Je, wajua? - Special Thread

Kwa sababu haujawai kuuona ndo maana unasema hana
NAOMBA TUJIFUNZE KUHUSU MAMBA

MAMBA anapatikana katika order ya crocodilia familia ya crocodilidae, Duniani kuna aina 23 za mamba, lakini kwa hapa afrika zipo aina tatu tu! Ambazo ni:
1.NILE CROCODILE

2.SLENDER SNOUTED CROCODILE

3.DWARF CROCODILE

neno "crocodile" limetokana na neno la kigiriki linalo maanisha "mjusi" , lakin ki uhalisia mamba hafanani na mijusi, ana fanana na ndege vitu vingi.

NILE CROCODILE ndio mkubwa kwenye hii familia na anaweza kufikisha uzito wa kilo 500 ad 1000

Sasa tuangilie sifa za Mamba kwa ujumla
- Ni wanyama wasio na ulimi

-Meno yao hayana mpangilio sahihi

-wana taga mayai

-Uzito wa mkia unachukua asilimia 40 ya uzito wake

-Macho na pua zimekaa kwa juu ya kichwa

-Miguu ya nyuma ni "webbed" hivyo huwasaidia kuogelea, (webbed feet ni kama miguu ya bata nimeshindwa kujua kwa kiswahili tunaitaje)

-Wana "gular sac" hii ni organ ambay inamsaidia wakat anameza chakula, au amepanua mdomo kwenye maji, maji hayawezi kupita kwenye koromeo

Kumekuwa na imani tofauti kuhusu mamba, Baadhi ya waindi na jamii za kiislam wana mpa heshima sana mamba wakiamini kuwa kuna baadhi ya verses kwenye QURAN, zimeandikwa kwenye kichwa cha mamba, Miaka ya nyuma walionekana mamba wengi sana kule nchini misri, hivyo watu wa misri waliamini kiumbe huyu ni baraka na ameletwa na MWENYEZI MUNGU, hivyo walimpa jina la Nile Crocodile.

Mamba anapo taka kutaga anaenda sehemu salama ya nchi kavu, anachimba shimo lenye urefu wa kama futi moja, kisha anatagia mayai yake hapo ,akimaliza ana fukia hilo shimo anarudi kwenye maji. Jinsia ya mtoto itategemea na joto la yai, Hivyo joto likiwa nyuzi 26--30 atatoka mtoto wa kike, na likiwa 31--34 atatoka wa kiume, na mayai yanaweza kuwa zaidi ya hamsini. Kumbuka hapa mayai yanategemea joto la jua na mchanga ili vitoto vijitotoe! na itaweza kuchuka miezi 2 ad 4. Na kwa kipindi chote hichi mama atakua anakuja kwenye eneo hilo kukagua.
Siku vitoto vikijitotoa vitaanza kulia, Mamba akiwa kwenye maji atasikia sauti na ataenda kuwafukua na kwenda nao kwenye maji,

WANAPOPATIKANA
Nile crocodile anapatikana ukanda wote wa Tanzania, na Slender snouted anapatikana ukanda wa ziwa tanganyika tu! Hawa ndio mamba tulio nao tanzania

Wana uwezo kuishi adi miaka 75 hata 100, mwili wao umefunikwa na magamba kwaajili ya kuzuia kupoteza maji mwilini, na ni reptile pekee mwenye Seheme nne za moyo hapa nazungumzia zile chambers of heart,

Wanakuwa hatari zaidi wakiwa kwenye maji, muda mwingine huonekana nchi kavu wakiwa wamepanua midomo yao, hapa wanakuwa wana pooza miili yao, kama nilivyo sema mwanza magamba yao ni magumu sana hivyo hewa haipiti, pia wanafanya hivyo ili kuwaruhusu ndege waje kula mabaki ya nyama yalio baki kwenye meno,

Je ni kitu gani kingine unafahamu kuhusu MAMBA?

Picha zao hizi hapa huyu alie panua mdomo ni Nile crocodile na hao wengine kwenye maji pia, hawa wenye midomo membamba nd wanaitwa slender snouted.. Enjoy brian shirima

Sent using unknown device
 
Kwa sababu haujawai kuuona ndo maana unasema hana
Anakitu kinaitwa false tongue ila hana ulimi, yeye hukata Na kumeza Tu ndio maana sumu/nyingi yake inatajwa kua Kali Kwa kuweza kuchakata msosi..BTW ukiach kuuwwa mamba kinacho muua ni njaa kwakua akizidi kukua anakosa msosi wa kimshibisha!
 
Anakitu kinaitwa false tongue ila hana ulimi, yeye hukata Na kumeza Tu ndio maana sumu/nyingi yake inatajwa kua Kali Kwa kuweza kuchakata msosi..BTW ukiach kuuwwa mamba kinacho muua ni njaa kwakua akizidi kukua anakosa msosi wa kimshibisha!
Hana true wala false tongue..... Mamba hajawai kujua ladha ya chakula
 
Je wajua lady jaydee hajaenda msibani kwa Ruge baada ya kuzuiwa ngoma zake zisipigwe clouds?
 
*Je wajua?*

-Ikulu ya magogoni ilikuwa ni Msikiti na boarding(Zawiyah) ya waisilamu waliotoka nchi mbali mbali za Afrika Mashariki na kati (Tanganyika, Congo, Malawi, Mozambique, Uganda, Burundi, Rwanda) kuja kusoma na msikiti huo kama ulivyo hii leo uliyojengwa mwaka 1865 na pakaitwa *Dar Us Salaam* na katika lango kuu pameandikwa ayah ya 46 surat hijr isemayo

*Udkhulu-ha bi-salamin aminina*

-Je wajua kwamba majengo ya Ocean Road Cancer Hospital yalikuwa ni majengo ya msikiti na boarding ya vijana na wazee waliokuja kusoma Dar Us Salaam na bado muonekano wake ni ule ule

-Je wajua Kwamba St Joseph Cathedral ilikuwa ni jengo la msikiti na ni kanisa pekee ambalo lina Qubah na limeelekea Qibla

-Je wajua Kwamba pale mnara wa saa(Clock Tower) ilikuwa kuna msikiti na makaburi ya Masharifu na pale mnara wa saa kuna kaburi la Sharif Atwaas mpaka hii leo kaburi hilo lipo wajerumani walishindwa kuliondoa?

*MAJENGO HAYA YOTE YALITEKWA NA WAJERUMANI NA KUFANYWA MAJENGO YA SERIKALI NA PALE OCEAN ROAD KUFANYWA HOSPITALI NA MAJENGO HAYA HAYAKUJENGWA NA MJEREMANI*

Khutba ya Al-Marhum Sheikh Zubeir Ibn Yahya Ibn Mussa Al-Kasaju Al-Qadiriy (Rahimahullah)
 
Yote ayo ni mambo ya wakoloni..embu tuambie kabla ya Mwarabu yalikuwa mashamba ya akina nani? Je waliuziwa au walitwaa kwa nguvu na kupeleka babu zetu utumwani na kuwaasi
NB: Mzugu na Mwarabu si Mungu wala watumishi pekee wa Mungu wao walikuja kutafuta Maisha na kuambukiza tamaduni na dini zao..
 
Mashamba ya Bibi mwanangoko huyo mwanangoko amerithishwa na mzee kibode

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…