Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Qatar nchi yenye km za mraba 11,000 na watu wapatao milioni 3 imeandaa Kombe la Dunia lililotumia gharama zaidi tangu Dunia iumbwe.
Zaidi ya dola bilioni 220 zimetumika kwenye maandalizi mpaka kufanikisha Kombe la Dunia huku mapato ya kiuchumi yakitarajiwa dola bilioni 7.5 pekee mpaka kuisha kwake. Vimejengwa mpaka viwanja na makazi yatakayobomolewa baada ya mashindano. Pato la Tanzania ni $ Bilioni 62 kwa mwaka.
Nini Tanzania inaweza kufanya na $ bilioni 220;
Zaidi ya dola bilioni 220 zimetumika kwenye maandalizi mpaka kufanikisha Kombe la Dunia huku mapato ya kiuchumi yakitarajiwa dola bilioni 7.5 pekee mpaka kuisha kwake. Vimejengwa mpaka viwanja na makazi yatakayobomolewa baada ya mashindano. Pato la Tanzania ni $ Bilioni 62 kwa mwaka.
Nini Tanzania inaweza kufanya na $ bilioni 220;
- Ingejenga bandari ya Bagamoyo($ Bil 10) na kuepuka kuingizwa mjini na Mchina.
- LNG plant($ Bil 30) na kutumia gesi kila sehemu kuondokana na utumwa wa kulipa mafuta nje.
- SGR($ Bil 14) tungeifikisha Mwanza na Kigoma, kwa jeuri tugemjengea na Congo, akitoa mzigo wake Bagamoyo kituo cha kwanza Lubumbashi.
- Deni la Taifa($ Bil 28) tungelipa lote na bungeni tufocus kwenye kuongelea maendeleo maana mjadala wa deni la taifa huwa unapoteza muda wakati tunaendelea kukopa.
- Madarasa($ Bil 2), tungeacha kwenda kumpigia goti Mzungu eti kujenga vyumba vya madarasa.
- BRT($ Bil 2), tungejenga mwendokasi Dar nzima na kuwaonjesha Mwanza ikiwa na mabasi ya kutosha kama yale mekundu ya waingereza na kuachana na haya ya bluu tena 'Level seat' yakiendeshwa na gesi ya bei nafuu.
- Ile 'smelter' aliyokuwa anaiota Magufuli kila akilala, tungejenga japo bei yake siijui tungemudu 😉. Tungeachana na kugombana kuhusu mchanga na makinikia, tungeuza madini yaliyokamilika.
- Gridi ya taifa ya mfumo wa maji safi maana ukame mdogo tu vilio kila kona.
- Tungemaliza tantalila zisizoisha kuhusu chanzo cha umeme nchini.
- Inabakia kama nusu, $ Bil 20 tungewapa kabisa mafisadi wagawane wasituharibie miradi yetu.
- $ Bil 5 tungewaita Mo, Bakhresa, Rostam na watoto wa Mengi wawekeze zaidi walichowekeza sasa na waajiri kina siye maana hizo pesa zinazidi walichonacho. Serikali wakifanya wao, miaka 5 mingi kila kitu juu ya mawe.
- Zilizobaki tunaziweka kwenye akauti tukisubiri mambo yaende mrama kama Tanzania tulivyozoea.