Je, Wajua mkopo uliokopwa katika awamu ya sita pekee ungetosha kufanya haya

Wewe inaonyesha Kama huna akili
Yaani miaka 60 trillion 60
Alafu Unataka kulinganisha na miaka 4 trillion 30 sawa na wastani wa trillion 7 Kila mwaka

Alafu huoni tatizo kweli , uko timamu upstairs mkuu ???
Hazilingani hata kidogo!
Ni kwamba Mama amekopa saaana anayebisha hilo ndo hana akili.
Swali langu bado liko palepale, hizo 60T walizokopa watangulizi wake kwa nini hazikumaliza shida za waTz kama tunavyoaminishwa 30T zingemaliza matatizo yetu yote?
 
Issue ni kwamba Samia ni kwamba Samia kashindwa kumaliza Matatizo ya waTZ kwa 30T ndo nikauliza kwa nini zile more than 60T hazikumaliza shida zetu? Au ziliisha ila Mama baada ya kuingia ndo shida zimeanza kujitokeza?
Nyie walamba asali mnapokuja kumtetea mama yenu kwenye mijadala kama hii ambayo kuna wachangiaji wengi wenye akili timamu, basi angalau muwe mna kuja na logic na sio kuandika tu upumbavu ilmradi unatetea....

Unavyolinganisha deni la 60T lilikopwa kwa mika takribani 60 na deni la 30T lilikopwa kwa miaka minne tu point yako ni nini hasa? Kwamba kwa vile hao watangulizi wake licha ya kukopa walishindwa kuyamaliza hayo matatizo basi ni sahihi tu hata Samia na yeye kushindwa kama walivyoshindwa wao licha ya yeye kukopa mapesa meengi ndani ya muda mfupi sio??? Is this how you reason?

Mantiki iliyopo kwenye hii mada ni kwamba pesa ambayo imekopwa ndani ya miaka 4 ya Samia haiendani kabisa na magnitude ya maendeleo au miradi ambayo imefanyika, oya 30T ni nyingi mno ilitosha kabisa kumaliza hayo matatizo madogo madogo kama ujenzi wa madarasa, kusambaza umeme na maji kwa kila kaya, pamoja na miradi mingine mikubwa endapo kama fedha hiyo ingesimamiwa vizuri kwenye utumikaji wake....

...kilichopo hapa ni kwamba mama Abduli akishakopa tu pesa na kutoa maagizo hizi pesa zitumike vipi basi ndio anakuwa amemaliza, hana muda wa kufuatilia kama maagizo yake yametimizwa kwa usahihi, na hata akijua kama kuna ubadhirifu hakuna anachofanya zaidi ya kulalamika tu, na ndio maana tunasema serikali yake inafuga majizi na mafisadi ambao nahisi nawe pia ni mmoja wao.

Samia ni raisi mzuri anayejua kuendesha nchi kulingana na wakati, lakini hili taifa halimfai, hili taifa linahitaji mtu ambaye ana energy ya kufuatilia kila jambo linalohusu mustakabali wa maendeleo katika kila hatua, kitu ambacho Samia hana... aina ya mtu kama Samia alistahili kuja kuiongoza Tanzania hata 2060 huko baada ya kuwa tayari tumeshaweka mifumo imara ya kiuongozi isiyompa raisi kazi kubwa ya kukimbizana na wabadhirifu wa mali za uma...

...the notion that Samia ni fisadi kama mafisadi wengine bado sijakubaliana nayo kwa 100% ninachojua mimi yeye ameruhusu walafi walifisadi taifa hili kama fadhila ya wao kumtetea hili aendelee kubaki madarakani akitembea na hofu kwamba yanaweza kumkuta yale ya mtangulizi wake.

Kuna muda binafsi huwa simlaumu sana kwa yanayoendelea hapa nchini, maana hakujiandaa kuwa raisi ilitokea tu akaokota dodo chini ya makarutusi, hivyo basi analazimika kufuata ushauri wa watu ambao ndio hao walafi wasiokuwa na nia njema na taifa hili, na hiyo miaka mitano mingine anayoiomba ndio mambo yatakuwa ovyo sana kuliko hata hivi sasa.

Nimalize tu kwa kusema kama raisi Samia anataka kutunza heshima yake, huu ndio uwe mwaka wake wa mwisho kuliongoza taifa hili.
 
Sawa sawa. Tumeambiwa hapa 30T zingejenga barabara za lami mpk basi zile 60T zingejenga angalau barabara za kuunganisha wilaya
Tumeanbiwa 30T zingejenga masarasa kila kijiji/mtaa, basi zile 60T angalau zingesaidia watoto wetu wote waende sekondari kwa mpigo kama ilivyo sasa tofauti na zamani watoto walienda shule kwa awamu, shule hazikuwa na madawati, uhaba wa walimu, majengo machakavu, ss zile 60T ndo ziliisha kwenye vitu ulivyovutaja tu.
Tumeambiwa hapa 30T zingemaliza shida ya maji nchi nzima, basi zile 60T zingepaleka maji angalau kila kata tu mbona bado shida ya maji ipo na 60T iliisha?
 
Unachotetea unatakiwa ukihalalishe. Kwamba trillion 30 kwa miaka 4 tu ni sawa na trillion 60 kwa miaka 59. Hujui mambo yaliyofanyika kwa miaka 59 tangu Uhuru ?. Ni lundo kuanzia viwanda, huduma za jamii, ajira, ukombozi wa kusini mwa Africa, elimu, taasisi za umma, ndege, reli 2 za Tazara na Dar Mwanza nk. Bado tunahoji hiyo trillion 30 ya mabwege Watanganyika mliyopora ndani ya miaka 4 mmeifanyia nini ?
 
Bado hamjasema kwa nini zile 60T hazikumaliza shida za WaTz kwa miaka zaidi ya 60 halafu mtake 30T zimalize matatizo yaliyoshindikana kwa 60T!
Hakuna cha kutetea hapa.
Rejea bandiko la mleta mada.
Anasema 30T zingetosha kujenga shule 278 kwa kila kata! Kwa nini basi 60T hazikujenga japo shule moja tu kwa kila kata?
Anasema 30T zingetosha kujenga vituo vya Afya 32 kila kata! Kwa nini basi 60T haukujenga japo kituo kimoja tu kwa kila kata?
Anasema 30T zingetosha kujenga barabara za lami 66,000km! Kwa nini 60T haikujenga japo 30,000km tu!?
 
Unajua tangu Uhuru Nyerere alijenga viwanda vingapi na kwa Tsh ngapi ? Unajua kwamba Nyerere alitibu watu wote bure ? Unajua alisomesha watu wote bure ? Unajua Nyerere alikomboa nchi zaidi ya 5 kusini mwa jangwa la Sahara ? Mwinyi alifanya sehemu, Mkapa sehemu na Kikwete alijenga Udom, barabara na kusomesha kila mwanachuo university kwa bodi ya mikopo. Magufuli alijenga SGR na Bwawa la umeme na flyover nk. Nimekuambia kwa uchache utitiri wa miradi ya miaka 59. Unakwama wapi kutueleza trillion 30 mlizotuibia zimefanya nini ndani ya miaka minne tu.
 
Q
Nisahihi
 
Ok, 30T zote zimepigwa na wajanja.
Lakini Kwa miaka 59 sh. 60T ndo zilifanya hayo tu!
Sasa mbona mnataka 30T ziwe zimejenga shule 278 kwa kila kata wakati 60T ilituachia shule zisizozidi 5 tu kwa kila Mkoa.
Unataka kila kata iwe na vituo vya Afya 32 wakati 60T iliacha wastani wa kituo cha Afya kimoja tu kwa mkoa mzima.
Mnataka 30T iwe imejenga 66,000km za lami wakati 60T hazikuweza kuunganisha baadhi ya mikoa!
 
Halafu kwa kufanya hivyo bado ungekuwa na SGR ikuyokamilika hadi Dodoma? Plus lot ya Makutopora - Tabora?

Je ungekuwa umeshwasha Bwawa la Nyerere ?

Hizi nyuzi zingine zinakuwa kama zimeandikwa na kuku wasio na vichwa
 
Toa mfano wa nchi iliyoanguka kwa sababu ya madeni
 
Angalia na population ya miaka hiyo, hakuna awamu ambayo haikujenga miundombinu ya huduma za kijamii.
 
Angalia na population ya miaka hiyo, hakuna awamu ambayo haikujenga miundombinu ya huduma za kijamii.
Miaka hiyo tulikuwa wachache sana lakini still hatukupata fuesa ya kwenda secondary.
Hakukuwa na barabara za lami kuunganisha mikoa pamoja na uchache wetu.
 
Development is a Process
 
Halafu kwa kufanya hivyo bado ungekuwa na SGR ikuyokamilika hadi Dodoma? Plus lot ya Makutopora - Tabora?

Je ungekuwa umeshwasha Bwawa la Nyerere ?

Hizi nyuzi zingine zinakuwa kama zimeandikwa na kuku wasio na vichwa
Akili yako iko timamu kweli? Hiyo miradi ilishafika stage ya kukamilisha, Hivi 30 Trilions unazijua kweli?
 
Hebu Sasa wewe tupe ufafanuzi wa hayo matumizi ya 30T.

Au wewe si Mtanganyika hayakuhusu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…