1) Unaongelea Mungu yupi?
MUNGU Wa Israeli anasema dhambi ni uvunjaji wa sheria.
Kama ni huyu unayemuongelea, nionyeshe aliposema "dhambi ni kutokujua neno la MUNGU."
"Kila mtu atendaye dhambi anavunja sheria ya Mungu, maana dhambi ni uvunjaji wa sheria."
1Yohana.3.4.BHN
2) Nitakuonyesha aliposema kuna watu ingawa hawajui sheria za MUNGU, kwa asili wanafuata sheria za MUNGU, dhamiri zao zinatoa ushuhuda juu ya sjeria za MUNGU, kwasababu MUNGU ameziandika sheria zake kwenye mioyo ya binadamu:
"Mathalani: Watu wa mataifa mengine hawana sheria; lakini kila wanapotimiza matakwa ya sheria wakiongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa kipimo cha sheria ingawa hawaijui sheria.
Mwenendo wao unaonesha kwamba matakwa ya sheria yameandikwa mioyoni mwao. Dhamiri zao zinashuhudia pia jambo hilo, maana fikira zao mara nyingine huwashtaki, na mara nyingine huwatetea."
Waroma.2.14-15.BHN