Je, wajua kuwa Simba ndio ilisababisha Tanzania kuitwa kichwa cha Mwendawazimu?

Wewe hujui humu watoto Wengi umri kuanzia miaka 24..mwaka 1994 Wengi hawajazaliwa...why ulete utani wa kutunga uongo???na kuharibu history na kumsingizia Mzee Mwinyi kitu sio cha kweli??
Mkuu huu uongo umekuumiza kama ulivyoniumiza mimi
 
Huu ndio ukweli,mleta mada acha kupotosha,wakongwe tunakuchora tu.
 
Wahindi wenzie walimuweka chini na kumuhusia aachane na mpira na kugawa fedha kwa ngoz nyeusi, ikabid hapo nyuma wachache wahongwe kuruhusu magoli ili kunusuru Tajiri kupoteza fedha kwa kugawa magari kwa wachezaji!
 
Wahindi wenzie walimuweka chini na kumuhusia aachane na mpira na kugawa fedha kwa ngoz nyeusi, ikabid hapo nyuma wachache wahongwe kuruhusu magoli ili kunusuru Tajiri kupoteza fedha kwa kugawa magari kwa wachezaji!
Mkuu mbona Azim aliwapo magari wachezaji wa Simba pamoja na kupoteza mechi ila hayakua magari ya KIA ambayo enzi zile yalitumika kama Daladala maarufu kama Chai maharage,

Aliwapa magari madogo ila wachezaji wengine waliamua kuchukua hela.
 
Kombe la Caf ni kombe la kimashindano kama lilivyokuwa kombe la klabu bingwa Afrika.na kombe la washindi (wakati huo) na kombe hilo msimu huo ndio ulikuwa msimu wake wa kwanza
na kombe hilo lilitolewa na mfanyabiashara maarufu wa huko Nigeria ambaye baadaye aligombea urais na kushinda kabla Dikteta Jenerali wa jeshi Sani Abacha kuchukuwa madaraka kwa nguvu na kumkamata na hatimaye kumuua Abiola akiwa gerezani.
Sasa sijui udikteta wa huyo mfanyabiashara Mashoud Abiola unatokea wapi!
N.b: Kombe la Caf na lile la Washindi mashindano yake yaliunganishwa na kuzaliwa kombe la shirikisho.
 
Kuna striker alikua akiitwa Bolizozo, huyo ndiye alipelekea kilio Msimbazi.
Kwa mara ya kwanza Simba na Yanga waliungana na wote kuishabikia Simba kwa nguvu sana.
Simba walipopigwa goli la kwanza, pale uwanjani hali haikubadilika amsha amsha za kuuhimiza Simba zilikua juu sana zikifanywa na mashabiki wa Simba na Yanga.
Hali ilibadilika pale Bolizozo alipotupia goli la pili, Yanga wakaona hawa jamaa vipi? Mbona badala ya kucheza mpira wanakati viuno na kuruhusu goli ziingie kiurahisi ?
Ghafla Yanga wakabadilika na kuanza kuimba "Uzalendoo, umetushinda" na kuanza kuishangilia Stella Abidjan ya Ivory Coast. Hapo wachezaji wa Simba kusikia hivyo wakabomoka kabisa kisaikolojia na kupoteza matumaini huku wakicheza bora liende mpira uishe.
Baada ya ile mechi ya fainali, Stella Abijan waliondoka na kombe. Ilipokuja kupigwa mechi ya Simba na Yanga, jina la Bolizozo likahamishiwa kwa mchezaji James Tungaraza wa Yanga baada ya kuwatungua Simba.
Michuani hiyo ilikua ikidhaminiwa na Bilionea wa Nigeria Moshood Kashimawo Olawale Abiola (Mashood Abiola).

Kuhusiana na jina la "Kichwa Cha Mwendawazimu", kumbukumbu zangu kama vile zinaniambia liliongelewa wakati wachezaji wa timu ya Tanzania Stars ambao walishinda Kombe la FAT walipokuwa wakikabidhiwa kombe hilo kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye moja ya michuano ya CAF.
 
Wahindi wenzie walimuweka chini na kumuhusia aachane na mpira na kugawa fedha kwa ngoz nyeusi, ikabid hapo nyuma wachache wahongwe kuruhusu magoli ili kunusuru Tajiri kupoteza fedha kwa kugawa magari kwa wachezaji!
walizitumia timu kuuza ngada,kipindi hicho ndiyo Simba ilikua inaenda nje kila mchezaji na mpira wake,wakirudi wanarudi na mpira mmoja,maswali yakaanza ya mipira mingine ilipo!?..ndiyo wakaziacha timu,yule wa upande wa pili yeye alikua anapenga kabisa,ukamuondoa nadhani dozi ilizidi
 
Dewji aliuza hyo mechi kwa pesa ndefu kuna mzee mmoja alikuwa anasimulia siku moja.
 
Wenye akili timamu huko uto ni wawili tu hivyo tusishangae kwa nyuzi za kibwegebwege kama hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…