Je Wajua? Ubongo wa binadamu hukua kwa haraka kabla ya kuzaliwa!

Je Wajua? Ubongo wa binadamu hukua kwa haraka kabla ya kuzaliwa!

Sema Tanzania

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2016
Posts
251
Reaction score
466
Ubongo wa binadamu hukua kwa haraka kabla ya kuzaliwa na katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo wa maisha ya mtoto.

Katika kipindi hiki, takribani 75% ya kila mlo unaenda kujenga ubongo wa mtoto wako na akipata walau dakika 15 za kucheza itamsaidia kuimarisha umakini wa ubongo wake.

Hivyo elewa kwamba: Kila unapomkumbatia, unapombusu, kila mlo kamili unaompa, na kila wakati unapocheza naye, unasaidia kujenga ubongo wa mtoto wako!

#Malezi
 
Kweli aisei, niliwahi soma somewhere kuwa ndani ya miezi sita ya mwanzo mtoto anajenga uwezo wa kugundua jinsia ya mtu kwa hisia na kugusana, na katika kipindi hiki huambukizwa hisia za kupenda jinsia tofauti kutoka kwa mzazi wa jinsia ya kinyume chake.

Kwa mfano mama humuambukiza hisia za kupenda wanawake/mademu/wasichana (yaani hamu ya kupenda papuchi) mtoto wa kiume huku baba akimuambukiza mtoto wa kike kupenda wanaume/wavulana (yaani kupenda gegedeo) haya ndiyo maajabu ya Mungu.
 
Na ndio maana akina mama wanatakiwa kula vizur wakati huu maana watoto wao wanapata chakula kupitia wao.
 
Na ndio maana akina mama wanatakiwa kula vizur wakati huu maana watoto wao wanapata chakula kupitia wao.
Yes mtoto mbali na lishe pia anatakiwa kufanyiwa uchangamshi hii ni pamoja na kucheza nae na kuwasiliana nae. Utawasiliana na mtoto kwa kumuongelesha na pia kumgusa ama kwa kumshika-shika au hata kumbusu. Cheza naye, michezo ipo ya aina mbalimbali kutegemea na umri wa mtoto. Yaani tangu siku sifuri hadi miaka 5 cheza naye kwa sana na msisitizo mkubwa ni kwa kipindi hicho cha umri wa miaka miwili. Fahamu pia kwamba unaanza kucheza na mtoto angali akiwa tumboni. ^CS
 
Back
Top Bottom