Kwa mujibu wa report ya CAG deni la taifa Kwa miaka minne pekee ya uwepo wa Rais Samia madarakani ni zaidi ya Trilioni 30. Kwa mujibu wa maelezo ya wasemaji mbalimbali wa serikali pesa hizo zimetumika kujenga shule, hospitali, barabara na miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mpaka sasa Tanzania ina jumla ya mikoa 31, Wilaya 184, Kata 3,956, Vijiji 12,319.
SHULE
1.Kama fedha hiyo ingetumika kujenga madarasa, kwa wastani gharama ya chumba kimoja cha darasa tuseme ni milioni 20. Hivyo tungeweza kupata jumla ya vyumba milioni 10. Yaani kila kata ingeweza kuwa na vyumba 2,782. Hiyo ni zaidi ya shule complete 278 kwa kila kata. Mind you sio kwamba hizo kata hazikuwa na shule kabla, Bali hizo zingekuwa shule mpya kabisa nchi nzima.Kwa maana nyingine mtoto hatembei zaidi ya hatua 10 kufika shule.
HOSPITALI/ZAHANATI
Tuseme kwa wastani, kituo kimoja cha afya/hospitali kinagharimu milioni 200. Na tuseme Trilioni kadhaa zilitumika kujengea madarasa imebaki Trilioni 25. Ukigawanya unapata hospitali/vituo vya afya 125,000 standard kabisa na kila kata ingekuwa na vituo 32 vya afya! Je, kwenye kata yako kuna vituo vingapi vya afya?
MIRADI YA MAJI
Kwa wastani mradi mmoja mkubwa wa maji unagharimu Bilioni 2. Tuseme ukitoa fedha za madarasa ma zahanati/hospitali, tumebaki na Trilioni 20. Hii inatosha kwa miradi mikubwa 10,000 yaani kila kata ina miradi mikubwa walau 2. Hii inatosha si tu kwa maji ya nyumbani, bali kwa umwagiliaji! Yaani kwa maana nyingine maji ya kutosha kwa kiasi kikubwa mno! Yaani kila mtanzania mmoja anaweza kumiliki bomba lake la maji peke yake! Je, hali ikoje mahali ulipo?
UJENZI WA BARABARA
Kwa wastani kilimita 2.2 za barabara ya lami yenye hadhi ya barabara kuu, au hadhi ya kimataifa kabisa, inagharimu takribani Tsh bilioni 1. Kwa kiasi cha Trilioni zilizokopwa, Tungekuwa na zaidi ya kilomita 66,000 ya barabara nzuri sana za lami nchi nzima( kumbuka si kwamba hapakuwa na barabara za lami hapo kabla) Kwa kilomita hizo, hata kwenda nyumba ya jirani kila mtanzania alitakiwa akanyage lami.Yaani hadi njia za uchochoroni zilipaswa kuwa lami. Je, hali ikoje hapo ulipo?
VIWANDA VIDOGO
Haoa tunazungumzia viwanda vidogo kama vile kiwanda cha kuchakata katani, mafuta, mbolea, chai nk.
Tuseme kwa wastani kiwanda kimoja kinagharimu takriban Bilioni 3. Kwa kiasi cha mkopo kilichokopwa, Tungekuwa na viwanda vidogo zaidi ya viwili kila kata na chenchi ya uendeshaji wa kila kiwanda ingebaki na ajira kadhaa zingezalishwa.
Je, hapo ulipo umezungukwa na viwanda vingapi katika kata yako?