Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Yes mtoto mbali na lishe pia anatakiwa kufanyiwa uchangamshi hii ni pamoja na kucheza nae na kuwasiliana nae. Utawasiliana na mtoto kwa kumuongelesha na pia kumgusa ama kwa kumshika-shika au hata kumbusu. Cheza naye, michezo ipo ya aina mbalimbali kutegemea na umri wa mtoto. Yaani tangu siku sifuri hadi miaka 5 cheza naye kwa sana na msisitizo mkubwa ni kwa kipindi hicho cha umri wa miaka miwili. Fahamu pia kwamba unaanza kucheza na mtoto angali akiwa tumboni. ^CSNa ndio maana akina mama wanatakiwa kula vizur wakati huu maana watoto wao wanapata chakula kupitia wao.