Je, wajua? - Special Thread

Je, wajua? - Special Thread

Je wajua cocacola ya kwanza kutengenezwa ilikua ya kijani. !
 
Je wajua kuwa neno refu zaidi la kiingereza lisilo na herufi hata moja inayojirudia ni UNCOPYRIGHTABLE
 
  • Thanks
Reactions: me1
Je wajua marais watatu wa hivi karibuni akiwemo huyu wa sasa wa nchi ya Ghana wanaitwa John,ni kama ifuatavyo 2001-2009 John Kofi Kufuor,2009-2012 John Evans Atta Mills,2012 hadi sasa John Dramani Mahama. Nadhani itafikia hatua kila mwanasiasa wa Ghana atajiita John

Majina yanayoanza na J wengi wao nyota zao ni za kuongoza. Angalia hapa kwetu,
JKN
JMK
JPM

Angalia pia
JOMO KENYATA
JOHN KENEDY
JOSE MUJICA
JOSEPH KABILA
JUMA KAPUYA
JOHN KOMBA
nk
 
Habari wana JF! Katika pita pita yangu nimekutana na mambo yafuatayo hapa chini nikaona ni vizuri tujuzane, kama kuna anayeweza kutuongezea, pia siyo mbaya: Je wajua;

1.Tar 4/4, 6/6, 8/8, 10/10 &12/12 zinaangukia siku moja kwa mwaka wowote?

2.Fisi hujifungua kupitia kisimi?

3.Mstari wa Equator hupitia nchi 13 ambazo ni: Ecuador,Colombia, Brazil, Sao Tome & Principe, Gabon, Republic of the Congo,Democratic Republic of the Congo, Uganda, Kenya, Somalia, Maldives, Indonesia na Kiribati.

4.Chuo kikuu cha Al ? Azhar kilichoko Cairo nchini Misri ndicho chuo kikuu cha zamani zaidi duniani, kilianzishwa mwaka 969 AD.

5.Pesa ya noti haikutengenezwa kwa karatasi bali kwa pamba?

6.Ulimi wa Kinyonga ni mrefu kuliko mwili wake?

7.Binadamu hutengeneza wastani wa nusu lita ya ushuzi kwa siku?


Mkuu hiyo namba 1 imenishangaza sana tu.

Huu uzi unafundisha sana.
 
Sema kutokea kwa ulimwengu maana ukisema kuumbwa kwa ulimwengu inamaanisha una-refer vitabu vya dini ambavyo kwa mujibu wake vinadai ulimwengu una miaka 6,000 tu

Labda useme kitabu "cha" dini na siyo "vya" dini, na utaje cha dini ipi ulichokisoma ukaona hayo.

Qur'an ambacho ni kitabu cha dini yangu kisicho shaka ndani yake, hakisemi hivyo.
 
Jee, wajua kuwa Muhammad Ali boxer maarufu kupita wote duniani. Kwenye nyota yake iliyopo Hollywood Walk of Fame, ndiyo pekee imetunddikwa ukutani na haikuwekwa chini kama za ma star wengine wote? Jionee kwanini:

 
Last edited by a moderator:
ju wajua uzito wa tembo unalingana au umepishana kidogo sana na uzito wa mnyama nyangumi?? wajua hilo??

No. Ulimi wa nyangumi ndio unalingana na tembo
 
Je, wajua kuwa zezeta wa Primary aweza kuwa bright wa secondari hadi chuo kikuu?
 
Je wajua kuwa magufuli amenirudisha ccm rasmi?
 
Je wajua kuwa tanzania kuna waspmi wengi wasioweza kuandika barua ya kikazi kwa lugha ya kiingereza??

Sio Tanzania pekee nina uhakika nchi nyingi ulimwenguni ambazo kiingereza sio lugha ya kwanza,zina wasomi wengi wasioweza kuandika,kusoma na kuongea kiingereza.Kama uamini nenda China
 
Back
Top Bottom