Je, Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo Kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?

Je, Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo Kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?

Wenzetu akina nani?! Si ndio hao ambao wamewahi kuniuliza ikiwa waislamu wakifikwa chooni lazima wapate kiu ya maji?! Nina umri wa miaka 47 na miaka 20 nimeishi na jamii ya wakristo huko kwetu Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera.
Mama yangu (Allaah amrehemu) alisilimu miaka michache kabla mimi sijazaliwa kwa hiyo wajomba zangu na familia zao Bado ni wakristo.
Swala la wakristo kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia limeanza siku za karibuni na ni kwa wakristo wanaoishi miji ya pwani kama Dar, ZNZ , Tanga na Mtwara.
Wakristo waliopo Vijijini kama huko marangu Kilimanjaro au Uyole huko Mbeya hawana habari ya kujisafisha na maji.
Acha uongo huo wewe, usafi binafsi hauna cha uislam wala Ukristo , mchafu ni mchafu tu. Dini zinafundisha na kuhimiza usafi wa miili na mioyo, watu huchagua waishi vipi halafu mnakuja na assumptions zenu hapa. Unadhani watu hatujaishi Pemba na Unguja? Mpaka vyakula unhisi kinyaa kula. Mnapenda kuongea jumlajumla sababu ya ukosefu wa taarifa na maarifa ndiyo maana mnakwepa kuchanganua mambo. Kama mama yako na wajomba zako walikuwa hawana utamaduni wa kujitawaza hiyo ni wao na tabia zao, siyo mafundisho ya dini yao hayo
 
Hahaha kaka kujisafisha siyo Uislamu, lile nitendo anafanya hata mpagani.

Huko vijiji nilivyotoka mimi maji ni ya shida sana, lakini wote waislamu na wakristo tulikuwa tunatumia vyoo vya shimo.

Na kumbuka hatakuwa hata na uwezo wa kupata hizi toilet paper, sijui tulikuwa tunatumia nini, nimesahau, lakini haikuwa maji.

Usafi ni swala binafsi, sidhani kama ni la dini fulani.
 
Kwa huu uzi ulivyo na logic yake ni hakika kuwa huyu Pascal Mayalla ana akili ndogo sana 🙄🙄 toilet paper siyo ukristo wala uislam ni mambo ya mageuzi ya kiuchumi kisayansi na kitekinolojia ...wakristo na waislamu wote walikuwa wanatumia maji miaka ya kale ...hivyo mada imekosewa kilogic ilitakiwa kusema wakristo wameacha kutumia maji kujisafisha na kutumia toilets paper wakati waislam wanaendeleza kutumia kutumia maji...mleta uzi kashindwa kujua kuwa zama zimebadilika sikuizi watu wanatumia toilets paper kisha wanatumia na maji pia..... ndiyo maana hata ujenzi wa vyoo vya kisasa kuna kijibomba cha kisasa cha kukishika mkononi cha kujisafishia tofauti na kutumia kopo... hata kwenye vyoo vya sgr kipo hicho kijibomba ....kazi ya toilet paper siyo kujisafishatu bali na kujikausha majimaji hivyo ni sahihi kutumia maji na toilet paper kwa,pamoja ...kanuni ni moja mbili tatu yaani ukishatoka kujisaidia tumia toilet paper kisha maji kisha tumia tena toilet paper kujikausha maji...badala ya kuponda toilet paper ni vizuri kufuata huu mfumo ulio sahihi zaidi ya kutumia maji tu au kutumia toilet paper tu ...hivyo tuwa fundishe wanao tumia maji tu na wanao tumia toilet paper tu kutumia vyote viwili kwa hiyo formation niliyo sema ya 1..2..3

💥💥THREAD CLOTHER📌📌📌📌
Nchi kama UK hawana hicho kijibomba cha kutawazia au kusafishia kwenye vyoo vyao. Kama wanaweka basi huo utaratibu umeanza hivi karibuni kwani ilikuwa hairuhusiwi na unaweza kupigwa faini kubwa sana.

Wanaamini kwamba utumiaji wa hivyo vibomba vinaweza kupelekea kinyesi kuingia kwenye bomba na kuchafua maji kwa sababu mifumo ya maji kwenye nyumba zao imeungana.

Wanatumia toilet paper kwa sababu vyoo vyao ni vya kukaa siyo vya kuchuchumaa kwa hiyo ni ngumu kutumia maji kutawaza kutokana na kwamba ni marufuku kuweka vijibomba vya kujisafishia.

Hata hivyo, hili suala limekaa kiutamaduni sana na siyo kiusafi kama mleta mada alivyosema. Siamini kwamba nchi ya watu zaidi ya milioni 60 wote ni wachafu na hawajui kutawaza kisa tu wanatumia toilet paper.

Vilevile, waafrika hasa watanzania hatujawahi kuwa na utamaduni au taratobu zetu zinazojitosheleza ndo maana tulishobokea tamaduni za watu bila kufikiria na tumekuwa watumwa.
 
Siku nyingine mkuu anzisha mada, asilimia kubwa nnaokutananao mijini au vijijini wanakula vitafunio, vinywaji kwa kutumia mkono wa kushoto, mkono wa kupambana na uchafu wa aina yote. Badilikeni.
Tena hujiona wamelatia maisha eti wanasema waislamu wanakula mkono wa kulia so wao is better to use lefthand side haaaa full maisha ya kwenye movies
 
Hii ni mada ya swali Je Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, kuna uwezekano Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?.
We mzee, hiyo research yako umeifanya kweli au umeamua tu kuwapa credit kobaz?. Hawa watu hawafai😂😂😂 huwa wanatumia hadi mawe na michanga. Kipindi tupo shule choo kilikuwa kinaziba kisa mawe hawa jamaa wanatumia kujisafishia
 
Naunga mkono hoja 100%, Mimi niingia chooni hakuna maji hata hizi airport za wenzetu na nunua maji safi ila hapa bongo nadhani sote tunatumia maji majumbani kwetu waislamu na wakristo. Umenipa ushawishi kutaka kujuwa nyumba za wakristo Tz haweki maji chooni? Mimi sina uhakika sana na hili naomba kusaidiwa. Wa Kenya wa bara kweli hawa maji hawajui lakini pwani wanatumia maji. Naomba kujuzwa tu hapa Tz nyumba za waislamu zina maji na wakristo hakuna? sitaki kuamini maana wa Tz huu ni ustaarabu wetu wa maji bila kujali dini.
Sio maji tu, Wakristo wanatumia maji pamoja na tissue paper
 
We mzee, hiyo research yako umeifanya kweli au umeamua tu kuwapa credit kobaz?. Hawa watu hawafai😂😂😂 huwa wanatumia hadi mawe na michanga. Kipindi tupo shule choo kilikuwa kinaziba kisa mawe hawa jamaa wanatumia kujisafishia
Research yake ameifanyia huko kwao Usukumani
 
Wenzetu akina nani?! Si ndio hao ambao wamewahi kuniuliza ikiwa waislamu wakifikwa chooni lazima wapate kiu ya maji?! Nina umri wa miaka 47 na miaka 20 nimeishi na jamii ya wakristo huko kwetu Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera.
Mama yangu (Allaah amrehemu) alisilimu miaka michache kabla mimi sijazaliwa kwa hiyo wajomba zangu na familia zao Bado ni wakristo.
Swala la wakristo kujisafisha kwa maji baada ya kujisaidia limeanza siku za karibuni na ni kwa wakristo wanaoishi miji ya pwani kama Dar, ZNZ , Tanga na Mtwara.
Wakristo waliopo Vijijini kama huko marangu Kilimanjaro au Uyole huko Mbeya hawana habari ya kujisafisha na maji.
Sio kweli. Sisi tulikuwa tunatawaza mtoni kwa maji kabla hujazaliwa mpaka sasa
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa, huja na kwa maslahi ya taifa.

Mimi kama mwandishi wa habari, ni muelimishaji umma, ukiona jambo zuri la jamii fulani, waelimishe na wengine wafuate.

Hii ni mada ya swali Je Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, kuna uwezekano Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?.

Jambo la leo ni usafi binafsi wa mwili, baada ya kupunguza uzito, wenzetu Waislamu na nchi za Kiislamu, wanatumia maji kujiswafi, lakini Wakristo na nchi za Kikisto wanatumia karatasi laini, toilet paper, kujiswafi kwa kujifuta baada ya ile shughuli, hapa nauliza ni kujifuta au pia kujipaka?.

Hizi dini kuu zote mbili, Wakristo na Waislamu, ni watoto wa baba mmoja Nabii Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mzaliwa wa kwanza, Ismail, na Wakristo wa ni uzao mzaliwa wa pili, Isaka. Sheria ya Mungu wa dini zote mbili ni sheria moja ya Musa iliyoshushwa kwenye torati.

Kwenye sheria hiyo, Mungu alielekeza namna ya kujiswafi, kabla hujaenda mbele zake na kuelekeza kabisa, lazima unawe kwa maji tiririka!.

Ukristo ulipoingia, wakabadili baadhi ya mambo, ikiwemo kutumia karatasi laini kujiswafi baada ya ile shughuli. Katika pita pita yangu nchi nyingi za Kiislamu, kwenye public toilets zao, kuna maji tiririka, lakini kwenye nchi za Kikristo, kuna TP!.

Sisi Tanzania kwasababu nchi yetu haina dini, public toilets zetu zina both, maji tiririka na TP. Ukisafiri kutokea Dar kwenda Dubai, Doha, Muscat, UAE, kote huko kwenye public toilets zao, utakuta maji tiririka, na TP. Ukienda SA, London, Paris, New York, kwenye public toilets zao, kuna TP only hakuna bomba lolote la maji!.

Japo TP inasafisha, kwa vile ni kavu, inasafisha kwa kupaka, huwezi kulinganisha na maji tiririka ambayo yanasafisha kabisa compared to TP.

Kwa vile sheria ya usafi wa mwili imeelekezwa kidini, na ni Waislamu wanaitekeleza kama Mungu alivyoelekeza, hivyo kuna uwezekano kwenye usafi wa mwili, tukubali tukatae, Waislamu ni wasafi zaidi kuliko Wakristo, na kwa kulijua hilo na umuhimu wa usafi, wanawake wa kisasa wenye kujijali, wanatembea na wipes, na nyumba nyingi za kisasa wanatumia maji tiririka.

Kwa wenzetu Waislamu, wale hata wale wenzetu wao, wakiwa kwenye hali fulani ile, huwa hawafungi na hawaruhusiwi kwenda kuswali Masjid au Msikitini, lakini sikuwahi kusikia hili kwa Wakristu, hivyo wenzetu wale, hata wakiwa kwenye ile hali, wanatinga tuu ibadani mbele za Mungu!, hivyo inawezekana kwenye usafi binafsi, wanawake wa Kiislamu ni wasafi kuliko wanawake wa kikristo?.

Tena usikute usafi huu kwa Waislamu sio usafi tuu wa mwili, ni mpaka moyo na roho, ndio maana wanawake wa Kiislamu wanaweza kuvumilia na kustahimili uke wenza, na ingefanywa survey ya ni wanawake gani akiwa mama wa kambo, anatesa watoto wa aliyemtangulia, a wicked stepmother, mngeshangazwa na matokeo.

Kuna vitu vingi wazungu wametupotosha sisi Wakristo ikiwemo hoja ya mke mmoja, sio mpango wa Mungu, ndio maana nilimpongeza yule Blaza wangu na kumshauri "Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?"

Nani aliwaambia wazungu na nchi za Kikristo TP tuu inatosha?.

Nimepandisha bandiko hili kufuatia mimi ni mpenda kula kula vyakula locals kila ninaposafiri, Uliwahi kula vyakula gani kutoka sehemu mbalimbali Duniani ukafaidi? sasa sometimes, tumbo linachafuka ukiwa safarini, inakubidi ujiswafi kwa maji tiririka, tumbo linapokutibuka, ukakuta hakuna maji ni TP pekee ni shughuli, hivyo nimekereka sana na hili!. Hawa wazungu vipi?.

WHO wanapaswa watoe muongozo na maelekezo, public washrooms zote lazima ziwe na maji tiririka na TP, ili wale wa kunawa, wawe huru wanawe na wale wa kujipaka, waendelee kujipaka!.

Paskali
Rejea za mleta mada kuhusu Waislamu na Wakristo
Pascal! Leo umepatwa na mkasa gani!
Baada ya kuisoma Post yako niliona kabla ya kuijibu nianzie kwenye maduka ambayo wakiristu wananunua hizo karatasi za kuchambia, bahati mbaya huku uswahilini kwetu hazipo nikajua utakuwa unamaanisha wakirisitu wanatumia mabunzi! Huku uswahilini hakuna magazeti na ulemtindo wa kusyanata(sic) yaani ukishamaliza haja unasogea pembeni unakaa chini kisha unafanya kama unapiga pasi, nao hawezekani kwani nyumba zina sakafu ya simenti.
Baada ya haya nimeshindwa kuwajua wakirisitu unaowazungumzia.
 
Nchi kama UK hawana hicho kijibomba cha kutawazia au kusafishia kwenye vyoo vyao. Kama wanaweka basi huo utaratibu umeanza hivi karibuni kwani ilikuwa hairuhusiwi na unaweza kupigwa faini kubwa sana.

Wanaamini kwamba utumiaji wa hivyo vibomba vinaweza kupelekea kinyesi kuingia kwenye bomba na kuchafua maji kwa sababu mifumo ya maji kwenye nyumba zao imeungana.

Wanatumia toilet paper kwa sababu vyoo vyao ni vya kukaa siyo vya kuchuchumaa kwa hiyo ni ngumu kutumia maji kutawaza kutokana na kwamba ni marufuku kuweka vijibomba vya kujisafishia.

Hata hivyo, hili suala limekaa kiutamaduni sana na siyo kiusafi kama mleta mada alivyosema. Siamini kwamba nchi ya watu zaidi ya milioni 60 wote ni wachafu na hawajui kutawaza kisa tu wanatumia toilet paper.

Vilevile, waafrika hasa watanzania hatujawahi kuwa na utamaduni au taratobu zetu zinazojitosheleza ndo maana tulishobokea tamaduni za watu bila kufikiria na tumekuwa watumwa.
Watu wanapenda kukimbilia kuandika bila kufanya reasoning ya kina. Kuonyesha kwamba usafi huo siyo jambo la dini yoyote ile, ndiyo maana jamii zoto kutumia mkono wa kushoto siyo jambo la kawaida sababu mkono wa kushoto kwa shughuli unaohusishwa nazo, basi kuutumia kula huonekana ni uchafu, na kuutumia kumsalimia mtu ni kama dharau.

Hayo ni mafunzo ndani ya familia, siyo dini.
Kazi kuu ya kwanza ya mkono wa kushoto ni kuiisafisha baada ya kutoka haja, inashangaza Pascal Mayalla na wafuasa wake wanavyokuja na poor agenda and reasoning, au mwenzetu Pascal hadi kazi ya mkono wa kushoto ni alijifunzia misikitini?
Mimi nakumbuka tukiwa wadogo huko vijijini watu wakienda kujisaidia maporini walitumia either majani kujisafisha, au au kujiburuza chini au makaratasi (haya tulikuwa tunakazwa kutumia sababu ya kupeperushwa na upepo), .

kuna kipindi ikaamriwa watu wanapoenda kuchunga wawe wanabeba vijembe vidogo/mbisu (vile vya kupalilia) kwa ajili ya kuchimba shimo, akimaliza kujisaidia anafukia lengo ni ili waache kujisaidia n kuacha vinyesi wazi huko kwani maporini kulikuwa na harufu kali au wengine nao wakiwa wanapita au wanachunga wanajikuta wanakanyaga vinyesi vya wenngine.

Leo kuna mtu kwa kuwa hay yote hakuyaona ndani ya familia, jamii na kabila lao, anakuja kudhani ni shauri ya dini.

Kwa wengi hizo toilet paper ni kwa ajili ya kazi mbili, moja baada ya kujisaidia inatangulia, halafu yanafuata maji, then wanamalizia toilet paper kujikausha.
 
Back
Top Bottom