Je, Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo Kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?

Acha uongo huo wewe, usafi binafsi hauna cha uislam wala Ukristo , mchafu ni mchafu tu. Dini zinafundisha na kuhimiza usafi wa miili na mioyo, watu huchagua waishi vipi halafu mnakuja na assumptions zenu hapa. Unadhani watu hatujaishi Pemba na Unguja? Mpaka vyakula unhisi kinyaa kula. Mnapenda kuongea jumlajumla sababu ya ukosefu wa taarifa na maarifa ndiyo maana mnakwepa kuchanganua mambo. Kama mama yako na wajomba zako walikuwa hawana utamaduni wa kujitawaza hiyo ni wao na tabia zao, siyo mafundisho ya dini yao hayo
 
Hahaha kaka kujisafisha siyo Uislamu, lile nitendo anafanya hata mpagani.

Huko vijiji nilivyotoka mimi maji ni ya shida sana, lakini wote waislamu na wakristo tulikuwa tunatumia vyoo vya shimo.

Na kumbuka hatakuwa hata na uwezo wa kupata hizi toilet paper, sijui tulikuwa tunatumia nini, nimesahau, lakini haikuwa maji.

Usafi ni swala binafsi, sidhani kama ni la dini fulani.
 
Nchi kama UK hawana hicho kijibomba cha kutawazia au kusafishia kwenye vyoo vyao. Kama wanaweka basi huo utaratibu umeanza hivi karibuni kwani ilikuwa hairuhusiwi na unaweza kupigwa faini kubwa sana.

Wanaamini kwamba utumiaji wa hivyo vibomba vinaweza kupelekea kinyesi kuingia kwenye bomba na kuchafua maji kwa sababu mifumo ya maji kwenye nyumba zao imeungana.

Wanatumia toilet paper kwa sababu vyoo vyao ni vya kukaa siyo vya kuchuchumaa kwa hiyo ni ngumu kutumia maji kutawaza kutokana na kwamba ni marufuku kuweka vijibomba vya kujisafishia.

Hata hivyo, hili suala limekaa kiutamaduni sana na siyo kiusafi kama mleta mada alivyosema. Siamini kwamba nchi ya watu zaidi ya milioni 60 wote ni wachafu na hawajui kutawaza kisa tu wanatumia toilet paper.

Vilevile, waafrika hasa watanzania hatujawahi kuwa na utamaduni au taratobu zetu zinazojitosheleza ndo maana tulishobokea tamaduni za watu bila kufikiria na tumekuwa watumwa.
 
Siku nyingine mkuu anzisha mada, asilimia kubwa nnaokutananao mijini au vijijini wanakula vitafunio, vinywaji kwa kutumia mkono wa kushoto, mkono wa kupambana na uchafu wa aina yote. Badilikeni.
Tena hujiona wamelatia maisha eti wanasema waislamu wanakula mkono wa kulia so wao is better to use lefthand side haaaa full maisha ya kwenye movies
 
Hii ni mada ya swali Je Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, kuna uwezekano Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?.
We mzee, hiyo research yako umeifanya kweli au umeamua tu kuwapa credit kobaz?. Hawa watu hawafai😂😂😂 huwa wanatumia hadi mawe na michanga. Kipindi tupo shule choo kilikuwa kinaziba kisa mawe hawa jamaa wanatumia kujisafishia
 
Sio maji tu, Wakristo wanatumia maji pamoja na tissue paper
 
We mzee, hiyo research yako umeifanya kweli au umeamua tu kuwapa credit kobaz?. Hawa watu hawafai😂😂😂 huwa wanatumia hadi mawe na michanga. Kipindi tupo shule choo kilikuwa kinaziba kisa mawe hawa jamaa wanatumia kujisafishia
Research yake ameifanyia huko kwao Usukumani
 
Sio kweli. Sisi tulikuwa tunatawaza mtoni kwa maji kabla hujazaliwa mpaka sasa
 
Pascal! Leo umepatwa na mkasa gani!
Baada ya kuisoma Post yako niliona kabla ya kuijibu nianzie kwenye maduka ambayo wakiristu wananunua hizo karatasi za kuchambia, bahati mbaya huku uswahilini kwetu hazipo nikajua utakuwa unamaanisha wakirisitu wanatumia mabunzi! Huku uswahilini hakuna magazeti na ulemtindo wa kusyanata(sic) yaani ukishamaliza haja unasogea pembeni unakaa chini kisha unafanya kama unapiga pasi, nao hawezekani kwani nyumba zina sakafu ya simenti.
Baada ya haya nimeshindwa kuwajua wakirisitu unaowazungumzia.
 
Watu wanapenda kukimbilia kuandika bila kufanya reasoning ya kina. Kuonyesha kwamba usafi huo siyo jambo la dini yoyote ile, ndiyo maana jamii zoto kutumia mkono wa kushoto siyo jambo la kawaida sababu mkono wa kushoto kwa shughuli unaohusishwa nazo, basi kuutumia kula huonekana ni uchafu, na kuutumia kumsalimia mtu ni kama dharau.

Hayo ni mafunzo ndani ya familia, siyo dini.
Kazi kuu ya kwanza ya mkono wa kushoto ni kuiisafisha baada ya kutoka haja, inashangaza Pascal Mayalla na wafuasa wake wanavyokuja na poor agenda and reasoning, au mwenzetu Pascal hadi kazi ya mkono wa kushoto ni alijifunzia misikitini?
Mimi nakumbuka tukiwa wadogo huko vijijini watu wakienda kujisaidia maporini walitumia either majani kujisafisha, au au kujiburuza chini au makaratasi (haya tulikuwa tunakazwa kutumia sababu ya kupeperushwa na upepo), .

kuna kipindi ikaamriwa watu wanapoenda kuchunga wawe wanabeba vijembe vidogo/mbisu (vile vya kupalilia) kwa ajili ya kuchimba shimo, akimaliza kujisaidia anafukia lengo ni ili waache kujisaidia n kuacha vinyesi wazi huko kwani maporini kulikuwa na harufu kali au wengine nao wakiwa wanapita au wanachunga wanajikuta wanakanyaga vinyesi vya wenngine.

Leo kuna mtu kwa kuwa hay yote hakuyaona ndani ya familia, jamii na kabila lao, anakuja kudhani ni shauri ya dini.

Kwa wengi hizo toilet paper ni kwa ajili ya kazi mbili, moja baada ya kujisaidia inatangulia, halafu yanafuata maji, then wanamalizia toilet paper kujikausha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…