Wanabodi
Hili ni bandiko la swali kuwa
Je, wajua kuwa sisi Wakristo huwa tunanawasindikizaga ndugu zetu Waislamu kufunga swaumu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan? Leo ni Jumatano ya Majivu, Wakristo tunaanza safari ya kufunga kwa siku 40, vipi nyie wenzetu Waislamu, je mtatusindikiza kama ambavyo sisi tunavyo wasindikizaga?
Leo ni siku ya Jumatano ya Majivu, Ash Wednesday ambayo ni kisheria cha mwanzo wa kufunga siku 40 kwa Wakristu kote duniani kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyofunga siku 40 Jangwani kabla ya kusulubiwa kwa mateso, na kufa msalabani siku ya Ijumaa Kuu ambapo Jumapili Alfajiri alifufuka katika wafu, akakaa na sisi duniani kwa siku 40 nyingine kisha akapaa mbinguni. Toka huko atarudi tena kwa utukufu kuwahukumu wazima na wafu na ufalme wake hautakuwa na mwisho.
Naomba kulianza bandiko hili lina sehemu 3.
- Sehemu ya kwanza ni sala ya Kanuni ya Imani
- Sehemu ya Pili ni Maana ya Jumatano ya Majivu
- Sehemu ya Tatu ni Mastori ya Pasco na Umuhimu wa kufunga.
Sehemu ya Kwanza
Sala ya Kanuni ya Imani
Amina.
Sehemu ya Pili
Maana ya Jumatano ya Majivu, hii ni C&P
Kutoka
IFAHAMU JUMATANO YA MAJIVU
UTANGULIZI
Sehemu ya Tatu: Mastori ya Pasco
Dini mbili Kuu duniani ni Wakristo na Waislamu, hakuna sensa yoyote iliyowahi kufanyika duniani kuestablish Wakristu ni wangapi na Waislamu ni wangapi hivyo hakuna data nani ni wengi zaidi ya wengine. Kwa Tanzania enzi za sensa za mkoloni waliwahesabu hadi makabila na dini, kuna wakati Waislamu wslikuwa wengi Tanganyika baadaye Wakristu wakawa wengi, tulipuungana na Zanzibar na kwa Tanzania, sensa ya mwisho yenye swali la dini Waislamu wakawa wengi.
Baada ya hapo Mwalimu Nyerere akafuta maswali ya udini, sensa zote zilizofuatia hakuna tena kujua idadi nani ni wengi, ila baada ya Awamu ya kwanza zikaanza kelele za marginalisation ya dini fulani mara, mara ... kwa vile hili sii jukwaa la siasa hayo tuyaache ila sio wengi wanaofahamu kuwa Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba Mmoja, Ibrahim na Sheria ya Mungu kwa hizi dini zote mbili Wakristo na Waislamu ni sheria moja ile ile ya Musa amiliyoshushwa kwenye Kitabu cha Kumbukumbu la Torati ndani ya Biblia Takatifu na Tourat ndani ya Quran Tukufu, na si wengi wanafahamu kuwa Yesu Kristo wa kwenye Biblia aliyezaliwa na Bikira Maria kwa kupata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ndiye yule yule Nabii Issa Bin Maryam wa kwenye Quran Tukufu.
Hili la Wakristu na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja, Jielimishe zaidi hapa
"Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu za Kufanya Miujiza ya Uponyaji kwa Imani. Kila Mtu Anazo!
Ndipo nikagundua kufunga kuna faida nyingi, achilia kufunga kwa ibada, kufunga hata bila ibada ni very beneficial to the body. Mwili unapumzika kufanya metabolism wakati wote hivyo kurelax na kufanya detoxification kuondoa sumu mwilini.
Tofauti ya Kufunga Kikistu na Kiislamu.
Kama nilivyo eleza mwanzo Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, na sheria ya Mungu ni sheria moja ile ile ya Musa, Waislamu wanaendelea kuifuata kama ilivyo, Kiislamu kufunga ni nguzo ya Kiislamu ni lazima.
Yesu alipokuja, hakuja kuitengua Tourat ya Musa, amekuja kuikamilisha, hivyo kufunga Kikistu sio lazima ni unapojisikia.
Kufunga kwa Waislamu ni hakuna kula chochote unakaa na njaa kuruhusiwi hata kunywa maji, ila rukhsa kumeza mate, kufunga kwa Wakristo ni ukozidiwa njaa, unaweza kula kidogo, ukizidiwa kiu unaweza kunywa kidogo.
Kufunga kwa Kiislamu ni kufunga kula tuu kunywa na kutokufanya dhambi ikiwemo kumega 'tunda!' kwa wenye ndoa zao baada ya kufuturu, unashushia chakula cha usiku ikiwemo kumega tunda!. Kufunga kwa Wakristo unaweza kufunga kitu chochote lakini starehe zote haziruhusiwi ikiwemo kumega 'tunda', hakuna cha wenye ndoa zao wala cha nini!, ndio maana wakati wa kipindi cha kwaresma hakuna sherehe yoyote wala ndoa yoyote ya Katoliki maana haiwezi kuwa consummated!
Kufunga kwa Kiislamu ni kufunga tuu chakula, lakini kufunga kwa Wakristo kuna room ya selectivity unachagua kufunga tuu kunywa pombe, au kuvuta sigara au starehe yoyote, mfano kwenda out, kufunga muziki, kufunga kuagalia TV, kufunga mitandao ya kijamii etc.
Kufunga kwa Waislamu kufungulia kunaitwa kufuturu na kunaendana na kuchomoza kwa jua ndio mwanzo wa kufunga na kuzama kwa jua ndio time ya kufuturu, kufunga kwa Wakristo hawana muda maalum wa kuanza wala muda maalumu wa kufungua na kufuangua kwetu hakuitwi kufuturu.
Kufunga kwa Waislamu kuna muda wa kula daku lakini kufunga kwa Wakristo hakuna daku, hivyo kuna baadhi ya Waislamu kwao mwezi mtukufu ni kubadili tuu masaa ya chakula cha milo mitatu, badala ya kula breakfast asubuhi lunch mchana na dinner usiku, ni breakfast anakula saa 12:30 jioni, wakati wa kufuturu, lunch anakula saa 5:00 usiku baada ya tarawea na dinner anakula saa 10:00 alfajir hivyo mchana wake ndio unakuwa usiku na usiku ni mchana.
Kufunga Kiislamu ni hadharani watu wote lazima wajue umefunga na ukikaribishwa chakula popote unasema uko kwenye swaumu, kufunga Kikistu ni siri, huruhusiwi kumwambia mtu yoyote kuwa umefunga na ukikaribishwa chakula popote unasema tuu asante, uko ok bila kusema umefunga.
Kufunga Kiislamu mdomo lazima ubaki mkavu usipake mafuta ili uonekane umefunga, uso unatakiwa kuonyesha huzuni or being serious all the time. Kufunga Kikistu unatakiwa kupaka mafuta mdomoni ili watu wasijue, kuwa umefunga, unatakiwa ku smile wakati wote na kuonyesha furaha na sio huzuni au kukunja uso.
Kufunga kwa Kiislamu ukifika muda wa kufururu ni lazima ufungulie na kufuturu na hakuna kufunga siku ya Idi, kufunga kwa Wakristo ni sio lazima kufungulia ukiweza kufunga two days, three days, 7 days, 40 days kama Yesu, unafunga. Unaweza kufunga foods only ukawa unakunywa maji tuu, hii inaitwa water fast, unaweza kufunga vyakula vyote ukawa ùnakunywa fresh juice only, inaitwa juice fast, unaweza kufunga vyakula vya nyama na starch ukawa unakula mboga mboga only, na kwa wale wanaofunga na ku meditate kuna wanaofunga kila kitu na kula hewa tuu, yaani breath, hawa wanaitwa, breathpeteriann wanafunga na kula hewa tuu!. Hawa ni ma master with full body control hakuna kuingiza kitu mwilini na hawatoi kitu mwilini wanakuwa wame stop all bodily metabolism processes hata chooni hawaendi wala perisperision process inakuwa stopped!
Wakati wa Mwezi Mtukufu wa Radhani Waristo Tunawasindikiza Waislamu, Vipi Wenzetu Kwaresma, mtatusindikiza?
Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan baa na clubs hazijai, hata sisi Wakristo kwa kutambua wenzetu Waislamu wamefunga, sisi nasi tunapunguza starehe, baadhi ya bendi za muziki wa dansi zinakuwa likizo hazi perform.
Hata sisi Wakristo walaji wa kitimoto, wakati wa mwezi mtukufu tunapunguza kula mauzo yanashuka.
Hata sisi Wakristo tunatumia zile bidhaa za wale wadada zetu wa ile biashara ya usiku, tunapunguza kununua, hivyo bidhaa zinawadodea, hivyo hata wadada Kikristu hawapeleki bidhaa sokoni!
Je, Kwaresma Ina Hadhi Sawa na Ramadan?
Je wajua kuwa ni mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadan tuu ndio unao fahamika rasmi kiserikali na kitaasisi mbalimbali utasikia viongozi wa kisiasa, kiserikali, taasisi na watu mbalimbali wakifuturisha, huku nyumba za matajiri zikifurika masikini kila Ijumaa ambapo matajiri hao hutoa sadaka kwa masikini, lakini kiukweli Kwaresma ni kama haitambuliki rasmi!, sijawahi kusikia ikizungumzwa popote hivyo Kwaresma ni ipo kama ipo ipo na funga yetu sisi Wakristo kuonekana kama funga zuga!, why funga ya Wakristo haipewi Umuhimu kama funga ya Waislamu?.
Ndugu Zetu Waislamu, Mtatusindikiza?
Vipi ndugu zetu Waislamu, sisi ndugu zenu wa baba mmoja Wakristo leo tumeanza mfungo wa Kwaresma ambapo tunafunga siku 40, vipi mtatusikiziza kama sisi tunavyowasindikizaga?
Nakutakia Kwaresma Njema.
Paskali.