Je, wajua? - Special Thread

Je, wajua? - Special Thread

Rajiv Gandhi International Airport iliyopo Hyderabad India ndio ambayo inahuduma ya facial recognition na kuifanya kuwa ya kwanza kutoa huduma hiyo duniani kote.
 
Je wajua kuna kaburi la vifaa anga (spacecrafts cemetery)! Eneo hili linaitwa Point Nemo ambalo lina urefu wa mita 4,000 kusinini mwa bahari ya Pacific na lipo mbali kabisa na nchi kavu kwenye pande zote za dunia. Point Nemo imezungukwa na maji pande zote kwa ukubwa wa zaidi ya Kilometa 2,250.
Cha kushangaza zaidi aliegundua eneo hilo hajawahi kufika hapo! Ilikuwa mwaka 1992 ambapo Croatian survey engineer Hrvoje Lukatela alitumia program ya computer kutafuta ni point gani iliyo mbali zaidi kutoka point nyingine za nchi kavu. Maana halisi ya Nemo ni "no man"....eneo hili limezungukwa na mawimbi makali yanayozunguka muda wote na kufanya eneo hili lisikaliwe na viumbe wa baharini kama samaki... Kiufupi hakuna maisha.
sasa mkuu hao marehemu wanapelekwaje hapo!,
 
sasa mkuu hao marehemu wanapelekwaje hapo!,
Marehemu satelite wamefungiwa vifaa maalumu ambayo vitatoa ishara kwamba kimekufa na imeditelly kwa kutumia mafuta yaliyobaki vinaelekezwa eneo hilo... Kwa ambazo zipo mbali sana na uso wa dunia zinapotelea kwenye anga jingine.
 
Habari bandugu!
Hii thread ni kwa ajili ya kupeana/kupashana juu ya mambo tusiyoyajua ama pengine tunayajua lakini kuna wengine wanakuwa hawajui kabisa.

Comment kile ulichonacho ufahamu kwa ajili ya kuelimisha wengine pia.

Je, Wajua kutoka kwangu japo ni zingine ni copy & paste hizi hapa.

[emoji117]Idadi ya Kuku waliopo duniani inazidi idadi ya watu wote walio hai mpaka mda huu.

[emoji117] Kulala pembeni ya mtu unayempenda huondoa msongo wa mawazo, inaongeza muda wa kuishi na inakufanya upate usingizi kwa haraka.

[emoji117] Kwa mujibu wa Bill Gate, hadi kufikia mwaka 2035 hakutakuwa na nchi yenye umasikini wa kutupwa kama ilivyo sasa.


Je wajua ya kwako ni ipi..... dondosha hapo chini tuwafungue na wengine pia.
 
Yaani kwa thread hii tu unataka watu wakufuate twitter. Je ukiandika threads kama za akina gudume,hanga,pascal si utataka watu wakufuate chooni?
😲😲😲😲😲

Taifa la China lina wavutaji sigara takriban milioni 351 - hili lina maana kwamba wavutaji sigara wa China ni wengi kuliko binadamu wote waishio Afrika mashariki na ya kati.


Ps- naomba tafadhali nifuate kwenye ukurasa wangu wa twitter(@kelvin_ikaria)- Amplifaya
 
Taifa la China lina wavutaji sigara takriban milioni 351 - hili lina maana kwamba wavutaji sigara wa China ni wengi kuliko binadamu wote waishio Afrika mashariki na ya kati.
Kweli kabisa... wale wanaojenga flyover pale ubungo kila mchina ninayemuona anavuta sigaraa.
Sijui wana matatizo gani???!!!!
 
Mambo 50 ya kisaikolojia yatakayokuacha
kinywa wazi.

Hii ni kwel hata kama ulikua hujui kubali
tu, maana ndio ukweli uliopo.

1. Mtu hufanya ishara nyingi za mikono
akiwa anazungumza ukweli. Azungumzae
uongo mikono yake huwa imetulia zaidi.
2. Sikiliza kwa makini namna mtu
anavyozungumzia watu wengine akiwa na
wewe, na ndivyo atakavyokuzungumzia
wewe akiwa na watu wengine.
3. Ndoto zako zinabeba ujumbe mhimu
sana. Asilimia 70 ya ndoto zako zina
ujumbe wa siri.
4. Kwa kawaida watu huwa waaminifu na
wakweli mwili ukiwa umechoka, na ndio
sababu hutubu na kutoa siri zao kwenye
mazungumzo yatekeayo usiku wa
manane,
5. Ukihisi mtu au watu wanakuangalia,
angalia saa au muda kama unataka kujua
wakati, watu wanaokutazama nao
watatizama saa, hii ni kwa sababu
kuangalia wakati/mda huambukiza.
6. Kunywa maji ya baridi sana mapema
asubuhi husaidia mwili wako kufanya kazi
vizuri hadi asilimia 25.
7. Kukumbatiana huondoa shauku,
msongo wa mawazo na huongeza kinga ya
mwili.
8. Kushindwa kumtoa mtu akilini mwako
imamaanisha kwamba nawe upo akilini
mwa mtu huyo.
9. Watu wenya akili yenye ubunifu hupata
shida sana kupata usingizi, hivyo
hupendelea kuwa macho hadi usiku wa
manane.
10. Kama utakataliwa na mtu ambaye
kujali kwake ni muhimu sana kwako, basi
maumivu utakayopata katika ubongo
wako ni kama maumivu ya mwili
yanavyokuwa.
11. Mtu ambaye ametendwa au
ameumizwa kisaikolojia huwa na hulka ya
kukasirika pasipo sababu yeyote ya
msingi.
12. Ukitaka kujua kama mtu unaezumguza
nae anapenda kusikia unayoyazungumza
kunja mikono yako, kama anapenda na
anafurahia mazungumzo nae atakunja
mikono pia.
13. Kama mtu anachekacheka tu bila
sababu maalumu au anacheka sana, basi
mtu huyo ana huzuni kuu moyoni mwake,
na kama mtu analala kwa mda mrefu
sana, mtu huyo ni mpweke.
14. Namna tunavyozungumza na watoto
wetu ndivyo inavyokuwa sauti katika
mioyo yao.
15. Mtu akitokea katika ndoto unayoota,
basi ni kwa sababu mtu huyo kakuhamu
(kakumiss).
16. Wa kwanza kuomba msamaha
sikuzote ni mwerevu, wa kwanza
kusamehe ni mwenye nguvu na wa
kwanza kusahau ni mwenye furaha.
17. Mashairi katika wimbo uupendao ni
ujumbe ambao unapambana kuufikisha
mahala flani au kuwaambia watu flani.
18. Ukitumia mkono wako usiotumika
mara kwa mara (wa kushoto kwa wengi)
itakusaidia kuwa na ‘self control’.
19. Kama mwanaume atasimama akiwa
ametanua miguu yake wakati akizungumza
na mwanamke, ni ishara kwamba
mwanaume huyo anampenda mwanamke
kwa dhati.
20. Mwanaume akiwa hajisikii huru au
akiwa hana amani, basi hushika kichwa au
uso wakati mwanamke hushika aidha
nywele, hereni, mavazi, mikono au shingo.
21. Siku zote fuata wazo linalokuogopesha
zaidi, sababu hili ndili litakalo kujenga na
kukuimarisha.
22. Aina mbili ya watu ambao
hawatakuangalia machoni: mtu anaejaribu
kuficha uongo na mtu anaejaribu kuficha
mapenzi/ upendo.
23. Wanasaikolojia wanasema mtu
anataka kumfurahisha kila mtu huishia
kuwa mpweke zaidi.
24. Mtu anaekasirika kirahisi, kwa vitu vya
kijinga, inaonesha kwamba anahitaji
upendo/kupendwa.
25. Sikuzote wanaoponda au kulalamikia
wengine kwa wanayofanya, ndicho kile
wanachofanya wao au wanatamani
kufanya wao- elewa hili.
26. Kulia ni afya kwako. Huondoa bacteria
wabaya mwilini mwako, hukupunguzia
msongo wa mawazo na kukuongezea
kinga ya mwili.
27. Saikolojia inasema: Huogopi kupenda,
unachoogopa ni kutokupendwa (afraid of
not being loved back).
28. Ukweli wa mambo: uko karibu zaidi
na kufanikisha malengo yako kama
utayaweka kuwa yako pekee, yaani kuwa
ni siri yako.
29. Saikolojia inasema: kujifanya mwenye
furaha wakati una maumivu ni mfano wa
kuonesha ni jinsi gani wewe ni
mwanadamu mweye nguvu. (strong
person).
30. Kabla ya kulala, asilimia 90 ya akili
yako huanza kufikiri mambo ambayo
ungependa yatokee.
31. Watu wanaotembea kwa hatua za
harakaharaka huonekana kuwa
wanajiamini na wenye furaha zaidi kuliko
wanaotembea taratibu.
32. Watu wanaojua utani zaidi wanajua
kusoma akili za watu pia.
33. Ubongo wa mwanadamu alielala
unaweza kuelewa mazunguzo ya watu
walio karibu eneo hilo.
34. Ukiwa uaongea na mtu, ongea huku
ukitaja jina lake, hii itasaidia kupendwa
zaidi na mtu huyo.
35. Kufuatana na uchunguzi wa wataalam,
kumtamani mtu kingono hiushia miezi
minne, zaidi ya hapo utakuwa ni upendo
wa dhati.
36. Uchunguzi unaonesha kuwa watu
wanaolala na mito mingi ni wenye msongo
wa mawazo na wapweke.
37. Umbo la ubongo wako hubadilika kila
unapojifunza jambo jipya.
38. Watu wakiwa katika kundi na ikatokea
kuna kucheka, wale walio na mahusiano
ya karibu zaidi hutizamana.
39. Kwa namna mwandiko wa mtu
unavyokosa mpangilio au kuwa mbaya
ndio kiashirio kwamba mtu huyo anafikiri
haraka zaidi ya mikono yake inavyoweza
kuandika.
40. Kuna watu wana alama ya asili ya
kuwaamsha muda wanaotaka, hii ni kwa
sababu wana homoni ya asili ya stress.
41. Haiwezekani kukaa na hasira dhidi ya
umpendae kwa mda mrefu. Hasira
inayofika siku tatu au zaidi inamaanisha
kwamba hauna upendo.
42. Chakula cha kwenya ndege hakina
ladha sana sababu uwezo wetu wa
kutambua ladha hupungua kwa asilimia 20
hadi 50 tukiwa angani.
43. Kama urafiki utafikisha miaka saba,
basi urafiki huo utadumu milele.
44. Kama mtu akiongea na wewe halafu
kwenye maongezi akakungalia machoni
kwa asilimia 60 ya maongezi basi
umemboa mtu huyo. Kama atakuangalia
kwa asilimia 80 basi umemvutia mtu huyo
na kama itafikia asilimia 100 basi mtu
huyo anakutishia.
45. Katika sekunde tatu za mwanzo
unapoamka, huwezi kumbuka chochote.
46. Uoga waweza kuua. Hii ni kwa sababu
mwili huzalisha adrenalin ambayo ni sumu
ikizidi.
47. Kawaida, mtu akianza kulia
atakumbukaia matukio mengine
yaliyomsikitisha au kumchukiza ili
kuongezea ubongo wake hamu ya kulia.
48. Unapopiga chafya, unakufa kwa
sekunde.
49. Unapotekenywa hucheki,
bali ni itikio na kupaniki (panic response).
Huwezi jitekenya mwenyewe kwa sababu
mwili hauhisi hatari yoyote. Kawaida enzi
za zamani kutekenya ilitumika kama
adhabu.
50. Kukosa usingizi husababisha ubongo kutokumbuka mambo kiusahihi.

Koment hapo no ipi umeipenda .
 
Back
Top Bottom