Je, wajua? - Special Thread

Je wajua marais watatu wa hivi karibuni akiwemo huyu wa sasa wa nchi ya Ghana wanaitwa John,ni kama ifuatavyo 2001-2009 John Kofi Kufuor,2009-2012 John Evans Atta Mills,2012 hadi sasa John Dramani Mahama. Nadhani itafikia hatua kila mwanasiasa wa Ghana atajiita John
 
John einar selander ni mmoja wa viongozi wa iliyokuwa serikali ya tanganyika miaka ya 1920 ambapo akiwa mkurugenzi wa ujenzi (public works) aliwezesha ujenzi wa daraja la salenda ambalo baadaye 1929 wakati wa uzinduzi wake lilipewa jina lake

ingawa yeye alifariki 1927 iliwekwa kumbukumbu ya jina lake kwa kuasisi mradi huo ambao kwa wakati huo ulilenga kuunganisha barabara ambayo kwa sehemu kubwa yalikuwa makazi ya wazungu waliokuwa viongozi wa tanganyika kipindi hicho

daraja hilo linalounganisha mto msimbazi na bahari ya hindi kupitia barabara ya ally hasan mwinyi (kwa sasa) lilikuwa muhimu kwa viongozi waliokuwa wakiishi maeneo ya osterbay na maeneo mengine ya mji wa dar es salaam ya sasa

mwaka 1980 serikali ya japan kupitia shirika lake la maendeleo ilitoa fedha za ujenzi na marekebisho ya daraja hilo ambayo yalilifanya kuwa moja ya miradi yake ya kwanza tangu kuanza ushirikiano na japan hasa katika eneo la miundombinu hapa nchini.

Daraja hilo lina urefu wa mita 85 sawa na futi 279 lina uwezo wa kupitisha magari manne (4 lanes -dual carriage kwa wakati
 
shukran mkuu, nilikuwa najiuliza miaka mingi , hili daraja kwa nn linaitwa jina tofauti, tushazoea, mkapa bridge, wami, ruvu, temi.
 
Je wajua, watu wote dunian hawapendi kuumwa jipu kwenye njia ya haja kubwa. Yaani kwenye mazingira ya kinye....h00!!!
 
je wajua watu wengi(sio wote) majina waliosave kwenye simu zao mengi yanaanzia herufi M ??
 
Je, wajua kwamba binadamu pamoja na akili zake zote, pamoja na mbwembwe zake nyingi, bado hana uwezo wa kufikisha ulimi kwenye kiwiko cha mkono wake?
 
Elimu nzuri hiyo.

Je wajua ya ubongo umegawanyika kulia na kushoto ambapo upande wake wa kulia hudhibiti upande wa kushoto wa mwili na ule wa kushoto hudhibiti upande wa kulia wa mwili.
Upo sahihi mkuu hata jana nilimsikia Dr Twalib Ngoma akiongea hiyo kitu kupitia sauti ya amerika(voa)
 
hiyo ya ushuzi imeniacha hoi,kipimo cha hewa ni tofauti na kipimo cha kimiminika
Mkuu usistuke! Mbona huulizi gesi tunazotumia maju,bani kupikia zinapimwa kwa kilogramu. Hapo anamaanisha ushuzi huo unaweza kujaza chupa ya nusu lita.
 
Binadamu wengi hawajui ya kwamba kinywaji cha fanta kinachotengenezwa na kampuni ya Marekani ya Coca Cola kiligunduliwa na Manazi chini ya Uongozi wa Adolfu Hitler! Hivyo kesho ukinywa Fanta ujue unakubali mchango wa manazi na Adolfu Hitler kwenya kustaarabisha Dunia!
 
Ndio tunaukubali unazi na mchango wa hitler. Km hujui hitler ndo ka7bisha hadi leo hii germany ni superpower.
 
Na tunaokunywa Viroba tunakubali mchango wa nani?
 

Hata Volkswagen ilikuwa special kwaajili ya vita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…