JamiiCheck
JF-Expert Member
- Nov 3, 2023
- 245
- 267
Ni ipi rangi ya ulimi wenye afya?
Machapisho ya kisayansi na tafiti zinabainisha kuwa rangi ya ulimi wenye afya inapaswa kuwa ya ‘Pink’. Ulimi wenye afya pia huwa na vipele vidogo vinavyoitwa papila kwenye uso wake wote. Papila hizi husaidia katika kuzungumza, kuhisi ladha, kutafuna na kumeza chakula.
Rangi tofauti na ‘Pink’ yaani nyeusi, njano, chungwa, kijivu, nyeupe, zambarau, buluu ni ishara kuwa ulimi wako haupo sawa na hivyo unaweza kumuona mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi.
Sababu zinazoweza kupelekea ulimi kubadilika rangi
Ulimi kuwa mweupe (Madoa au tabaka jeupe) mara nyingi inaweza kuwa ni mkusanyiko wa bakteria ambao unaweza kuondolewa kwa kusafisha vizuri ulimi wako.
Hata hivyo, wakati mwingine madoa meupe kwenye ulimi yanaweza kuhusishwa na hali nyingine za kiafya, kama vile:
Ulimi mwekundu sana. Ikiwa ulimi wako unaonekana laini na mwekundu sana, inaweza kuwa ishara ya upungufu wa virutubisho mwilini, kama vile madini ya chuma (iron) au vitamini B12.
Kwa watu wazima, madoa au mabaka mekundu kwenye ulimi yanaweza kuwa si hatari. Hata hivyo, wakati mwingine yanaweza kuashiria hali inayoitwa erythroplakia, ambayo ni nadra lakini inaweza kuwa dalili ya awali ya saratani ya mdomo.
Kwa watoto, ulimi wenye rangi nyekundu kama stroberi (sitroberi) unaweza kuwa dalili ya homa nyekundu (Scarlet fever), ama Kawasaki.

- Fangasi wa mdomoni (Oral Thrush): Huu ni maambukizi ya fangasi yanayotokea mara nyingi kwa watoto wachanga au watu wazima wanaotumia meno bandia. Husababisha tabaka jeupe lenye mwonekano wa krimu. Kwa kawaida si hatari na linaweza kutibiwa na daktari au mfamasia.
- Lichen Planus: Hii ni hali ya uchochezi inayoweza kusababisha madoa meupe yenye muundo kama wa wavu ndani ya mdomo. Inapaswa kuchunguzwa na daktari wa meno ambaye anaweza kushauri hatua zinazofuata.
- Leukoplakia: Haya ni madoa meupe mazito ambayo hayaondoki unapoyafuta. Mara nyingi si hatari, lakini wakati mwingine yanaweza kuendelea na kuwa saratani ya mdomo. Ni muhimu kumuona daktari ikiwa madoa hayo hayapotei ndani ya kipindi cha wiki tatu.
Ulimi mwekundu sana. Ikiwa ulimi wako unaonekana laini na mwekundu sana, inaweza kuwa ishara ya upungufu wa virutubisho mwilini, kama vile madini ya chuma (iron) au vitamini B12.
Kwa watu wazima, madoa au mabaka mekundu kwenye ulimi yanaweza kuwa si hatari. Hata hivyo, wakati mwingine yanaweza kuashiria hali inayoitwa erythroplakia, ambayo ni nadra lakini inaweza kuwa dalili ya awali ya saratani ya mdomo.
Kwa watoto, ulimi wenye rangi nyekundu kama stroberi (sitroberi) unaweza kuwa dalili ya homa nyekundu (Scarlet fever), ama Kawasaki.
Chanzo: Clevercland clinic