Je, wajua? - Special Thread

No 9 we acha tu !! Hata hao wanaonawa wanaotumia sabuni ni asilimia inayochungulia sifuri . Hata ukitumia sabuni wenye makucha marefu sabuni inapenya ?
 
je wajuwa JF ina member zaidi ya laki 5???

Je wajuwa jamii Jf ni mtandao pekee ambao huwezi kubadili jina lako,kufuta uzi uliotuma bila msaada wa mods??
NSHAJUA MKUU AHSANTE KWA KUNIJUZA /KUTUJUZA
 
Bar nzuri na nyama choma ya uhakika . Umeagiza pande lako unasubiri ikatwe vipande mara akachomoka mtu kutoka maliwatoni na kuikata na hana dalili ya kunawa mikono , utaipokeaje ? Nafuu umeona , wanaokaa mbali na kuagiza wanajua usafi wake ? Wanaume vipi ?
 
Tz siyo nchi ya amani
 
UNAJUA KUWA___

1.'Made in China' stickers hutengenezwa Korea?

2.Asilimia 10 ya watu duniani hutumia mkono wa kushoto?

3.Asilimia 75 ya wanawake huuliza maswali ambayo tayari wanajua majibu yake?- hivyo ni bora umwambie ukweli

4.Asilimia 91 ya watu sio tena rafiki na watu ambao waliwaita ni 'rafiki kipenzi'?

5.Google map hucalculate traffic kwa kutrack ni kwa kasi gani android devices zinamove barabarani?

6.Wakati ukitafuta ticket ya ndege online, nauli ya ndege hupanda pale unapotembelea site mara nyingi zaidi?- hivyo futa internet cookie kabla ya kununua ticket ya ndege

7.Mwandiko mbovu wa daktari huhusika na taklibani vifo 7000 vya watu dunia nzima kila mwaka?

8.Wino wa kuchapishia ni ghali zaidi kuliko damu?

9.Kama ilivyo kwa 'fingerprint', kila mtu pia ana 'tongue print' tofauti?

10.Gesi halisia haina harufu ila harufu huongezwa artificially kwa sababu za kiusalama?

11.Shakespeare ndie alietunga maneno 'assassination' na 'bump' ?

12. Unasahau asilimia 80 ya kile unachojifunza kila siku?

13.Kuna matetemeko ya ardhi zaidi ya 50000 duniani kila mwaka?

14.Jimboni Michigan mwanamke haruhusiwi kukata nywele zake bila ruhusa ya mumewe?

15.Kuna mbwa wengi zaidi jijini Paris kuliko watoto?

16.Jijini Athens Ugiriki leseni ya udereva huwezwa kutwaliwa kisheria endapo dereva atagunduliwa kuwa hajaoga au amevalia vibaya?

17.Jimboni Massachusetts ni haramu kwenda kulala pasipo kuoga?

18.Kitabu cha record cha Guinness kinashikilia record ya kuwa kitabu kilichoibiwa zaidi kutoka katika maktaba za umma?

19.Jina kamili la jiji la Los Angeles ni "El Pueblo de Nuestra Senora la Reina de los Angeles de Porciuncula"?

20.Antarctica ina ATM machine moja tu?

21.Hakuna ice zozote zilizoifunika Iceland?

22.Mwanamke wa kawaida hutumia mwaka 1 wa maisha yake yote akijaribu kuamua ni nini avae?

23.Mwanamke wa kawaida hubugia zaidi ya kg 2.7 za lipstick katika maisha yake yote?

24.Mnyama pekee wa kufugwa ambae hakutajwa kwenye biblia ni paka?

25.Viatu vyako ni kitu cha kwanza kabisa ambacho mtu hugundua kuhusu wewe?- viatu vyako ni muhimu kuliko unavyofikiri, watu hutoa mahitimisho mbalimbali kuhusu wewe kutokana na viatu ulivyovaa.

26.Unachangia siku yako ya kuzaliwa na angalau watu wengine million 9 duniani?

27.Unapokumbuka tukio lililopita kikawaida unakumbuka mara ya mwisho ulipolikumbuka na sio siku ya tukio lenyewe?

28.Emirates Palace, Abu dhabu kuna ATM machine ambayo hutoa miche ya dhahabu na sio pesa?

29.Gari za police Dubai hujumuisha Lamborghini, Ferrari na Bentley? - kulingana na wao magari ya gharama na ya haraka huwasaidia kukamata wahalifu

30. Expiration date katika chupa ya maji ni kwa ajili ya chupa na sio maji?

31.Ubongo wa binadamu aliesinzia bado unauwezo wa kuelewa maneno yanayosemwa karibu yake?

32.Angalau kwa kila siku moja mfumo wako wa kinga wa mwili huharibu seli moja ambayo ingeishi ingetengeneza kansa?

33.Asilimia 95 ya watu wamedondosha simu zao usoni kwao wakati wakichati huku wamelala?

34.Kobe hazina meno?

35.Kuskia jina lako likiitwa ilihali Hakuna aliekuita ni ishara ya akili yenye afya?

36.Kuna sekunde 31,557,600 katika mwaka?

37.Binadamu hutumia taklibani miaka 25 ya maisha yao wakiwa wamelala?

38. Umwambiapo rafiki yako siri pia huwaambia watu wake wa muhimu hata kama utamwambia asimwambie yeyote yule?

39.India ina zaidi ya Nyani 50?

40. 111,111,111 × 111,111,111 =12,345,678,987,654,321

41.Ndizi ni tunda la furaha na hivyo kula Ndizi huondoa hisia mbaya, msongo wa mawazo na hasira?

42.Watu wenye uwezo mkubwa wa akili hufikiri kwa haraka na kufanya mwandiko wao uwe mbaya?

43.Watu hukuona ni mwenye mvuto kwa asilimia 20 zaidi ya unavyojiona wewe?

44.Watu ambao huuma kucha zao huwa na kinga imara zaidi ya mwili?

45.Watu ambao hutumia simu zao wakati wakidrive husababisha foleni kwenda pole pole zaidi kwa asilimia 10.

46.Watu ambao huzungumza peke yao wanauwezekano wa kuwa na IQ kubwa zaidi?

47.Kucheza video games husaidia kupunguza kuota ndoto mbaya na huboresha uwezo wa kufanya maamuzi kwa asilimia 25 na huboresha umakini na ubunifu?

48.Watu wanaotumia mkono wa kulia kwa wastani huishi miaka 9 mbele zaidi ya watu wanaotumia mkono wa kushoto?

49.Kulala kazini inakubalika nchini Japan? Inachukuliwa kama uchovu kutokana na kufanya kazi kwa bidii

50.Tembo ni mnyama pekee ambae hawezi kuruka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…