Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
NAOMBA TUJIFUNZE KUHUSU MAMBAKwa sababu haujawai kuuona ndo maana unasema hana
MAMBA anapatikana katika order ya crocodilia familia ya crocodilidae, Duniani kuna aina 23 za mamba, lakini kwa hapa afrika zipo aina tatu tu! Ambazo ni:
1.NILE CROCODILE
2.SLENDER SNOUTED CROCODILE
3.DWARF CROCODILE
neno "crocodile" limetokana na neno la kigiriki linalo maanisha "mjusi" , lakin ki uhalisia mamba hafanani na mijusi, ana fanana na ndege vitu vingi.
NILE CROCODILE ndio mkubwa kwenye hii familia na anaweza kufikisha uzito wa kilo 500 ad 1000
Sasa tuangilie sifa za Mamba kwa ujumla
- Ni wanyama wasio na ulimi
-Meno yao hayana mpangilio sahihi
-wana taga mayai
-Uzito wa mkia unachukua asilimia 40 ya uzito wake
-Macho na pua zimekaa kwa juu ya kichwa
-Miguu ya nyuma ni "webbed" hivyo huwasaidia kuogelea, (webbed feet ni kama miguu ya bata nimeshindwa kujua kwa kiswahili tunaitaje)
-Wana "gular sac" hii ni organ ambay inamsaidia wakat anameza chakula, au amepanua mdomo kwenye maji, maji hayawezi kupita kwenye koromeo
Kumekuwa na imani tofauti kuhusu mamba, Baadhi ya waindi na jamii za kiislam wana mpa heshima sana mamba wakiamini kuwa kuna baadhi ya verses kwenye QURAN, zimeandikwa kwenye kichwa cha mamba, Miaka ya nyuma walionekana mamba wengi sana kule nchini misri, hivyo watu wa misri waliamini kiumbe huyu ni baraka na ameletwa na MWENYEZI MUNGU, hivyo walimpa jina la Nile Crocodile.
Mamba anapo taka kutaga anaenda sehemu salama ya nchi kavu, anachimba shimo lenye urefu wa kama futi moja, kisha anatagia mayai yake hapo ,akimaliza ana fukia hilo shimo anarudi kwenye maji. Jinsia ya mtoto itategemea na joto la yai, Hivyo joto likiwa nyuzi 26--30 atatoka mtoto wa kike, na likiwa 31--34 atatoka wa kiume, na mayai yanaweza kuwa zaidi ya hamsini. Kumbuka hapa mayai yanategemea joto la jua na mchanga ili vitoto vijitotoe! na itaweza kuchuka miezi 2 ad 4. Na kwa kipindi chote hichi mama atakua anakuja kwenye eneo hilo kukagua.
Siku vitoto vikijitotoa vitaanza kulia, Mamba akiwa kwenye maji atasikia sauti na ataenda kuwafukua na kwenda nao kwenye maji,
WANAPOPATIKANA
Nile crocodile anapatikana ukanda wote wa Tanzania, na Slender snouted anapatikana ukanda wa ziwa tanganyika tu! Hawa ndio mamba tulio nao tanzania
Wana uwezo kuishi adi miaka 75 hata 100, mwili wao umefunikwa na magamba kwaajili ya kuzuia kupoteza maji mwilini, na ni reptile pekee mwenye Seheme nne za moyo hapa nazungumzia zile chambers of heart,
Wanakuwa hatari zaidi wakiwa kwenye maji, muda mwingine huonekana nchi kavu wakiwa wamepanua midomo yao, hapa wanakuwa wana pooza miili yao, kama nilivyo sema mwanza magamba yao ni magumu sana hivyo hewa haipiti, pia wanafanya hivyo ili kuwaruhusu ndege waje kula mabaki ya nyama yalio baki kwenye meno,
Je ni kitu gani kingine unafahamu kuhusu MAMBA?
Picha zao hizi hapa huyu alie panua mdomo ni Nile crocodile na hao wengine kwenye maji pia, hawa wenye midomo membamba nd wanaitwa slender snouted.. Enjoy brian shirima
Sent using unknown device