Je, Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo Kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?

Pia wasio jitawaza vizuri wakati wa kuoga si wanajisafisha vizuri ? Kuhusu kukataza hicho kibomba mbona logic ya maelekezo yao siyo sahihi maana hata maji ya kuflash choo yanaweza kuingiza uchafu kwenye huo mfumo ...hata maji ya kunawia mikono baada ya kujisafisha na toilet paper yanaweza kuingiza huo uchafu ...hata maji ya kibomba cha kuoga kile cha kushika mkononi wakati wa kuoga kinaweza kuingiza huo uchafu ...maana wakati wa kuoga mambo yote ya usafi ufanyika ikiwa ni pamoja na kujisafisha hayo maeneo kwa maji ....kama nilivyo sema njia sahihi na iliyo bora na yenye kuwafunika wote wanao tumia maji tu na wanao tumia toilet paper tu ni kutumia njia ZOTE MBILI YAANI UNATUMIA KWANZA TOILET PAPER KUJIFUTA KISHA UNAKUJA KUTUMIA MAJI KUJISAFISHA KIKAMILIFU KISHA UNAMALIZIA TOILET PAPER KUJIKAUSHA .
 
Kwa USAFI WA MWILI OK
JE USAFI WA MOYO?
 
Wewe ushamba wa kisukuma na uchawa vinakutesa. Swala la chooni ni uamuzi wa mtu binafsi wala halina uhusiano wowote na dini wala mwenyezi Mungu. Hivi ni karne ya 21 badirikeni
 
Ndugu Pascal Mayalla ,
Yalipoingia Magonjwa Makubwa Kama Bubonic Plague, tunajua Nini kiliikumba Europe.( Maradhi Yanaweza kuingia popote Hilo silikatai, ila measures za kujikinga dhidi ya ugonjwa huo inaweza kusaidia sana).
Sifikirii Dini kuwa inawafanya watu kutojisafisha (kwa maana usafi ni jadi ya mtu au asili ya kabila) ila Dini inaweza kutoa maelekezo mazuri juu ya kuhimiza watu kuwa wasafi, hali ambayo baadhi ya wanasayansi wanaamini kuwa kule kutawadha (kuanzia kuosha mikono mpaka miguu mara tano kwa siku) kuliwalinda na magonjwa Yale ya kuambukiza.

Kama uliwahi kukisoma kitabu Cha How Europe Underdeveloped Africa, Cha yule Mmarxist (Walter Rodney) anazungumzia kadhia hii pale aliponukuu Maneno kutoka kwa mwanafalsafa mmoja aitwaye Ibn Khaldun Alisema;

"Wakati Chuo Kikuu Cha Oxford kinaamini kuwa Kuoga ni jambo la hatari sana kwa Afya ya Mwanadamu, Watu WA Maghreb (Tunisia,Algeria na Morocco) kwenye miji Yao walikuwa na mabafu na watu walikuwa wakijitwaharisha(kujisafisha kimwili).
Naomba kuwasilisha.
 
Katika mambo ya Imani kiroho Bado mdogo sana WAIKRISTO Wanaenenda kiroho WAISLAM KIMWILI
 
Katika mambo ya Imani kiroho Bado mdogo sana WAIKRISTO Wanaenenda kiroho WAISLAM KIMWILI
Mkuu Chinchiler , kwanza asante kuchangia mchango wako wa maana kwenye uzi wangu huu,

Ni kweli katika mambo ya Imani za kiroho, mimi bado
ni mdogo sana.
Bandiko hili ni kuhusu usafi wa kawaida kabisa wa mwili baada ya kupunguza uzito na sio kujiswafi kwa ajili ya kujitoharisha kwa ajili ibada.

Je, Wajua Kwenye Usafi wa Mwili, Waislamu ni Wasafi Zaidi ya Wakristo?. Waislamu Hujiswafi kwa Maji, Wakristo Kwa Karatasi!, Huku Sio Kujipaka?​

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…