Je Wajua Mchezo wa Mieleka Uliwahi Kuwepo Hapa Nchini?

Je Wajua Mchezo wa Mieleka Uliwahi Kuwepo Hapa Nchini?

Kijana wa leo akisikia mieleka anaweza kudhani ni mchezo unaochezwa tu huko marekani na akina John Cena, The Undertaker, CM Punk n.k.

Nipo hapa kukujuza kuwa huo mchezo ulikuwa moja ya michezo maarufu hapa nchini miaka ya nyuma (hadi kufikia miaka ya tisini hivi). Mchezo ulichezwa kwenye viwanja hivihivi ambavyo leo vinatumiwa kucheza mpira wa miguu. Watu wakiingia biwanjani kwa kulipa viingilio km ilivyo leo hii unavyoenda uwanja wa mpira kutazama mchezo wa mpira wa miguu, basketball, ngumi n.k.

Wachezaji wake walijulikana kwa jina la "PAWA" kwa kiswahili likimaanisha mtu mwenye "NGUVU" ambayo kiingereza chake ni "POWER". Hawa wachezaji walikuwa na miili mikubwa iliyojengwa na misuli 'muscles' (na sio ule unene wa nyama uzembe). Mchezo wenyewe uliitwa mieleka na ukihusisha wachezaji husika kupimana mbavu kwa kusukumana hadi pale mmoja alipozidiwa nguvu na mwenzake. Power walicheza michezo mingine iliyohusisha matumizi makubwa ya nguvu km kuvuta na kuzuia magari, pikipiki n.k.

Kwa baadhi ya nchi hasa za Afrika hasa Afrika Magharibi bado mchezo huu unachezwa km sehemu ya michezo ya jadi.

Baadhi ya power maarufu wa kipindi hicho walikuwa ni power mabula huyu alikuwa msukuma, power bukuku "mwalafyale" huyu alitokea mkoa wa mbeya, power suzuki huyu alitokea songea ruvuma. Yule power iranda ambaye kwa sasa anamkochi bondia kiduku wa morogoro alikuwa mmojawapo wa hao power ndomaana hadi leo amebakia na hilo jina la power.

Mchezo huo ulififia taratibu na hatimaye kupotea kabisa machoni mwa watanzania katikati ya miaka ya tisini. Uwepo wa baadhi ya wadau kama huyo Power iranda na wengineo unaweza kutumiwa kuurejesha mchezo huo nchini ili nao ukachangia ajira kwa vijana wa leo.

Wakale una kumbuka nini kuhusu mchezo wa mieleka?

Unawakumbuka Power yupi wa kipindi hicho?

Chao!
Babalao mwenyewe alikuwa Power Mabula.

Power Mabula alikuwa anavuta gari kwa meno 🤣🤣🤣
 
Mieleka bafo ipo, nimetoka kusechi youtube nawaona wakurya wa Tarime wanapenda huu mchezo


 
Mara ya mwisho nakumbuka niliangalia pambano kati ya Sangandele na Sumu ya mamba, Pamoja na kufanyiwa sana promo mpambano haukuwa na mvuto kabisa.
 
Back
Top Bottom