Je ! wajua nani alianzisha Mwenge ?

Je ! wajua nani alianzisha Mwenge ?

matitu

Senior Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
119
Reaction score
23
JE, WAJUA NANI ALIANZISHA

MWENGE?

MJUE FARAJA GANZE,
MCHAWI
WANZILISHI WA MWENGE WA

UHURU (Huu Tuuonao Hadi LEO)!

"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau

"Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl.Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru. Kinachonishangaza hapa ni kile kipengele kisemacho"UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU"..... Inamaana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa? Na kwann Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge?

Huyu Forojo Ganze,alikuwa ni mmoja kati ya wazee waliotumwa kufanya zindiko la nchi baada ya uhuru kule bagamoyo, walipewa kazi ya kuhakikisha rais aliye madarakani hapingwi na mtu yeyote(Mwl.Nyerere), zindiko hilo lilifanyika bagamoyo ktk moja ya mashimo yanayopatikana wilayani hapo,zoezi hilo lilienda sambamba na kumuuliza shetani na malaika zake ni jambo gani lifanyike ili Tanzania iendelee.

Forojo Ganze ndiye mtu pekee aliyeingia ktk hilo shimo kwaajili ya kuuliza, alikaa huko kwa muda wa siku 10 huku akiwa amewaacha wenzake nje wakimgoja atakuja na jibu gani ili wakampatie rais na wazee wa Dar es salaam, kilichoshangaza siku ya kumi na moja alitoka akiwa hoi hajiwezi akiwa kama mtu aliyepigwa na alikuwa anaongea lugha isiyofahamika,

wenzake wakiwa wanaongozwa na Yahaya Hussien walimbeba hadi ikulu Dar es salaam na walipomfikisha mbele ya mwalimu Nyerere alitamka maneno hayo yanayohusu mwenge kwa kiswahili kisha akanyoosha juu mkono wake wa kulia ambao tayari ulikuwa umeandikwa namba hii 115, kisha akakata roho.

-Baada ya mazishi mwalimu aliyafanyia kazi maneno ya Forojo Ganze akaanzisha mwenge wa uhuru bila kujua ulikuwa na maana gani, baada ya hapo aliwagiza yahya Hussein atafasiri maana ya ile namba 115, kama kawaida ya shehe Yahaya alitafasiri akamwambia kuwa namba hiyo inamaanisha "utakufa ukiwa na umri wa miaka 77 na taifa la Tanzania kwa kipindi hicho litakuwa na umri wa miaka 38.

Hii inamanisha ukichukua 77 umri wa mwalimu jumlisha 38 umri wa taifa utapata 115, na hii ndivyo ilivyokuwa, mwaka 1999 mwalimu alikufa akiwa na miaka 77 na taifa lilikuwa na miaka 38 ya uhuru (77+38=115) pia utamaduni wa rais kuongea na wazee wa Dar es salaam unaendelea hadi sasa na wamekuwa na maamuzi ya kitaifa na husikilizwa sana wanachokisema,mbona haijawahi kutokea rais akaongea na wazee wa bukoba jambo la kitaifa?,zindiko la bagamoyo linafanya kazi.-

Safu hii ilikuwa ya watu 5 ambao ni.

1. mzee ramadhan,alizaliwa mwaka 1920

2. Ally tarazo(1929),

3.Komwe wa Komwe(1918)

4.Sheihe Yahya Hussein(1925),na

5.Forojo Ganze (1902),

NB: Sina uhakika na taarifa hii kama ina ukweli wa 100%,mwenye uelewa Wa ukweli wa habari hii.
 
Ukakae kwenye shimo siku 10, hakuna chakula wala hewa safi. Hujaongea na mtu wala kuona mwanga na sura za watu! Ukitoka huko ubongo umeathirika, una psychosocial impairment na lazma ufe. Kifo chake is purely scientific.

Nyerere akichukua nchi hii alikuwa hana pa kuanzia. Kwa hiyo popote alipopata pale tufa a kwa ajili ya kupata support. Ukiangalia kwa wakati ule mwenge ulisaidia kutambua matatizo ya wananchi na kuwafikia pia. Ulisaidia kugundua wapi hakuna barabara na hospitali au maji.

Upuuzi ni kuendelea kutumia fedha kukimbia mwenge Badala ya kusukuma viongozi wahusika kutatua shida za wananchi. Haina tofauti na kumlipa mganga anaekaa kwenye kibanda cha nyasi ili akupe maarifa ya kujenga ghorofa.

Nimefurahia hizo hesabu za sheikh yahya hahaha. Alianza kuotea kitambo! Kama tb Joshua vile haha
 
Very interesting, ndio maana viongozi wa dini wengi wanaipiga sana vita hii kitu ya mwenge...

Ngoja nichimbue vyanzo vyangu nitarudi
 
hizi mbio za mwenge Wa uhuru ziliasisisiwa lini? mwenye kufahamu naomba msaada hapo
 
Na mataifa mengine yanayotumia mwenge(kabla yetu sisi) nao walizama kwenye mapango na kutoka na hilo wazo la kishetani?

Huyo alikopi tu utamaduni wa sehem zingine kama mwenge wa olimpiki, jumuia ya madola E.t.c

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Kumekuwepo na hadithi nyingi Sana juu ya mwenge baadhi zikidai kwamba ni utamaduni uliokuwa ukitumiwa na wazanaki Enzi hizo kwamba uliangaza himaya yote iliyokuwa chini ya chief wa kabila hilo.

Anyways,haka ka-article kanatafakarisha pia.
 
JE, WAJUA NANI ALIANZISHA

MWENGE?

MJUE FARAJA GANZE,
MCHAWI
WANZILISHI WA MWENGE WA

UHURU (Huu Tuuonao Hadi LEO)!

"Baba, sisi tunataka kuwasha mwenge na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro, umulike hata nje ya mipaka yetu, ulete tumaini mahala pasipo na tumaini, faraja palipo na huzuni, tumaini pasipo na tumaini, upendo penye chuki na heshima palipo na dharau

"Baada ya kutamka hayo mbele ya Mwl.Nyerere, Ganze alikata roho na ndipo ukaanzishwa Mwenge wa Uhuru. Kinachonishangaza hapa ni kile kipengele kisemacho"UMULIKE NJE YA MIPAKA YETU"..... Inamaana ndani ya nchi tubaki gizani kama tulivyo sasa? Na kwann Forojo Ganze hakutangazwa kama mwanzilishi wa Mwenge?

Umulike hata nje ya mipaka yetu ili ulete tumaini.

Hapo wanasema hivyo sio kama ulivyoandika hivyo sentensi hiyo ina maana ni ndani na nje.
 
Na mataifa mengine yanayotumia mwenge(kabla yetu sisi) nao walizama kwenye mapango na kutoka na hilo wazo la kishetani?

Huyo alikopi tu utamaduni wa sehem zingine kama mwenge wa olimpiki, jumuia ya madola E.t.c

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums

Ila miongon mwa symbol na tawala za giza ,mwenge upo
 
Ila miongon mwa symbol na tawala za giza ,mwenge upo

Mambo mengi ya hizo falme na tawala za giza ni za kufikirika sana! Hakuna mtu alie extract to the skeleton kuleta ushahidi wa dhahiri! Kwenye huo ulimwengu watu wanakwenda kwa assumption tuu

Yani hakuna ushahidi wa moja kwa moja na ndio loop hole hiyo watu wanaitumia na kila mtu kuibuka na lake! Nani wakuyapinga wakat hizo falme haziko real?

So huamin huwepo wake!?
 
Naamini kuwa,MWENGE WA UHURU NI SANAMU.
Na kukimbizwa kwa mwenge ni ibada ya sanamu ya miungu kwa kuzingatia mashartie !
 
Mzee mmoja alinadithia kua mwenge ulianza kutumika baada ya zindiko la nyerere kuzikwa kwa muda kwenye kaburi
 
So huamin huwepo wake!?

Kuamini kunatokana na nini ndugu? Kuona/kusikia/kugusa au kushika!

Imani ya kitu inakuwa valid unapo ona na ukaweza ku prove uwepo wa unachokiamini! Siamini nachosimuliwa kama binafsi siwezi kukithibitisha!

Nadhani nimekujibu hapo tayari.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Kuamini kunatokana na nini ndugu? Kuona/kusikia/kugusa au kushika!

Imani ya kitu inakuwa valid unapo ona na ukaweza ku prove uwepo wa unachokiamini! Siamini nachosimuliwa kama binafsi siwezi kukithibitisha!

Nadhani nimekujibu hapo tayari.

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums

Oouh, ina maan wew si muumin wa dini yeyote?
 
Umeileta huku! C ilikuwa kule jukwaa la historia? Ila huku ndio tutaona mwanga. Mzee Kichuguu uko wapi?
 
Last edited by a moderator:
Oouh, ina maan wew si muumin wa dini yeyote?

Dini ni utaratibu/mfumo uliowekwa na binadamu kutengeneza mwenendo bora wa maisha ya binadamu kifamilia,kiuchumi,kisiasa na mchangamano wa watu wote kwa ujumla!

Misingi ya heshima na nidhamu kwa kila mmoja! Uwe ndani ya dini au uwe nje ya dini cha msingi ni kuwa na utu,kujithamini na kuthamini wengine!

Kwangu dini kuu na kubwa ni Upendo!

Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
Back
Top Bottom