Je, Wajua ma-Pharao wa Misri wana asili ya Afrika Mashariki na hawana uhusiano wowote na waarabu?

Je, Wajua ma-Pharao wa Misri wana asili ya Afrika Mashariki na hawana uhusiano wowote na waarabu?

Uko sahihi..Ila nitakupa ufafanuzi zaidi usio na shaka.
Katika Misri aliwahi kutokea mwandishi maarufu ''sribe'' aliyeitwa Hunefer. Kabla hajafa aliacha maandiko yanayoeleza asili ya waMisri wa wakati wake.
Aliandika hivi
''We came from the beginning of the Nile where the god Hapi dwells, at the foothills of the mountains of the moon.''
Wataalamu wengi wanaamini alikuwa anaongelea eneo la maziwa makuu na milima yenye barafu ya Kilimanjaro na Ruwenzori.
Egypt (Kemet): The Egyptian Book of the Dead-Admissions Of Faith & Purity(The So-Called Negative Confessions)-Part 1
..what u mean? mto nile umeanzia m/kilimanjaro or what?
 
Usipotoshe..Firauni alikuwa ni Pharao wa enzi za Mtume Muhammad. Ma-farao katika historia ya Misri ni wengi sana.toka enzi za Mtume Musa.na hata kabla yake.Ukiwahesabu katika ''dynasties'' ni wengi mno.
Na Firauni enzi za Mtume Muhammad alishakuta pyramid zimejengwa.
Huyu Pharao Ramses III aliishi miaka elfu moja kabla ya hata Yesu mwenyewe hajazaliwa.
Kwa kifupi ..Yesu aliyakuta ma-pyramid yashajengwa miaka elfu iliyopita ..na akawa anayashangaa kama sisi tunavyoyashangaa.Mtume Muhammad alikuja miaka 500 baada ya Yesu.
kiswahili cha 'Pharaoh' ni kipi?
 
Kuna dhana pia kwamba weusi wa ngozi ya mafarao si hoja. Hoja ni kwamba maarifa yao ya ujuzi wa hesabu (mf. pai na kanuni ya Pythagoras), Elimu ya nyota (Astrology), Astronomia, uhandisi na ujenzi yaliingiliana sana na maarifa ya Waroma na Wagriki wa kale. Wengine wanakwenda mbali zaidi na kudai kwamba mawazo hayo kwa kiasi kikubwa yalitoka Roma na Ugriki ya kale.

Kama hivi ndivyo, hoja hii kengeufu inaendelea, japo mafarao hawa na Wamisri walikuwa Afrika na inawezekana ni kweli walikuwa weusi tititi kiteknolojia na kisayansi walikuwa wamefungamana na Roma na Ugriki ya kale. Ndiyo maana ujuzi na ugunduzi unapungua kwa jinsi unavyozidi kwenda Kusini mbali zaidi na Roma na Ugriki. Kwa hivyo basi, wanahitimisha watetezi wa hoja hii, maendeleo yote ya kisayansi na kiteknolojia yaliyotokea Afrika ya Kaskazini hayawezi kutengwa na mvuvumko wa kimaendeleo uliokuwa umejitandaza katika eneo hilo na chanzo chake kikiwa Roma na Ugriki ya kale.

Kuna ukweli katika hoja hii au ni zile juhudi za kimakusudi za kumdogosha mtu mweusi na kumfanya ajione kuwa hana mchango wo wote wa maana katika historia ya dunia wala maendeleo yake hasa kisayansi na kiteknolojia?
 
Last edited:
Jamaa umenifurahisha...eti labda ni Mshana Jr...! Mshana ni mtata sana mambo yake....pengine ni kweli...udhaniavo!
Asante mkuu. Hata hivyo naona umeninukuu vibaya. Ni "labda na wa Mshana Jr". Siyo Ni Mshana Jr. Kuna tofauti kubwa!
 
Kuna dhana pia kwamba weusi wa ngozi ya mafarao si hoja. Hoja ni kwamba maarifa yao ya ujuzi wa hesabu (mf. pai na kanuni ya Pythagoras), Elimu ya nyota (Astrology), Astronomia, uhandisi na ujenzi yaliingiliana sana na maarifa ya Waroma na Wagriki wa kale. Wengine wanakwenda mbali zaidi na kudai kwamba mawazo hayo kwa kiasi kikubwa yalitoka Roma na Ugriki ya kale. Kama hivi ndivyo, hoja hii kengeufu inaendelea, japo mafarao hawa na Wamisri walikuwa Afrika na inawezekana ni kweli walikuwa weusi tititi kiteknolojia na kisayansi walikuwa wamefungamana na Roma na Ugriki ya kale. Ndiyo maana ujuzi na ugunduzi unapungua kwa jinsi unavyozidi kwenda Kusini mbali zaidi na Roma na Ugriki. Kwa hivyo basi, wanahitimisha watetezi wa hoja hii, maendeleo yote ya kisayansi na kiteknolojia yaliyotokea Afrika ya Kaskazini hayawezi kutengwa na mvuvumko wa kimaendeleo uliokuwa umejitandaza katika eneo hilo na chanzo chake kikiwa Roma na Ugriki ya kale.

Kuna ukweli katika hoja hii au ni zile juhudi za kimakusudi za kumdogosha mtu mweusi na kumfanya ajione kuwa hana mchango wo wote wa maana katika historia ya dunia wala maendeleo yake hasa kisayansi na kiteknolojia?
Ukweli ni huu..na kila anaeisoma thread hii alifahamu hili. Egypt ya ma-Pharao weusi ndio jamii ya kwanza kutumia Pythagoras theorem,ingawaje wao wamisri hawakuiita hivyo. Wagiriki wamejifunza kuandika na kusoma kutoka kwa Wamisri. Wakati wa-Egypt wanajenga mahekalu kwa tofali na kuvaa mavazi ya hariri wazungu wa ulaya walikuwa bado wanaishi kwenye mapango na kuvaa ngozi za wanyama.
Pythagoras mwenyewe alienda Misri kusoma..akaja akaibuka na hiyo theorem. Lakini kiukweli si yake ,ni ya wa Misri.
Ushahidi huu hapa
''Thales advised Anaximander's student,Pythagoras, to visit Egypt in order to continue his studies in mathematics and philosophy.''

Biography of Thales - math word definition - Math Open Reference
Biography of Pythagoras - math word definition - Math Open Reference

Ushahidi ni mwingi mno
Egypt: origin of the Greek culture
 
Last edited:
Ngozi nyeusi ni kama carbon ipo tangia dunia inaumbwa.

Kwa sisi tulio wengi tumeaminishwa na mafundisho na vitabu vya watu weupe,yaani wazungu na waarabu, kuwa ma-Pharaoh wa Misri walikuwa ni watu wenye asili kama ya kwao ,na kwamba ma-pyramid yalijengwa na jamii iliyokuwa na maendeleo ya hali ya juu sana ,na haiwezekani hata kidogo watu hao wakawa ni watu weusi,yaani waafrika.
Hata Ma-freemason/illuminati wanatumia sana alama za ma-pyramid-ishara yakuwa watu hawa hawakuwa wa kawaida.
Aibu imewakuta ...watu weupe ma-egyptologist walioamini mtu mweusi -negro,hana uwezo wa hata kuwa na maarifa yanayo fanana na Egypt ya ma-pyramid..wameumbuka.
DNA ya Pharaoh Ramses III imethibitisha farao huyu alikuwa mweusi piiiii,tena asili yake ni hapa Afrika mashariki..DNA yake imepewa jina.. inaitwa E-V38. Kinasaba hiki kinapatikana sana kwenye damu za wanaume wa Afrika mashariki,na si kwingineko.
Why Hollywood Thinks the Pharaohs Were White
ukweli ndo huu
Haplogroup E-V38 - Wikipedia, the free encyclopedia
Ma-Pharaoh ni ndugu zetu,tena wa damu.
Wanasema waingereza ''Science doesn't lie''
 
pumba kabisa wewe!..kwani yesu alikuwa dini gani?

Jigo
Uko sahihi kabisa..Yesu hakuwa mkristo..alikuwa ni myahudi mpaka siku anaondoka duniani. na wala hakuacha dini inayoitwa ya ''wakristo''.

Ukristo ulianzishwa na wanafunzi na wafuasi wake.Yesu Mnazareti mpaka siku zake za mwisho alisali kutumia Torati. Na wala agano jipya New Testament halikuandikwa na Yesu.
The Origin of Christianity - Biblical Archaeology Society
Msingi wa Biblia ni masimulizi ya wale waliomuona au kumsikia.
SparkNotes: Bible: The New Testament: Context
 
dini ya kiyahudi, waliamini katika torati. ukristu ulikuja miaka ya baadae baada ya yesu mwenyewe kufa
Yesu Mnazareti hakuwa mkristo..Alikuwa anasali kiyahudi na alitumia torati kuhubiri.Ukristo ulianzishwa na wanafunzi na wafuasi wake baada ya Yesu kuondoka. Na wakati ukristo unaanza wakristo hawakuwa na kitabu chao.Yesu hakuwaachia maandiko yoyote zaidi ya mafundisho tu. Wanafunzi wake walianzisha ukristo kwa kutumia Torati .
The Origin of Christianity - Biblical Archaeology Society
 
weeee! Waakikusikiaaaa.....wenyewe wanasema Ibrahim alikua Mwislam japo Mohammed alizaliwa miaka 500 baada ya Yesu, tena wanasema hata Adam Na Eva walikua Islam!
Eti unasema mtume Muhammad alikuja miaka 500 baada ya Yesu kristo?
Hakika kweli nimeamini ukristo ndio dini ya kweli hao wengine ni taasisi za ujanja ujanja
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Usipotoshe..Firauni alikuwa ni Pharao wa enzi za Mtume Muhammad. Ma-farao katika historia ya Misri ni wengi sana.toka enzi za Mtume Musa.na hata kabla yake.Ukiwahesabu katika ''dynasties'' ni wengi mno.
Na Firauni enzi za Mtume Muhammad alishakuta pyramid zimejengwa.
Huyu Pharao Ramses III aliishi miaka elfu moja kabla ya hata Yesu mwenyewe hajazaliwa.
Kwa kifupi ..Yesu aliyakuta ma-pyramid yashajengwa miaka elfu iliyopita ..na akawa anayashangaa kama sisi tunavyoyashangaa.Mtume Muhammad alikuja miaka 500 baada ya Yesu.

Mkuu Farao au Firauni si jina bali ni cheo kama vile King Mfalme Kuhani na kadhalika.
Na kwa taarifa yako Mtume Muhammad hakukutana na yule firauni mkorofi kwani kipindi cha Nabii musa ndio kilimaliza ufirauni wake na kuja firauni wengi e ambao ni moderate na walikuwa watawala zaidi kuliko huyu aliyejifanya god king!
 
Mkuu Farao au Firauni si jina bali ni cheo kama vile King Mfalme Kuhani na kadhalika.
Na kwa taarifa yako Mtume Muhammad hakukutana na yule firauni mkorofi kwani kipindi cha Nabii musa ndio kilimaliza ufirauni wake na kuja firauni wengi e ambao ni moderate na walikuwa watawala zaidi kuliko huyu aliyejifanya god king!
Hayo ni maelezo yako kwa mujibu wa Quran. Kumbuka neno Firauni katika Quran linafananishwa na mtawala/mfalme asie fuata maelekezo ya mtume wa kiyahudi Musa. Kumbuka pia katika Quran Mtume Muhammad anamsimulia zaidi Pharao wa enzi za Mtume Musa ..kuliko Pharao (Roman Emperor) aliemkuta yeye katika uhai wake.
 
Back
Top Bottom