Je, wajua kuwa Simba ndio ilisababisha Tanzania kuitwa kichwa cha Mwendawazimu?

Je, wajua kuwa Simba ndio ilisababisha Tanzania kuitwa kichwa cha Mwendawazimu?

Wewe hujui humu watoto Wengi umri kuanzia miaka 24..mwaka 1994 Wengi hawajazaliwa...why ulete utani wa kutunga uongo???na kuharibu history na kumsingizia Mzee Mwinyi kitu sio cha kweli??
Mkuu huu uongo umekuumiza kama ulivyoniumiza mimi
 
Nilivyofika pale kwenye ahadi ya magari niligundua Azim Dewji alitoa ahadi ambayo hata Simba wangeshinda angeshindwa kuitekeleza maana hayo magari wakati huo hayakuwepo duniani na hadi leo hayajawahi kutengenezwa(hizo Toyota Kia).
Hata hivyo Rais Mwinyi alitoa kauli hiyo kutokana na matokeo mabaya ya mara kwa mara kwa timu yetu ya taifa wakati huo sio Simba,acha uongo.
Huu ndio ukweli,mleta mada acha kupotosha,wakongwe tunakuchora tu.
 
Hivi Dua alikuwepo!?..aliyeiponza ni mfadhili,alihonga baadhi ya wachezaji, fullback ya kulia ilikua uchochoro kusudi tu,mwameja akimlaumu 'mbona unamuacha huyo anapita tu'!?..hapo Azim dewji alijifanya anaumwa,kalazwa hospitali muda wote wa maandalizi
Wahindi wenzie walimuweka chini na kumuhusia aachane na mpira na kugawa fedha kwa ngoz nyeusi, ikabid hapo nyuma wachache wahongwe kuruhusu magoli ili kunusuru Tajiri kupoteza fedha kwa kugawa magari kwa wachezaji!
 
Wahindi wenzie walimuweka chini na kumuhusia aachane na mpira na kugawa fedha kwa ngoz nyeusi, ikabid hapo nyuma wachache wahongwe kuruhusu magoli ili kunusuru Tajiri kupoteza fedha kwa kugawa magari kwa wachezaji!
Mkuu mbona Azim aliwapo magari wachezaji wa Simba pamoja na kupoteza mechi ila hayakua magari ya KIA ambayo enzi zile yalitumika kama Daladala maarufu kama Chai maharage,

Aliwapa magari madogo ila wachezaji wengine waliamua kuchukua hela.
 
Ndio mfungwe mbele ya raisi wa nchi na kombe likapepea? Halafu Simba haijawahi kuwa na mafanikio yoyote ya kimataifa.
Ninachojua ni Simba imepiga hatua fulani kimataifa ila haijawahi kufanikiwa popote kwenye angaza izo za kimataifa..

Pia hata hili caf cup kumbe lilikuwa ni bonanza tu lililofadhiliwa na Dikteta Moshood Abiola na sio kama mnavyojinasibu kuwa mlifika fainali kombe la shirikisho.
Kombe la Caf ni kombe la kimashindano kama lilivyokuwa kombe la klabu bingwa Afrika.na kombe la washindi (wakati huo) na kombe hilo msimu huo ndio ulikuwa msimu wake wa kwanza
na kombe hilo lilitolewa na mfanyabiashara maarufu wa huko Nigeria ambaye baadaye aligombea urais na kushinda kabla Dikteta Jenerali wa jeshi Sani Abacha kuchukuwa madaraka kwa nguvu na kumkamata na hatimaye kumuua Abiola akiwa gerezani.
Sasa sijui udikteta wa huyo mfanyabiashara Mashoud Abiola unatokea wapi!
N.b: Kombe la Caf na lile la Washindi mashindano yake yaliunganishwa na kuzaliwa kombe la shirikisho.
 
Ingawa huu usemi umetamalaki kwenye sekta mbalimbali hasa za michezo hapa Tanzania, ila kama ulikuwa hujui basi chukua hii Leo.

Mwaka 1993 klabu ya Simba ilifika fainali ya michuano iliyoitwa Caf cup dhidi ya Stella Abidjan ya nchini Ivory coast.
Mchezo wa kwanza ulipigwa nchini Ivory Coast uliisha kwa suluhu, hivyo mechi ya marudia ilikuwa lazima mshindi apatikane

Simba walijiandaa vizuri na mchezo huu wa marudia na hamasa ilikuwa kubwa ambapo aliyekuwa mfadhili wa Simba wakati huo ndugu Azim Dewji aliwaahidi wachezaji wote kuwanunulia magari aina ya Toyota KIA endapo wangeshinda mchezo huo.

Siku ya mchezo ilifika na Uwanja wa taifa wa wakati huo( Uwanja wa Uhuru) ulijaa pomoni kuisapoti timu ya nyumbani simba

Stella Abidjan walipiga mpira mwingi sana na kuichabanga Simba 2-0 magoli yote yakiwekwa kimiani na Mshambuliaji wao hatari BOLIZOZO

Ndipo baada ya mchezo huo, mgeni rasmi akitoka jukwaa kuu huku akiwa amelowa kwa aibu kubwa baada ya kuona timu ya nyumbani inafungwa mbele yake na kombe linachukuliwa kwenye ardhi ya nyumbani alitoa kauli hii" TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU" maneno haya alikuwa akiwalenga Simba waliokubali kufungwa uwanja wa nyumban Tena mbele ya mashabiki wao.
Kuna striker alikua akiitwa Bolizozo, huyo ndiye alipelekea kilio Msimbazi.
Kwa mara ya kwanza Simba na Yanga waliungana na wote kuishabikia Simba kwa nguvu sana.
Simba walipopigwa goli la kwanza, pale uwanjani hali haikubadilika amsha amsha za kuuhimiza Simba zilikua juu sana zikifanywa na mashabiki wa Simba na Yanga.
Hali ilibadilika pale Bolizozo alipotupia goli la pili, Yanga wakaona hawa jamaa vipi? Mbona badala ya kucheza mpira wanakati viuno na kuruhusu goli ziingie kiurahisi ?
Ghafla Yanga wakabadilika na kuanza kuimba "Uzalendoo, umetushinda" na kuanza kuishangilia Stella Abidjan ya Ivory Coast. Hapo wachezaji wa Simba kusikia hivyo wakabomoka kabisa kisaikolojia na kupoteza matumaini huku wakicheza bora liende mpira uishe.
Baada ya ile mechi ya fainali, Stella Abijan waliondoka na kombe. Ilipokuja kupigwa mechi ya Simba na Yanga, jina la Bolizozo likahamishiwa kwa mchezaji James Tungaraza wa Yanga baada ya kuwatungua Simba.
Michuani hiyo ilikua ikidhaminiwa na Bilionea wa Nigeria Moshood Kashimawo Olawale Abiola (Mashood Abiola).

Kuhusiana na jina la "Kichwa Cha Mwendawazimu", kumbukumbu zangu kama vile zinaniambia liliongelewa wakati wachezaji wa timu ya Tanzania Stars ambao walishinda Kombe la FAT walipokuwa wakikabidhiwa kombe hilo kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye moja ya michuano ya CAF.
 
Wahindi wenzie walimuweka chini na kumuhusia aachane na mpira na kugawa fedha kwa ngoz nyeusi, ikabid hapo nyuma wachache wahongwe kuruhusu magoli ili kunusuru Tajiri kupoteza fedha kwa kugawa magari kwa wachezaji!
walizitumia timu kuuza ngada,kipindi hicho ndiyo Simba ilikua inaenda nje kila mchezaji na mpira wake,wakirudi wanarudi na mpira mmoja,maswali yakaanza ya mipira mingine ilipo!?..ndiyo wakaziacha timu,yule wa upande wa pili yeye alikua anapenga kabisa,ukamuondoa nadhani dozi ilizidi
 
Dewji aliuza hyo mechi kwa pesa ndefu kuna mzee mmoja alikuwa anasimulia siku moja.
 
Wenye akili timamu huko uto ni wawili tu hivyo tusishangae kwa nyuzi za kibwegebwege kama hizi
 
Back
Top Bottom