Je, wajua Wakristo huwasindikiza Waislamu Kufunga Ramadhan? Leo ni Jumatano ya Majivu, Wakristo tutafunga siku 40, vipi Waislamu Mtatusindikiza?

Wanabodi

Hili ni bandiko la swali kuwa

Jee wajua kuwa sisi Wakristo huwa tunanawasindikizaga ndugu zetu Waislamu kufunga swaumu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan?. Leo ni Jumatano ya​


Paskali.
Kufunga Kiislamu mdomo lazima ubaki mkavu usipake mafuta ili uonekane umefunga, uso unatakiwa kuonyesha huzuni or being serious all the time.


hiyohapana Pasco.
 
Kufunga Kiislamu mdomo lazima ubaki mkavu usipake mafuta ili uonekane umefunga, uso unatakiwa kuonyesha huzuni or being serious all the time.


hiyohapana Pasco.


Endeleeni kudanganyana. Kwani nani asiejua kua ikifika kipind flan waislam wanatakiw kufunga na ni lazima. Mradi awe na akili timamu na awe balegh, bila fharura nyingin yyt.
Nyi mnadanganyana sana yan
 
Kama walikula IDD ina maana walifunga Kwa utaratibu huu huu wasioutaka,wakaacha maelekezo wakafuata ya kwao,

Hosea 9:5
"Mtafanya Nini katika siku ya mkutano wa IDD na katika siku ya karamu ya bwana"
 
Kama walikula IDD ina maana walifunga Kwa utaratibu huu huu wasioutaka,wakaacha maelekezo wakafuata ya kwao,

Hosea 9:5
"Mtafanya Nini katika siku ya mkutano wa IDD na katika siku ya karamu ya bwana"
Sasa nyinyi mna Idd ??tuanzie hapo kwanza
 
Uislamu ni zao la Ukatoriki! Ni Mapacha katika ulimwengu wa roho! Ndiyo maana karibu taratibu za Ibada zao zinafanana,(Walawi26:1)! Kwa hiyo Waislamu na Wakatoriki si vibaya wakisindikizana!
 
Msingi wa Uzi wako mkuu ni kama vile unasema Funga ya waislamu ni ya Kinafiki zaidi kuliko ile ya wakiristo vile.
Kwa mujibu wa Biblia
Mathayo 6:16-18
Neno la: Bibilia Takatifu
Mafundisho Kuhusu Kufunga
16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao.
17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu
18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.”

Lakini ujuwe kuwa Waislamu hatufungi kwa kufuata mafundisho ya Biblia wala Vigezo vyenu.laa ,bali Qur-an Tukufu ndiyiyo inatuongoza.

Qur-an Sura ya 2
2:183. Enyi mlio amini! (Waislamu) Mmeandikiwa Saumu (Ya Ramadhan), kama waliyo andikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kumchamngu.


2:184. (Mfunge) siku maalumu za kuhisabika. Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini. Na atakaye fanya wema kwa kujitolea, basi ni bora kwake. Na mkifunga ni bora kwenu, kama mnajua. 184


185. Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru. 185


186. Na waja wangu watakapo kuuliza khabari zangu, waambie kuwa Mimi nipo karibu. Naitikia maombi ya mwombaji anapo niomba. Basi na waniitikie Mimi, na waniamini Mimi, ili wapate kuongoka. 186


187. Mmehalalishiwa usiku wa Saumu kuingiliana na wake zenu. Wao ni vazi kwenu, na nyinyi ni vazi kwao. Mwenyezi Mungu anajua kwamba mlikuwa mkizikhini nafsi zenu. Kwa hivyo amekukubalieni toba yenu na amekusameheni. Basi sasa changanyikeni nao na takeni aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu. Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Saumu mpaka usiku. Wala msichanganyike nao, na hali mnakaa Itikafu msikitini. Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikaribie. Namna hivi Mwenyezi Mungu anabainisha Ishara zake kwa watu ili wapate kumcha.



Kwa Muongozo Huu hapo juu sioni mfanano na ule wa Kibiblia isipokuwa lile neno Swamu tu.
Huenda Wakiristo wangelielewa maana ya Neno ''WALIOKUWA KABLA YENU '' basi wangelifuata mfungo wa kiislamu.
Maana Huu umeboreshwa na klupunguziwa uzito kwa viumbe.
 
ukishajua kuwa ukristo ulianza karne ya kwanza kisha uislamu ukaanza karne ya saba....utajua nani humsindikiza mwenzake
 
Kama walikula IDD ina maana walifunga Kwa utaratibu huu huu wasioutaka,wakaacha maelekezo wakafuata ya kwao,

Hosea 9:5
"Mtafanya Nini katika siku ya mkutano wa IDD na katika siku ya karamu ya bwana"
JE KUNA SIKUKUU YA IDI KWENYE BIBLIA?

SWALI: Je! Karamu za ‘Idi’ ndio zipi hizo tunazozisoma katika Hosea (12:9)

Hosea 12:9 Lakini mimi ni Bwana, Mungu wako tangu ulipotoka katika nchi ya Misri; nitakukalisha tena katika hema, kama siku za KARAMU YA IDI.

JIBU: Tofauti na inavyodhaniwa hapo, na watu wa dini tofauti, kwamba Biblia inazitambua sherehe za kiislamu!. Jambo ambalo si kweli.

Ni vizuri kufahamu kuwa lugha yetu ya Kiswahili imetohoa maneno mengi sana kutoka katika lugha ya kiharabu, hata wakati ambapo biblia inatafsiriwa katika Kiswahili ilifuata mkondo huo huo. Kwamfano Sehemu nyingine utaona neno “shehe” likitajwa (1Samweli 5:8), na hapa unaona pia Neno “Idi” .

Kulingana na lugha ya kiharabu neno IDI, linamaanisha “Sherehe”. Haijalishi ni sherehe ya aina gani, inaweza ikawa ni ya kidini au ya kitaifa, au ya kitamaduni, au ya kimuungano..

Hivyo imezoeleka na watu wengi wasioilewa lugha ya kiharabu kudhani kuwa Idi ni neno la sikukuu ya kiislamu, kumbe sio.

Katika biblia ya kiharabu, mahali popote, kulipotajwa sherehe ya kiyahudi, Neno Idi liliandikwa pale. Mfano, palipoandikwa sikukuu ya pasaka, iliandikwa “idi ya pasaka” n.k..

Hivyo, hatushangai na Neno hilo kuonekana katika baadhi ya vifungu kwenye biblia. Hiyo yote ni kwasababu lugha yetu ya Kiswahili, imeundwa kutoka katika lugha nyingi mbalimbali. Kwahiyo inayozungumziwa hapo sio sikukuu ya kiislamu, bali ni sikukuu ya vibanda, ambayo wana wa Israeli walikuwa wakiisheherekea kwa katika vibanda pindi walipokuwa jangwani.

Bwana akubariki.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwislamu hawezi kumsindikiza mkristo kufunga,abadan(kamwe)

Sunagogi ni misikiti ya wayahudi,angalia kamusi ya biblia nyuma.

Nia yangu hapa ni kukupiga msasa kuwa yesu hakua Kristo.

View attachment 2526017
Katika tafsiri ya Biblia Union Version yapo maneno kadha wa kadha yenye asili ya lugha ya Kiarabu na Kiswahili cha kimvita hii ina tokana na mfasili(Mmisionary) wa kwanza aliye tafsiri biblia kumshirikisha mzee (Shekhe) ili aweze kusaidiana naye katika kazi hiyo iliyo onekana kuwa ngumu kwake kutokana na kutojua vizuri Kiswahili hivyo ndiyo maana utakuta maneno mengi yenye asili ya Kiarabu ndani ya Biblia (Tazama Mifano). Mashekhe kwa maana ya wazee, Kadhi kwa maana ya hakimu, Iddi kwa maana ya Sikukuu, kutawadha kwa maana ya kunawa miguu na kadhalika



Pamoja na hayo alipo tafsiri neno hili Sinagogi kuwa ni msikiti haku tafsiri kwa kuzingatia utalaamu wa lugha bali alifananisha mambo Fulani Fulani yanayo tendeka katika majengo hayo mawili yaani Sinagogi na Msikiti na ndipo akafasiri kuwa Sinagogi ni Msikiti wa Wayahudi kwa kulinganisha baadhi ya matendo yanayo fanana baina ya majengo hayo mawili.



Ni sawasawa na leo mtu kumwambia babu yake kuwa Computer ni Runinga ya kisasa wala kamwe hana maana ya Computer ni TV ila amechukua anachokifahamu mhusika ili kumweleza kitu au jambo Fulani. Hivi na sawa na mjaluo wa ugenya kusilimu kisha akirudi huku nyarigunga kavaa kanzu yake akiulizwa vipi kulikoni? Anasema “Siku hizi mimi naenda ile kanisa ya Waislamu” .



Hieleweke pia lugha yeyote ile iliyohai uzidi kuimalika . Ndivyo ilivyo na Kiswahili pia. mathalani leo tunayo maneno mengi yamezalishwa ambayo kimsingi miaka michache hayakuwepo kwenye kiswahili



Aina ya tafsiri iliyotumika kitaaluma

Kwa kadri ya taaluma ya Kiutafsiri mtafsiri huyo wa Biblia ametumia moja kati ya aina kuu mbili za kiutafsiri ambapo aina ya kwanza ni ile ya tafsiri “Shabihifu” na ya pili ni tafsiri “Maanifu”.



Hivyo kimsingi katika kutoa maana hiyo ya Sinagogi- Msikiti wa Wayahudi. msaidizi huyu katika utafsiri wa Biblia alionekana kukosa namna ya kulieleza neno hilo sinagogi na ndipo akaadhimu kutoa tafsiri hiyo ambayo kitaaluma siyo tafsiri “Maanifu” (haiendani na asili ya neno katika lugha husika) bali alitumia tafsiri “Shabihifu” inayozingatia mambo machache yanayofanana baina ya vitu viwili ndiyo maana alisema ni Msikiti wa Wayahudi hivyo kamwe hakusema kuwa ni Msikiti wa Waislam maana alitambua kuwa katika wakati huo bado uislam haukuwa umeanzishwa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyoingia katika sunagogi.
SURATIL BAQARAH AYA YA 65 NA YA 66, inayosomeka hapo chini


65. “NA HAKIKA MLIKWISHA YAJUA YA WALE MIONGONI MWENU WALIO IVUNJA SABATO,(SIKU YA MAPUMZIKO, JUMAA MOSI) NA TUKAWAAMBIA: KUWENI MANYANI WADHALILIFU”



66. KWA HIVYO TUKAYAFANYA HAYO KUWA ONYO KWA WALE WALIO KUWA KATIKA ZAMA ZAO NA WALIO KUJA BAADA YAO, NA MAWAIDHA KWA WACHAMNGU.


AYA ZOTE HAPO JUU ZIMESADIKISHA AMRI YA MWENYEZI MUNGU KUHUSU TAADHIMA YA SABATO.


4. TAURATI KAMA KIPAMBANUZI CHA QURAN


SURATI (21:48) “NA KWA YAKINI TULIWAPA MUSA NA HAARUNI KIPAMBANUZI, NA MWANGAZA, NA MAKUMBUSHO KWA WACHAMNGU,”


5. TAURATI KWA UONGOFU WETU

SURATIL BAQARAH AYA YA 53 (2:53) “NA TULIPO MPA MUSA KITABU NA PAMBANUO ILI MPATE KUONGOKA”


Tunasimamia hapa kwa kusema aya ndani ya Mhubiri 12:13 , 14 inayosema

“13. Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. 14 Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.”


2 TIMOTHEO 3:16

“Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;”



54 SURAT AL QAMAR 52 na 53 “Na kila jambo walifanyalo limo vitabuni, Kila kidogo na kikubwa”



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku ya sabato ni ipi,?
Hebu sasa twende mbele zaidi, ili tuweze kuifahamu hasa siku hiyo ambayo mwenyezi mungu hakufanya kazi yeyote maandiko ya Qur-an yataendelea kutusaidia katika Jambo hili-



Qur-an Surat A-NISAA 4:154 na tukanyanyua mlima juu yao[hao

Mayahudi] kwa kufanya Agano nao [la kufuata

taurat] na tuliwaambia"Liingieni lango [la

nchi ya shamu]" hali ya kuinama {kama

mnafukuu] [wakapinga]. Na [pia] tukawaambia;

"msiruke mipaka kwa [kuvunja taadhima ya]

Jumamosi" na tukachukua ahadi iliyo madhubuti

kwa mambo hayo na mengineyo wala wasitimize.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilijua utakuja na jibu la sampuli hii ambalo mnajifichia pale panapowashinda.

Kunradhi,,,ule msikiti pale Jerusalem ulijengwa kipindi kipi?
 
Ha haaa,,,ulinyanyuliwa mlima juu ya vichwa vyao wakaambiwa mnafata ya Mwenyezi Mungu au la?

Wakafua Kwa muda baadae wakarudi Kule Kule.[emoji1787]
 
Uislam siyo dini ya "rituals", Uislam ni mfumo kamili wa maisha. Hatujifanyii mambo yetu kwa matamanio yetu. Kila linalohusu maisha yetu ya kila siku lina taratibu zake.

Katika Uislam hatuna hukum Ya kusindikizana kwenye funga. Funga ya Kiislaam ina funga za faradhi (compulsory) na kuna funga za sunna, zote zimeainishwa.

Hatuna funga ya Kusindikizana na mfungo wa Kikristo au wa imani nyengine yoyote ile.
 
Uislam siyo dini ya "rituals", Uislam ni mfumo kamili wa maisha. Hatujifanyii mambo yetu kwa matamanio yetu. Kila linalohusu maisha yetu ya kila siku lina taratibu zake.
Asante sana kwa ilmu hii
Katika Uislam hatuna hukum Ya kusindikizana kwenye funga. Funga ya Kiislaam ina funga za faradhi (compulsory) na kuna funga za sunna, zote zimeainishwa.
Asante pia kwa ilmu hii
Hatuna funga ya Kusindikizana na mfungo wa Kikristo au wa imani nyengine yoyote ile.
Simaanishi kusindikizana kufunga kwa ibada bali kusindikiza huku nimeisha. Mimi ni Mkristo, nimesoma chuo TSJ na Muislamu Abubakar Liongo, tumelala chumba kimoja. Wakati wa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, nikajikuta na mimi nafunga kumsindikiza!.
Kikawaida kufunga sita ni kwa wanawake, lakini nawajua wanaume wa Kiislamu wanaofunga 6 kwa sunna tuu kuwasindikiza wake zao wanaofunga 6 kwa faradhi!.

Hili ni bandiko la swali
Wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, sisi tunakusindikizeni, jee kuna ubaya nanyi mkitusindikiza?.
P
 
Hiyo ndio dini ya haqi,Fanya maamuzi mapema ndugu.View attachment 2625969


JE ANAYESEMA ATAWAZAA HAPA DUNIANI NA KUWAPOTEZA WOTE NI NANI??????

Quran 15:39.
Akasema :mola wangu mlezi! Ilivyokuwa imenitia makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa Duniani na nitawapoteza wote.


HUYU ANAYESEMA ATATUZAENI WAISLAMU NA KUTUPOTEZA WOTE NI NANI????


Shetani hakuwafīcha kuwa anawapeleka motoni


وَإِن مِّنكُمْ إِلَّا وَارِدُهَا ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتْمًا مَّقْضِيًّا

[ MARYAM - 71 ]
Na hakuna yeyote katika nyinyi ila mwenye kuifikia jehannam Hiyo ndiyo hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe.

allah mwenyewe makazi yake ni motoni!

Sahih al-Bukhari 4848
Narrated Anas:
The Prophet (ﷺ) said, "The people will be thrown into the (Hell) Fire and it will say: "Are there any more (to come)?' (50.30) till Allah puts His Foot over it and it will say, 'Qati! Qati! (Enough Enough!)'"
حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ أَبِي الأَسْوَدِ، حَدَّثَنَا حَرَمِيٌّ، حَدَّثَنَا شُعْبَةُ، عَنْ قَتَادَةَ، عَنْ أَنَسٍ ـ رضى الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ يُلْقَى فِي النَّارِ وَتَقُولُ هَلْ مِنْ مَزِيدٍ‏.‏ حَتَّى يَضَعَ قَدَمَهُ فَتَقُولُ قَطِ قَطِ ‏"‏‏.‏
Reference : Sahih al-Bukhari 4848
In-book reference : Book 65, Hadith 369

Kama anaebishia allah sio maskani yake motoni atuwekee ushahidi aliutoa mguu wake motoni lini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…