Je, wajua kwanini mwaka mpya huwa ni tarehe 1 january na siku ya wajinga ni tarehe 1 Aprili?

def_xcode

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
2,551
Reaction score
6,837
Kabla ya mwaka 1582, jamii nyingi zilikuwa zinaadhimisha mwaka mpya tarehee 1 Aprili. Kumbuka karne hiyo papa alikuwa na nguvu kubwa ya kuamua chochote. Mnamo mwaka 1582, papa Gregory XIII akaamua kubadilisha kwamba mwaka mpya utasheherekewa inapofika tarehe 1 Januari.
Kuna watu hawakukubaliana na hilo wakaendelea kusheherekea mwaka mpya tarehe 1 Aprili. Hivyo wakaanza kuitwa wajinga na ndipo tarehe 1 Aprili ikageuka kuwa siku ya wajinga.
Hivyo epuka kusheherekea vitu usivyo kuwa na uelewa navyo.
 
Inakuaje waislam wanakuwa na kalenda yao ya mwaka wa kiislam lakini wakitaja matukio yao hawaachi kutumia kalenda hii tunayotumia wote? Kuna haja gani waislam kutumia kalenda yao ya kiislam pamoja na hii ya gregorian wakati ya kiislam haifuatwi na watu wengi? Mbona kama waislam wanajichanganya kutumia kalenda mbili, si bora watumie moja?
 
Ni kama standard tu ili tuweze kuelewana haijalishi kwa dini, tamaduni au background zetu, basi tunarejelea hii. Ni kama wachina vile nao wa new year yao pia tofauti na ya kwetu.
Kusingekuwa na standard si tungekuwa na mvurugano mkuu
 
Halafu ni mwalimu na anauliza swali kama hili ambalo hata mwanafunzi wa darasa la pili anaweza kulijibu kwa ufasaha. Kwa hali hii sijui huko shuleni anakofundisha kukoje
 
najua kwa nini unatokwa povu kuhusu kuuliza, mwenzio kajibu kiungwana bila kuleta dharau. Unadhani walimu wanajua kila kitu?
 
Back
Top Bottom