikwa Simba Taifa kubwa.
Kulikua na Kila aina ya Vituko kabla ya mchezo.
Baada ya mechi kwisha Kuna mashabiki hawakuweza kutoka uwanjani mpaka saa mbili usiku Kwa namna Walivyo duwazwa wakiwa awa amini kilicho tokea.
 
Wapi ufahamu wangu umetoka mkuu? Mbona bandiko liko wazi, wewe hutaki vijana wa kizazi hiki wajue maana halisi ya huu msemo na wapi chimbuko lake?
Maana yake halisi ni wanasiasa kukimbia lawama pale wanapokuwa chanzo cha uharibifu.

Timu za taifa ndiyo zilikuwa hazifanyi chochote, utalinganisha na timu ambayo imefika fainali tena kwa juhudi za watu binafsi?
 
Kuna mtu alikua Mwenye kiti wa Simba kama sijasahau jina alikua akiitwa Amir Bamchawi, Yule Mzee kabla ya mechi alikua anatangaza njia ambazo kombe litapita.
Lile jukwaa kuu lote pale shamba labibi Lili pambwa na kanga zimeandikwa Simba Taifa kubwa.
Kulikua na Kila aina ya Vituko kabla ya mchezo.
Baada ya mechi kwisha Kuna mashabiki hawakuweza kutoka uwanjani mpaka saa mbili usiku Kwa namna Walivyo duwazwa wakiwa awa amini kilicho tokea.
Ndiyo mjue Simba wa sasa ni mwerevu maana amepitia machungu mengi. Kucheza na kombe la CAF uwanjani na kulikosa si jambo dogo, unachoshangaa nini? Kuna sababu kwa nini uzoefu unathaminiwa.

Kwenye mashindano yote duniani, kwenye mechi ya fainali kombe likiwa uwanjani timu zote zinajiandaa kwa ushindi ikiwemo kwa tshirt na shamrashamra zingine, nini cha ajabu hapo?
 
Ingawa huu usemi umetamalaki kwenye sekta mbalimbali hasa za michezo hapa Tanzania, ila kama ulikuwa hujui basi chukua hii Leo.

Mwaka 1993 klabu ya Simba ilifika fainali ya michuano iliyoitwa Caf cup dhidi ya Stella Abidjan ya nchini Ivory coast.
Mchezo wa kwanza ulipigwa nchini Ivory Coast uliisha kwa suluhu, hivyo mechi ya marudia ilikuwa lazima mshindi apatikane

Simba walijiandaa vizuri na mchezo huu wa marudia na hamasa ilikuwa kubwa kiasi cha kumwalika rais wa nchi wa wakati huo ndugu Ally Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi siku hiyo.
Pia Aliyekuwa mfadhili wa Simba wakati huo ndugu Azim Dewji aliwaahidi wachezaji wote kuwanunulia magari aina ya Toyota KIA endapo wangeshinda mchezo huo.

Siku ya mchezo ilifika na Uwanja wa taifa wa wakati huo( Uwanja wa Uhuru) ulijaa pomoni kuisapoti timu ya nyumbani simba

Stella Abidjan walipiga mpira mwingi sana na kuichabanga Simba 2-0 magoli yote yakiwekwa kimiani na Mshambuliaji wao hatari BoLi Zozo

Ndipo baada ya mchezo huo, raisi Ali Hassan Mwinyi akitoka jukwaa kuu huku akiwa amelowa kwa aibu kubwa baada ya kuona timu ya nyumbani inafungwa mbele yake na kombe linachukuliwa kwenye ardhi ya nyumbani alitoa kauli hii" TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU" maneno haya alikuwa akiwalenga Simba waliokubali kufungwa uwanja wa nyumban mbele ya rais wa nchi Yao.
Kwenye hii mechi kuna mwamba alikuwa anaitwa BOLIZOZO,aliwakimbiza Simba hakuna mfano. Huyu mtu alikuwa maarufu zaidi ya rais wa nchi.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Kuna wapuuzi wenzenu wa Simba uwa muda wote Wana mwimba Chama.
Pale Simba viungo wajuu walikua Husen Marsha, George Lucas (Gaza), Michael Paul (nailon) Kwa uwezo walio kua nao Uyu Chama wenu wa Sasa hata Viatu vya ao watu haruhuaiwi kuvibeba achana na kukaa Bench.
Pale Yanga 1993 viungo vessel tile Issa athuman, Method Mogela , Stephen Musa. Hamis Tobias Gaga anasubiri sub Kwa Stephen Musa.
Ao jamaa Kwa uwezo walio kuanao Feisal wasasa ata Bench hakai.
 
Hii haifuti ukweli kwamba simba anahistoria kubwa kimataifa kuliko utopolo. Usione leo hii simba anaenda kushiriki super cup ukafikiri ni kwa sababu ilya kujaza mashabiki uwanjani ndio kigezo. Mizizi ya simba imejikita mbali sana kimataifa ikiwemo kupitia aibu na misukosuko mingi.
 
Wapi ufahamu wangu umetoka mkuu? Mbona bandiko liko wazi, wewe hutaki vijana wa kizazi hiki wajue maana halisi ya huu msemo na wapi chimbuko lake?
Kuna mtu alikua Mwenye kiti wa Simba kama sijasahau jina alikua akiitwa Amir Bamchawi, Yule Mzee kabla ya mechi alikua anatangaza njia ambazo kombe litapita.
Lile jukwaa kuu lote pale shamba labibi Lili pambwa na kanga zimeandikwa Simba Taifa kubwa.
Kulikua na Kila aina ya Vituko kabla ya mchezo.
Baada ya mechi kwisha Kuna mashabiki hawakuweza kutoka uwanjani mpaka saa mbili usiku Kwa namna Walivyo duwazwa wakiwa awa amini kilicho tokea.
Wakuu asanteni kwa historia mi nasoma tu wala sijui mengi kuhusu mpira
 
Nilivyofika pale kwenye ahadi ya magari niligundua Azim Dewji alitoa ahadi ambayo hata Simba wangeshinda angeshindwa kuitekeleza maana hayo magari wakati huo hayakuwepo duniani na hadi leo hayajawahi kutengenezwa(hizo Toyota Kia).
Hata hivyo Rais Mwinyi alitoa kauli hiyo kutokana na matokeo mabaya ya mara kwa mara kwa timu yetu ya taifa wakati huo sio Simba,acha uongo.
 
Hii haifuti ukweli kwamba simba anahistoria kubwa kimataifa kuliko utopolo. Usione leo hii simba anaenda kushiriki super cup ukafikiri ni kwa sababu ilya kujaza mashabiki uwanjani ndio kigezo. Mizizi ya simba imejikita mbali sana kimataifa ikiwemo kupitia aibu na misukosuko mingi.
Ndio mfungwe mbele ya raisi wa nchi na kombe likapepea? Halafu Simba haijawahi kuwa na mafanikio yoyote ya kimataifa.
Ninachojua ni Simba imepiga hatua fulani kimataifa ila haijawahi kufanikiwa popote kwenye angaza izo za kimataifa..

Pia hata hili caf cup kumbe lilikuwa ni bonanza tu lililofadhiliwa na Dikteta Moshood Abiola na sio kama mnavyojinasibu kuwa mlifika fainali kombe la shirikisho.
 
Back
Top Bottom